Hivi kuna washabiki wanaongoza kwa unafiki kama washabiki wa Simba?

changaule

JF-Expert Member
Jan 10, 2020
5,580
9,166
Mashabiki wa Simba wanaongoza kwa kubadilika badilika maneno..
Manula akifanya makosa basi wote wanaimba wimbo wa Munula hafai. Mugali akifanya makosa wote wanaimba wimbo mmoja kuwa Mugalu awekwe benchi apangwe Kagere. Kagere akipangwa na hakufanya vyema basi wimbo unabadilika kuwa Kagere hatufai tunamtaka Mugalu

Mechi ya iliyofanyika Botswana, hakuna mshabiki yeyote aliyepiga kelele kwa Simba kucheza chini ya kiwango pamoja na kupata matokeo ya goli mbili, hii yote ni kwavile walilevya na matokeo.

Leo hii pia nimeona kila mshabiki wa Simba alitabasamu huku moyo wake akijwa na faraja kuwa pira birisni limerejea. Hii ndio Simba sasa tunayoijua Scars akadiriki hadi kusema kuwa hata tusipopata goli lakini biriani tumelipiga. Wakati huo kila mchezaji wa Simba alipewa credit hakuna ambaye aliyekuwa na jicho la ziada kubaini mapungufu ya kitimu na kujua uzuri wa wapinzani wao ukoje pamoja na kutokupata matokeo, zaidi ya wao kupata faraja ya kuona
Biriani imerejea.

Baada ya kufungwa nimeshangaa zinaanza lawama kwanzia kwa kocha, kwa wachezaji wote wapya hawafai, Manula naye analalamikiwa, Wawa nae analalamikiwa, timu kwa ujumla inalalamikiwa kuwa hamna kitu safari wanacheza ovyo. Mmesahau kipindi cha kwanza tu mmetoka kujisifia kuwa biriani imerejea,. Mliosajili ni watu kweli kweli tena watu na nusu. Simba wanaupiga mwingi mpaka unamwagika.
 
Mimi mi shabiki wa Simba.Nimegundua watu wengi mpira hawaujui licha ya kuonekana washabiki kuliko hata mimi.

Nilikuwa nikiwaambia timu ile si mbovu kama wengi walivyoidharau.Hata wachezaji wa Simba wakaingia kwenye mtego huo.Walicheza ki star sana.
 
Mimi mi shabiki wa Simba.Nimegundua watu wengi mpira hawaujui licha ya kuonekana washabiki kuliko hata mimi.

Nilikuwa nikiwaambia timu ile si mbovu kama wengi walivyoidharau.Hata wachezaji wa Simba wakaingia kwenye mtego huo.Walicheza ki star sana.
Ile timu nilivyoiona tangu kule Botswana ilicheza mpira na wanaujua haswa mpira,ila kule Botswana Simba walicheza kwa tahadhari ndo maana Jwaneng hakuweza kulisogelea kabisa lango la Simba na kuonekana kama si timu nzuri kwasababu hiyo.

Kwa mkapa Simba kwa sababu yupo nyumbani akafunguka ili acheze mpira biriani ambao kiukweli hawana mpira huo siku hizi,hapo ndipo Jwaneng wakaweza kuonesha walichoshindwa kuonyesha kule Botswana

Mashabiki wa Simba na Yanga hawaangalii mpira kwa macho matatu,bali wanaangalia kishabiki lkn kilichotokea hakikunishangaza japo ilikuwa ngumu kufikiria kwamba Jwaneng wangewatoa Simba mazima lkn nilijua tu lazma Jwaneng wataonekana tofauti sana leo.
 
Simba wakacheze tu shirikisho ndio saizi yao na hata huko pia hawatafika mbali kwa sababu timu uwezo mdogo na imesheheni vijeba wengi.

Ni muda sasa ku-recruit vijana na kuachana na hawa wachezaji wazee akina Wawa, Onyango, Kagere, Bocco, Morrison nk kwani hawawezi kubadilika na pumzi sasa inaanza kukata.
 
Back
Top Bottom