Hivi kuna uwezekano wa watu au mtu binafsi kufungua kesi mahakama kuu kuishtaki serikali?

Kiti

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
359
234
Hivi kuna uwezekano wa watu au mtu binafsi kufungua kesi mahakama kuu kuishtaki serikali. Mfano, Waziri wa afya alitamka kuwa serikali haina mpango wa kuagiza chanjo ya korona.

Serikali inaweza kushtakiwa kwa kuwanyima raia wake haki ya kuzuia maambukizo?
 
Ndiyo inawezekana kuishtaki serikali lakini kwa mazingira uliyoyasema hapo juu haiwezekani.

Ngoja niseme kwanini
Mtu anaweza kufungua shauri dhidi ya serikali kwa haki zilizopo Ibara ya 12 mpaka 29 tu. Sasa ni kwa bahati mbaya haki ya kupata huduma bora kiafya haipo katika katiba yetu ya 1977.
Pia marekebisho ya sheria ya haki na wajibu sura ya 4 na marejeo yake inamtaka mtu atakaye fungua kesi dhidi ya serikali kusema kwamba haki yake imevunjwa lazima aonyeshe, kuvunjwa kwa haki hiyo kumemuumiza vipi binafsi.

NB: serikali kutoa huduma za kijamii kama afya kunategemeana na uwezo wake huwezi kuilazimisha serikali kununua chanjo ya korona wakati haina hiyo budget na haipo kwenye vipaumbele vyake.
 
Kabla hujaishtaki serikali lazima utoe notes tya siku 90 nini kusudio lako.la kuoshtaki serikali naambo kibao anyway ni wasting of time na jokes
 
Back
Top Bottom