Hivi Kuna Washabiki wa American Football 🏈/NFL Humu JamiiForums?

King Shaat

JF-Expert Member
Aug 30, 2013
863
835
Habarini Wakuu,

Natumaini mko poa kabisa katika jitihada za kujiendeleza kila siku.

Kama kichwa cha habari kinavyouliza hapo juu, ningependa kufahamu (na kufahamiana) kama kuna mashabiki humu JamiiForums wa mchezo wa American Football 🏈 au "ligi" ya NFL ya Marekani.

Bucs-Chiefs Super Bowl LV Scrimmage
Bucs SB LV Champions.jpg


Nafahamu ni moja kati ya michezo isiyokuwa na washabiki/wafuasi wengi "kiviile" hapa Tanzania, ila naamini watakuwepo tu wachache wanaoufuatilia, iwe kindakindaki au mara mojamoja pale mchezo/michezo pendwa inapokuwa "msimu wa mapumziko"/off-season.

Hapa JF nilibahatika kukutana na mshabiki mmojawapo wa American Football/NFL, ndugu Nyani Ngabu. Huyu legend tulikuwa wote mashabiki wa New England Patriots; mimi tangu 2004 kupitia enzi yote ya Brady-Belichick hadi pale Tom Brady alipohamia Tampa Bay Buccaneers mwaka jana (2020) na kushinda nao kombe la ligi hiyo kwenye Super Bowl LV (55), Feb 2021.

Naamini kutakuwepo na wengine wachache (wanaweza wakawa wengi, tofauti na ninavyodhania!) wanaoshabikia mchezo huo. Tufahamiane. Unashabikia timu gani?, enzi gani ya ligi unaikumbuka kama iliyofana sana? wachezaji gani unawaelewa sana NFL?, timu zipi unapenda zikikutana/Quarterbacks gani unapenda wakikutana kwenye mechi (QB match-ups)? [binafsi mechi yeyote yenye "elite" quarterbacks (kama last Super Bowl) Tom Brady, Patrick Mahomes, Aron Rodgers, Lamar Jackson, Big Ben au mechi zenye uhasama wa ki'kanda/divisheni (divisional rivalry)].

Karibuni!
 
Football au handball? Huhuhu
Football , mkuu!

Sema ndo hivyo wenyewe wanavyouita huo mchezo. Kwao huu mpira wa miguu sisi tunaouita "football" wao wanauita "soccer".

Ingawa unahusisha kuubeba mpira ili ku'score, mchezo huo ni tofauti kabisa na Handball .
 
Back
Top Bottom