Hivi kuna wanachama wa JF wanaoishi vijijini?

Nimekuwa najiuliza hili swali.maana me naamini sisi sote tunaishi mijini hasa majiji dar na labda katika miji mikuu ya mikoa.kwa kuangalia threads za wengi naona wengi wajanja wote Wana misemo ya kimjini mjini.sifikirii Kama Kuna yoyote ambaye yupo ndani ndani bush kabisa.
Jina nalotumia JF linasadifu nilipo acha mtandao wa shida hapa kuna wakati napata tabu sana
 
Nipo TUBUGWE - KONGWA, na Last Friday tulikuwa na Mh. Mbunge wetu Ktk uwanja wa Mpira TUBUGWE, alikuja kutoa zawadi kwa washindi! Katika mashindano yake aliyoyaanzisha yeye mwenyewe!

Tangu nusu ya pili ya mwaka 2018 anazunguuka sana vijiji vyetu. Huku wanasema atakuja sana kipindi hiki mpk 2020!

Pia amesema atatuwekea lami barabara ya MLALI - TUBUGWE! Kiukweli sisi watu wa Kongwa tuna bahati Sana!

From nowhere, Jumatatu ilopita wakaja ma VX ya waziri wa nishati, akatukusanya, akahutubia! Akasema "naamuru TANESCO msiondoke site (Tambi - Kijiji jirani) mpk umeme uwake! Cha ajabu hakukuwa na nguzo wa shimo!

Nikawa nasubiria kuona " wireless electric power!" Hamna Kitu na washaondoka!
 
Back
Top Bottom