Hivi kuna watu wamechagua ualimu wa arts?

Habari zenu wana jukwaa nimesikitika kuona utitiri wa madogo bado wanaigombania BAED hivi wameyasikia matangazo kweli ya mkulu
Kwa nini usomee course ya unemployment?
Kwa nini watu hawana vision?
Ualimu ni zilipendwa madogo

Kwa jinsi ninavyojua humu JF kuna Walimu ' Kibao ' wamejazana nakuomba tu Mkuu anza kujiandaa Kisaikolojia kwani kama vile nayaona majibu yao ' choma / umiza ' watakayokuja nayo kukujibu. Kuwa tu mvumilivu ila najua hawatakuacha hivi hivi.
 
Kwa jinsi ninavyojua humu JF kuna Walimu ' Kibao ' wamejazana nakuomba tu Mkuu anza kujiandaa Kisaikolojia kwani kama vile nayaona majibu yao ' choma / umiza ' watakayokuja nayo kukujibu. Kuwa tu mvumilivu ila najua hawatakuacha hivi hivi.
Sasa majibu yao yana hasara gani wana stress nyingi hao
 
Nimesoma HGL na ufaulu wangu unanirusuhu kusoma BAED . Mtaani kugumu jamani ngoja nikale Boom kwa miaka mitatu walau wazazi wangu niwapunguzie utegemezi. Baada ya kumaliza kozi nitafanya kazi yeyote ya kujiajiri, sio lazima nifanye kazi ya ualimu. BAED ina kozi nyingi ndani yake.
Nawasilisha!
 
Watu wameomba BAED wakidhani labda kauli zitabadilishwa yaan Kana kwamba, kauli ilikosewa au huwenda wanalidhani labda mpka wamalize huenda sera itabadilishw Kwa upande wa walimu wa arts.

Ila Kwa mtu mjanja lazma asome nyakati kua Kwa sasa kulikua hakuna haja ya walimu wa arts tena maana mashuleni intact wamejaa kama utitiri kiasi kwamba wanagawana topics tu na wanahudhuria Mara moja Kwa wiki tu alafu cha ajabu wanalipwa mshahara sawa na mwalimu wa sayansi.

Nasikitishwa na ambao wanabeza et mbona hata laws ipo ivo sijui BBA : sasa ngoja nikuibie siri mwanasheria anauwezo wa kuja kujiajiri katika sheria yake na pia BBA anaweza akaanzisha business yake kubwa tu na kuiendesha kitaalamu zaidi.

Sasa wewe mwenzangu na Mimi eti ukisema utakuja kujiajiri ajira nyingine nje na ualimu aisee it is a loss , kulikua hamna haja ya kufungua biashara mpka upate BAED utakua umepoteza Muda.
Kwasasa najua mtakasirika sana Ila subirini mmalize shule ndo itajulikana
 
Kwani mkuu ukisoma Baed nilazima ukawe mwalimu????

Sasa mkuu kuna haja gani ya kusoma hiyo kama huendi kuitumia taaluma yako, utakua umepoteza Muda wako tu. Ni bora ungefanya mambo mengine tu kama hautokuja kuwa mwalimu. Ada zote zile gharama za kila namna ni bora ungefanya hiko kitu kingine unachokifikiria mbali na ualimu. Au una lengo la kumiliki degree haijalishi ni ipi
 
Sasa wee kilaza yaani umeskia kabisa serikali imesema haiajiri waalimu wa sanaa alfu mtu bado unaomba na unajua fani hii inategemea Ajira ya serikali 96%
Tatizo ni kuwa watu wanategemea ajira ya serikali tu! Unaweza kuanzisha shule yako ya awali na maisha yakasonga mbele! Mnaweza kujiunga Wa masomo mbalimbali mkaanzisha tuition centre ya nguvu na maisha yakasonga mbele!
 
Back
Top Bottom