Hivi kuna watu kweli wamenunua hisa za Vodacom?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,898
43,806
Kuna maswali huwa najiuliza bila majibu. Hivi kama kampuni ina jumla ya thamani ya shillingi Billion kumi, na ina jumla ya hisa 10 ( kila hisa ina thamani ya bilioni 1). Na hiyo kampuni kwa makusudi kabisa ikaamua kununua shamba lenye thamani ya million 500 kwa gharama ya billion 5, inamaana hisa hizo 10 kiuhalisia zina thamani ya bilioni 5.5 na sio bilioni 10 kama madaftari yanavyoonyesha. Sasa siku ya siku kila mtu atakapodai chake na kumbe pesa zilizopo ni pesa hewa, ndio mtakapo lia na kusaga meno.
====================================
UPDATE: 12/07/2017
Taharuki Airtel ipo 25 bilioni huku Vodacom ni 476, Vodacom wali overprice thamani yao
Airtel wameanza maandalizi ya kuingia katika soko la hisa huku wakii value kampuni yao kwa 100 bil ambayo naona ni sawa kabisa na uhalisia.

Wale wenzangu voda waliosema vodacom ina thamani ya tril 2 yaani thamani yao ni mara 20 ya airtel , wakaingia soko ya hisa wakaweka mathamani makubwa yasihakisi uhalisia mpaka watu wakashindwa kununua hisa , sasa watanzania mmejionea voda walivofanya makusudi mpaka kupelekea waziri mpango kubadili sheria kuruhusu watu wa nje kununua hisa ambao watakuja kununua hao hao wamiliki wa voda.

Airtel nawapongeza. Voda wamechukua pesa zetu wamekaa kimya
=====================================
UPDATE: 01/11/2017
Pendekezo la gawio la hisa za Vodacom, najuta kununua hisa za Vodacom
=======================================
UPDATE: 29/01/2018
Wawekezaji VodaCom wapoteza bilioni 350Tsh
Wawekezaji wa kampuni ya simu za mkononi ya VodaCom Tanzania wapoteza mtaji wa Sh350 bilioni katika kipindi cha miezi mitano tangu kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE)

Chanzo: MWANANCHI
================================
Update: 25/09/2019

=============================
Update: 30/01/2020
Bunge limeagiza uchunguzi ufanyike uuzwaji wa hisa za vodacom

==============================
Update: 17/11/2020

=======================
Update: 03/07/2022
 
Kuna maswali huwa najiuliza bila majibu. Hivi kama kampuni ina jumla ya thamani ya shillingi Billion kumi, na ina jumla ya hisa 10 ( kila hisa ina thamani ya bilioni 1). Na hiyo kampuni kwa makusudi kabisa ikaamua kununua shamba lenye thamani ya million 500 kwa gharama ya billion 5, inamaana hisa hizo 10 kiuhalisia zina thamani ya bilioni 5.5 na sio bilioni 10 kama madaftari yanavyoonyesha. Sasa siku ya siku kila mtu atakapodai chake na kumbe pesa zilizopo ni pesa hewa, ndio mtakapo lia na kusaga meno.
Jiepushe sana kujifanya unajua jambo usilolijua hii itakujengea heshima.
Kama hujui kitu ni afadhali ukauliza siyo kujifanya unajua.
Na kwa taarifa yako vodacom hawakuwa na huo mpango wa kuuza hisa ila tu ni sheria iliyopitishwa na bunge letu kuyataka makampuni ya simu yauze 25% kwa watanzania.
 
Natamani kufundishwa kuhusu masuala ya hisa. Nilijifunza kidogo kupitia makala ya The bold (THE KINGS MAKERS) nilielewa kidogo call options na put opitions.
Ki uhalisia sifahamu kabisa masuala ya Hisa hata hii thread yako nimeshindwa kuelewa nini maana ya hisa,kwa nini zinauzwa, faida na hasara, mnunuaji ananufaika vip n.k
 
acha uongo nani kakudanganya CHADEMA mna gubu sana ungejua tu Sumaye ana hisa za kutosha CRDB..........thamani ya hisa inatokana na performance ya kampuni husika kampuni ikipata faida kubwa na thamani ya hisa inaongezeka ndio maana thamani ya hisa za CRDB zimeshuka sana kwa sababu ya poor performance ya benki .
 
Jiepushe sana kujifanya unajua jambo usilolijua hii itakujengea heshima.
Kama hujui kitu ni afadhali ukauliza siyo kujifanya unajua.
Na kwa taarifa yako vodacom hawakuwa na huo mpango wa kuuza hisa ila tu ni sheria iliyopitishwa na bunge letu kuyataka makampuni ya simu yauze 25% kwa watanzania.
1.) Sijasema najua, nimetangulia kwa kusema "najiuliza", au ni kosa kujiuliza na kutafakari juu ya jambo?

2.) Ndicho wanachotaka muamini, kama ni kweli hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuwanufaisha watz basi isingepitishwa bungeni, hao voda hawashindwi kuhonga hao wachumia tumbo na muswada unagonga mwamba. Hao Voda watakuwa na financial problems tu, sio bure, na wengi mtaingizwa mkenge, tusubiri tuone hii DECi a.k.a Kamari itakapowafikisha.
 
Na hajui kuwa CHADEMA Wenzao kina LOWASSA, ROSTAM, Wamejitahidi kwa hali na mali kumtumia BASHE Kama MBUNGE apinge kwa nguvu zote sheria ya kuyalazimisha makampuni ya simu kuuza 25% ya hisa. Mijitu kama hii ndo huwa inauliwa kwenye maandamano baada ya kutangaziwa na mtu akiwa Sea Cliff huku familia yake iko DUBAI na DENMARK
Wamelazimishwa? Nasubiri kuona Tigo, Airtel, Zantel, Smart, TTCL wakijitangaza kwa NGUVU KUBWA sana kuuza hisa zao, au sheria hiyo imewalazimisha kutenga bajeti kubwa za matangazo? Mbona sioni TBL na wengine wakifanya promo za hisa namna hiyo?
 
Natamani kufundishwa kuhusu masuala ya hisa. Nilijifunza kidogo kupitia makala ya The bold (THE KINGS MAKERS) nilielewa kidogo call options na put opitions.
Ki uhalisia sifahamu kabisa masuala ya Hisa hata hii thread yako nimeshindwa kuelewa nini maana ya hisa,kwa nini zinauzwa, faida na hasara, mnunuaji ananufaika vip n.k
Google
 
Fafanua, nitashukuru
Yaani uwe tayari kutake risk..kwa maana bei za hisa huwa zinapanda na kushuka..sio bei za kukaa stable, pia kwenye ishu ya gawio ndio hivo.. kampuni husika ikipata hasara na gawio nalo hupungua..ukiweka hela nyingi na mambo yakajipa faida pia unapata... Mtaji wa hisa ni muhimu kuwa nao kama umedhamiria..

Pia, ununuzi wa hisa unakabiliwa na changamoto mbalimbali, kwa msaada zaidi wasiliana na mshauri wako wa masuala ya kifedha na uchumi..

(Nimeelezea kadiri ya uelewa wangu, natumai wengine watakuja kukuelewesha zaidi)
 
Nina uhakika tena pasi na shaka, hiza za voda zitashuka kwa 25% pindi watakapomaliza hili zoezi, (naota tu)
 
2.) Ndicho wanachotaka imuamini, kama ni kweli hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuwanufaisha watz basi isingepitishwa bungeni, hao voda hawashindwi kuhonga hao wachumia tumbo na muswada unagonga mwamba. Hao Voda watakuwa na financial problems tu, sio bure, na wengi mtaingizwa mkenge, tusubiri tuone hii DECi a.k.a Kamari itakapowafikisha.
Usibishane ili mradi tu... Siyo voda tu watakaouza hisa 25% bali makampuni yote ya simu yatafanya hivyo...
Tatizo kubwa la watanzania ni kila mtu kujifanya ni expert wa kila kitu na ndilo hata mkulu anafanya.
Always simple answers to complex matters with no research.
Kwanini biashara zinafugwa kariakoo, hao walikuwa wapiga deal hayo ndiyo majibu ya watanzania.
Kafanye research tena kwanini wanauza hisa wala hawakuwa na lengo la kuuza hisa zao.
 
Jiepushe sana kujifanya unajua jambo usilolijua hii itakujengea heshima.
Kama hujui kitu ni afadhali ukauliza siyo kujifanya unajua.
Na kwa taarifa yako vodacom hawakuwa na huo mpango wa kuuza hisa ila tu ni sheria iliyopitishwa na bunge letu kuyataka makampuni ya simu yauze 25% kwa watanzania.
Well said mjumbe
 
Yaani uwe tayari kutake risk..kwa maana bei za hisa huwa zinapanda na kushuka..sio bei za kukaa stable, pia kwenye ishu ya gawio ndio hivo.. kampuni husika ikipata hasara na gawio nalo hupungua..ukiweka hela nyingi na mambo yakajipa faida pia unapata... Mtaji wa hisa ni muhimu kuwa nao kama umedhamiria..

Pia, ununuzi wa hisa unakabiliwa na changamoto mbalimbali, kwa msaada zaidi wasiliana na mshauri wako wa masuala ya kifedha na uchumi..

(Nimeelezea kadiri ya uelewa wangu, natumai wengine watakuja kukuelewesha zaidi)

Sitaki kusikia kabisa habari za hisa baada ya nilichofanywa na wale NICOL!
 
Nachukia sana namna wanavyowaradicalise vijana wasiotumia akili zao na kuwaburuza wawezavyo.
Yaani katika vitu ambavyo nachukia sana dunia hii,

1.UMASIKINI

2.UGAIDI

3.CHADEMA
Kwa kweli na Mola aendelee kutuongoza na kutupa hekima na busara milele
 
Back
Top Bottom