Hivi kuna Watanzania wangapi wanajua madini ya Diamond,Gold na Tanzanite tuliyonayo yanapitia mchaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna Watanzania wangapi wanajua madini ya Diamond,Gold na Tanzanite tuliyonayo yanapitia mchaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nderingosha, Feb 6, 2012.

 1. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu nimebidi kuuliza hili jambo kwani nimekuwa nikijiuliza kwa muda mrefu kuwa sisi kama nchi mojawapo Africa yenye madini tajwa mengi ….lingekuwa ni jambo la kawaida kwa raia yoyote mtanzania kuelewa hatua kadhaa za uchambuaji wa haya madini na maandalizi yake kabla ya kuuzwa nje ya nchi ambako tunaambiwa yanatuletea pesa za kigeni.Nadhani kwa umuhimu wa madini haya kama vyanzo vya pesa za kigeni ningetegemea watanzania wengi haswa kuanzia ngazi za wanafunzi wangekuwa wanapata fursa za kutembelea migodi yetu na kujionea wenyewe utajiri wa nchi yao na jinsi mchakato mzima wa uchimbaji, uchambuzi na utayarishaji kabla ya kuuzwa ng’ambo unavyofanyika(kama ambavyo zamani watanzania walivyokuwa na fursa za kutembelea viwanda vyetu na kujifunza mambo kadha wa kadha kwa faida za kielimu …na maarifa…..mfano viwanda vya chuma,nguo…etc..).

  Nasema hivi kwa kuwa sioni ni kwanini hili lisifanyike na hata kama haliwezekani basi angalau watanzania wangepata fursa ya kuonyeshwa hata kwenye luninga jinsi madini haya ya almas, dhahabu na tanzanite yanavyopatikana ardhini,uchambuzi wake na hata maandalizi kabla ya kuuzwa ng’ambo.Nasema hivi kwa kuwa kwa kweli imeniuma sana wakati huu ambapo kuna hili kombe la mpira la mataifa ya Africa(AFCON)…ambalo linaonyeshwa live kwenye luninga za mataifa mengi barani Africa…..na moja ya kivutio kikubwa kwangu ni jinsi wenzetu wanavyojivunia kuonyesha matangazo ya raslimali zao za kiuchumi za Taifa…haswa kwenye sekta za madini na mafuta.Ukifatilia luninga nyingi utaona kuwa wanaodhamini matangazo yao ya TV live AFCON ni makampuni makubwa ya mafuta au madini(ukiondoa machache ya kampuni za simu)…Ukiangalia wenzetu wanavyofanya na ukaja tz unakuwa na maswali ambayo kwa kweli mi nashindwa kuyajibu na unabaki kuumia saana tu..

  Moja ya jambo lililonivutia wakati natizama AFCON kwa kupitia luninga ya Zimbabwe (ZBC)……kwa kweli ni jinsi wanavyoonyesha kampuni yao kubwa ya almasi inayoitwa Mbada Diamonds….ambayo ndiyo imedhamini matangazo yaoote…inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na serikali yao na ni kati ya makampuni makubwa ya almas Africa…...yaani wanaonyesha jinsi kampuni inavyowanufaisha raia kwa kuwajengea miundo mbinu,kuwapa vyakula n.k…….pamaja na yote pia wanaonyesha mchakato mzima wa uchimbaji na uchambuzi wa almasi kwa stage zote mpaka mwisho inapoenda sokoni…….mi nikajiuliza mbona TZ tuna makampuni mengi ya madini lakini hatujui kinachoendelea kule????yaani hata kwa TV hatuonyeshwi??What is this yaani?....haya makampuni ya madini tuliyonayo yanashindwa leo hii hata kudhamini matangazo ya michezo (e.g mpira)kwa TV?na sisi watanzania na vingozi wanayaona haya ya kawaida kweli??....inasikitisha saana…ukingalia nchi zote hata Gabon wanaonyesha AFCON kwa TV yao ya taifa na mdhamini ni kampuni yao kubwa ya mafuta……..leo hii tz haya makampuni ya gas tuliyo nayo na madini yanashindwa hata kudhamini michezo???alafu tunaona sawa kweli……hata juzi tumeona timu yetu ya wanawake(Twiga stars) ikikaribia hata kushindwa kushiriki mechi yao kisa kukosa udhamini wakati kuna mikampuni inachimba madini yetu wala hatujui kinachoendelea huko migodini…….hivi watanzania tumelogwa???au laana???....nina hakika watanzani walio wengi hawajui madini ya almas,gold na tanzanite yanafananaje kabla ya kuuzwa nje zaidi ya kuyaona kwenye picha….this is one of the very painful fact for Tanzanians …very unfortunately………
   
 2. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Sorry for the incomplete heading....bad that its impossible to modify headings after posting...please mods..make it look like..."Wangapi wanaelewa madini yetu yanapitia mchakato gani kabla ya kuuzwa nje"?
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  You have very interesting points. Ulichokisema kimenigusa sana, i would need sometime to digest before I comment anything.
   
 4. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu we wacha tu yaani ukifikiria kuna mambo yanafanyika nchi hii hata mwendawazimu anaweza akatushangaa.....yaani nimeandika hii post kwa hasira wakati naangalia mpira mpaka nimeshindwa kumalizia heading......ebu we fiikiria.....mtu unaangalia TV ya taifa ya zimbabwe free ambako unaona uwazi wa shughuli zao kwenye mgodi wao mkubwa wa madini ya almas...dunia nzima inaona hili.....wakati hapa TZ hiyo kitu hamna(haiwezekani)wakati Zimbabwe ndiko kunajulikana kuwa wanatawaliwa na dikteta(Mugabe).....hii itamwingia nani akilini????.....hizi ndizo changamoto ambazo zingatakiwa kufanyiwa kazi na waziri wetu wa michezo....lakini wanakaa eti wanazungumzia vazi la taifa!!!what a country we have eh!!
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  unaijua sheria ya madini ya TZ?
  Unazijua gov agreemnt wanazoingia na makampuni husika?
  Unajua hata kidogo process ya dhahabu ilivyotoafuti na mafuta? Hii inapelekea risks za kuleta watu wengi karibu kutofautiana

  cha kujiuliza kwanza, watz tunapenda kusoma?
  Kuna faida gani ya kutembelea mgodi ambao hauna uelewa hata kidogo, si utadanganywa ukiwa hapo hapo.
   
 6. J

  JeanPrierre Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Labda tu kwa taarifa, UDSM kuna kitengo kinaitwa Mining and Mineral Processing Eng (B.Sc). Kila mwaka wanafunzi wa mwaka wa tatu (approx 70 students) kwenye hizi programs hutembelea migodi (KMCL, Buzwagi,Tulawaka,GGM etc) ili kuweza kujifunza kwa vitendo zaidi. Ni trip ambayo huchukua si chizi ya wk moja. Mbali na huo muda, kil
   
 7. J

  JeanPrierre Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  cont. mbali na huo muda, baadhi ya wanafunzi hupata nafasi za Practical Training (PT) kwa muda wa wk nane. Migodi ya BARRICK pekee huchukua si chini ya wanafunzi 80 kila mwaka.

  Kwa ufupi napenda tu nikufahamishe kuwa, mpaka sasa kuna Ma Ingineur wa madini wengi tu na wako huko migodi, japo wengi wao hawako kwenye nafasi za maamuzi. Ma Ingineur wengi wenye uzoefu hawabaki tena kwenye hii migodi yetu, wengi wako nje kama Mali, Niger, Australia, Canada ambako wanalipwa kama experts.
   
 8. K-killer

  K-killer Senior Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hivi ndugu yangu una reason kweli au unatapika tuu?umemuelewa ndugu yetu anachouliza hapo juu?unatutajia habari ya wanafunzi 70 wa udsm tena wa mwaka wa3 ndo hupewa fursa yakwenda kutembelea migodi yetu.Unataka kutuambia Tanzania kuna watu 70 tuu au?je unataka kuniambia hamna wengine wenye intrest yakujua kinachoendelea huko?Fikiri fizuri kaabla yakujibu swali.Serikali yetu imekua ikificha sana swala lolote linalohusiana na madini,na hii ni kwasababu hayo madini wanayochimba sio kwa intrest ya watanzania,ndo maana hadi leo huwezi kwenda kuhuzuria kwenye migodi kirahisi vizingiti ni vingi.Mpaka I can assure u it hardly 2% of Tanzanians wanaojua kuhusu madini yao.Swali ni kwamba kwanini hawaweki wazi kama wenzetu nchi zingine wafanyavyo?kwanini wanafunzi kuanzia primary mpaka elimu ya juu wasiwe wanapewa school trips sehemu hizo za machimbo ili wajue kinachoendelea na utajiri wa nchi yao.Madini tuu tuliyokuwa nayo yanatosheleza kuiendeleza hii nchi na kuchangia asilimia kubwa sana kwenye maendeleo bila kutumia secta zingine zozote...Naomba tuendelee kuchambua hii hoja.
   
 9. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  Kuna majibu mengine hata mtu unajiuliza huyu kweli mtanzania??...sasa wewe unamtetea nani??Watanzania ignorance itawamaliza.....
   
 10. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,526
  Likes Received: 1,313
  Trophy Points: 280
  You are talking about a few tz students here??.....i'm talking about the Tanzanian population here...by the way...rejea nilichoandika na usome kwa uelewa.....imeshindikana kwa watanzania wengi kujua shughuli zinazoendelea kwenye migodi ya madini(na hata gas)physically lakini hivi hata kuwaonyesha watanzania hizi shughuli kwenye TV ya taifa imeshindikana???.....wewe JeanPierre....are you a Tanzanian??...kwasababu hata Engineer umeiandika very differently...Ingineur.....i can query your nationality here......
   
Loading...