Hivi kuna watu bado wanaamini wakiingia kwenye ndoa hawatasalitiwa milele?

Mission

Member
Feb 16, 2016
66
78
Matukio mabaya kuhusu ndoa yamekua mengi sana ambayo ni ya kufedhehesha na kudhalilisha. Najiuliza kuna watu wana matumaini ya kuishi kwenye ndoa bila kusalitiwa? Binafsi najua kusalitiwa kupo tu ila nisigundue na kusaliti kupo pia cha muhimu asigundue. Maana hata kama wote sio waaminifu atakayejulikana kwanza ana shida.
 
Ayubu 31:9-10 9. Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu; 10. Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, na wengine wainame juu yake.
 
Kwa mjibu wa Ayubu, ni sawa na kusema what goes around, comes around. Unachapa wake wa wengine, na wako anachapwa, hauchapi wa wengine na ni mwaminifu mbele za Mungu, Mungu atamlinda mkeo(rejea kisa cha Ibrahimu na mkewe Sarah wakiwa Misri pia wakiwa kwa Abimeleki).
 
Ila hauchapi wa wengine, lakini dhambi zinanuka mwili mzima(uko mbali na Mungu), mkeo atachapwa(maana hakuna wa kumlinda asichapwe nje).
 
Huwezi kumlinda binaadamu mwenzio, kusaliti au kusalitiwa hakuna formula
 
Mmmh mimi najiaminishaga na kujidanganya pekeyangu sintosalitiwa (maana sitaki mpando na mshuko wa sukari mwilini) japo ni msalitiii
 
DUH YATAKA MOYO KUAMINI KWAMBA SITASALITI AU KUSALITIWA NA HII INATOKANA NA UKWELI KWAMBA TUNAOWAPENDA KWA DHATI YA MOYO INATOKEA KUSHINDWA KUOANA NAO TUNAISHIA KUOA AU WENGINE KUOLEWA KWA SABABU YA UMRI NA KUTAFUTA HESHIMA TU. TUKIKUTANA NA VISHAWISHI NA MATAMANIO MAPYA TUNAWASALITI WANANDOA WENZETU.HOFU YA MUNGU TU NDIO DAWA TOFAUTI NA HAPO LAZIMA MMOJA WA WANANDOA ATAMSALITI MWENZIE COZ NI NGUMU KUPATA PAIR YENYE UWIANO SAWA WA KUPENDANA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom