Hivi kuna wahariri ambao ni wapigapicha?

hoyce

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,117
297
Kama ilivyo kwa polisi, Trafiki, FFU na askari wa kawaida wote husoma kozi ile ile; pia kwa uandishi wa habari, waandishi wa magazeti, watangazaji wa redio/tv na wapiga picha husoma kozi moja, labda pale mtu anapoamua kujiendeleza mwenyewe. Tumezoea kuona wahariri wakiandika habari, makala na maoni mbalimbali, vivyo hivyo wahariri waliopo kwenye redio/tv wameendelea kuwa watangazaji.

Swali langu ni je, kwa nini hatuoni wahariri ambao wameendelea kuwa wapiga picha za matukio ya kihabari?
 
Back
Top Bottom