Hivi kuna-uwezekano watu wengi tumeshaumwa hii corona!

gango2

JF-Expert Member
Aug 31, 2011
1,941
2,251
Igwee!!!

Katika pita pita zangu nimekuwa nikisikia kila mtu akinipa maelezo kuwa aisee nimeumwa mafua, mara last week nilikuwa sisikii harufu hata ya kinyesi, mwengine atasema mara koromeo limemuuma mpaka basi.

Now considering hii wanayosema haka kavirus kanajibadilisha badilisha kila siku- hivi kuna uwezekanao kale kalikowatesa wanzetu kule china na italia kwetu kamejibadilisha kamekuwa sio kakali zaidi na tumeshaumwa umwa sana haka ka-corona mpka kanaisha kenyewe!

hetu kama kuna wataalamu wa afya humu watujuze based na experience wanazokutananazo huko!
 
Mkuu wengine tumeanza kuumwa hivyo toka mwaka jana,mwaka jana watu tumeumwa sana mafua makali kusiko kawaida na baadhi ya dalili za corona kipindi hicho mastory ya corona bado kabisa.
 
Hapa mwenyewe shingoni pako Kama Kuna kibanzi kimekwama hivi baada ya kubanwa na pumzi kiasi na maumivu ya kifua mwisho juzi Jana na Leo ndo hivyo shingoni hapasomeki
 
Mimi naelekea kupona hizo dalili namshukuru Mungu...pua yangu inawasha bila mafua,kichwa kinauma,homa inapanda..hio ya koo kuwasha ndo sina.
 
... acheni kujipa moyo! Corona likutembelee halafu usilijue? Corona likiingia mwilini halina haja ya introduction; huwa linajitambulisha lenyewe. So, hizo labda, labda, labda ondoa likiingia utalitambua tu tena kwa uwazi kabisa.
 
... acheni kujipa moyo! Corona likutembelee halafu usilijue? Corona likiingia mwilini halina haja ya introduction; huwa linajitambulisha lenyewe. So, hizo labda, labda, labda ondoa likiingia utalitambua tu tena kwa uwazi kabisa.
Wapo ambao wanaonyesha dalili chache na wengine hawaonyeshi kabisa.
 
Waziri wa afya asema dalili za corona Tanzania ni tofauti na nchi nyingine duniani, aagiza uchunguzi
BongoleoMay 6, 2020Read original

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya utafiti kuhusu ugonjwa wa Corona (Covid-19) kwa kuwa kuna tofauti kubwa ya dalili zilizojitokeza kwa wagonjwa hapa nchini ukilinganisha na wagonjwa waliopo nje ya nchi.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipokutana na watafiti wa taasisi hiyo wakati wakijadili maambukizi ya ugonjwa wa Corona na aina ya matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa hasa baada ya kubainika kuwa dalili za ugonjwa huo zinatofautiana na dalili za wagonjwa wa mataifa mengine.

“Kuna mambo mengi ambayo tunapaswa kuyafanyia utafiti wa kisanyansi, moja ni uelewa wa jamii, tunataka kujua wagonjwa wanaougua Corona ni wagonjwa wa namna gani, wana magonjwa ya aina gani, dalili zinazowapata wagonjwa ni za aina gani. Hapa tunataka tupate uwelewa,” amesema Dkt. Ndugulile.

Leo Mei 7, 2020 , amesema kupitia utafiti huo wanataka kujua aina za matibabu ambayo wagonjwa wanatakiwa kupatiwa ili kuhakikisha ugonjwa wa Covid-19 unadhibitiwa hapa nchini.

“Kutokana na muitikio mkubwa wa tiba asili na tiba mbadala, kupitia kikao hiki nawaelekeza wataalamu wetu wajipange kufanya utafiti na kutoa majibu ya tiba ya maambukizi ya virusi vya Corona,” amesema Dkt. Ndugulile.

Amesema wamekubaliana na watafiti hao kufanyia kazi maagizo hayo ndani ya muda mfupi na kutoa majibu sahihi ambayo yatasaidia katika mapambano ya ugonjwa wa Corona.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Prof. Yunus Mgaya amesema mapambano dhidi ya ugonjwa Covid-19 ni vita ambayo inapaswa kufanyiwa utafiti ambao utasaidia kupatikana kwa njia sahihi za kukabiliana na maambukizi ya ugponjwa huo.

“Tunafahamu kwamba jamii za kiafrika zina utaalamu katika miti shamba. Katika hili kuna tafiti mbalimbali zinaendelea ili kuchunguza uwezo wa miti shamba kwa lengo la kupunguza makali ya Covid-19.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana kabisa. Mimi na familia yangu tumepata homa na kuharisha. Tulikwenda hospital tukapima kila kitu expect korona lakini hatujakutwa na ugonjwa wowote. Mke wangu, mama yangu na shemeji yangu mmoja ambao tulikutana nao hivi karibuni (ninamaanisha mama na shemeji yangu) hawasikii harufu yoyote hata iwe ya mzoga. Mtoto mmoja ana Kama miaka 5 yeye anaarisha na kinawakati anapatwa na homa kidogo. Nahisi hizi ni dalili za korona kabisa especially kushindwa kunusa harufu.
 
Niliumuwa mafua,kifua,uchovu na homa ya kutisha December mwaka jana.Ilikuwa hali ya kutisha na sikujua ni nini mpaka napona!
Mkuu wengine tumeanza kuumwa hivyo toka mwaka jana,mwaka jana watu tumeumwa sana mafua makali kusiko kawaida na baadhi ya dalili za corona kipindi hicho mastory ya corona bado kabisa.
 
... acheni kujipa moyo! Corona likutembelee halafu usilijue? Corona likiingia mwilini halina haja ya introduction; huwa linajitambulisha lenyewe. So, hizo labda, labda, labda ondoa likiingia utalitambua tu tena kwa uwazi kabisa.
Unaitambuaje? maana watu wanaeleza dalili ambazo ndizo dalili tulizoelezwa za corona.
 
Niliumuwa mafua,kifua,uchovu na homa ya kutisha December mwaka jana.Ilikuwa hali ya kutisha na sikujua ni nini mpaka napona!
Mkuu hiyo imewapata wengi sana na hadi sasa hakuna anayejua ilikuwa ni nini hasa,upo uzi humu kabisa watu wanaelezea jinsi walivyoumwa last year.
 
Back
Top Bottom