Hivi kuna umuhimu gani kumtafunia mtoto chakula

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
69,788
137,044
Wazazi na walezi wote, huwa kuna sababu gani ya kumtafunia mtoto chakula? Mi huwa naona ni uchafu tu kwakweli hata kama mtoto ni wako. Mambo mbona yamerahisishwa kama unataka kumwahisha kula nyama na vyakula ambavyo hawezi kutafuna kwanini usitumie blender kusaga viwe laini umpe?

Unakuta mama anaweka nyama mdomoni anaitafunaaa afu anatema anampa mtoto ptyuuuu sio mapenzi ni uchafu hayo ya hivo mfanyie baba ake sio mtoto please, midomo yenyewe hii ina bacteria tu, midomo imenyonya sijui nini huko ikala na zile sijui nini ikalamba na nanii sasa kwanini umtafunie mtoto.

Kueni wastaarabu
Weekend njema
 
Last edited by a moderator:
Kweli ata mi naonaga naskia kichefchef sio ustaarabu kabsa
 
mtu kalamba chumvini huko kisha anakuja kulamba uji wa mtoto kwa kupooza afu anamnywesha! tena ni celebrity!
 
Hiv kuna watu kabisa wanafanya hivo" duh
Jirani yangu nishamuona anaweka kipande cha papai mdomoni kwake hatafuni then anatema anampa mtoto, nikamuuliza mbona papai ni laini linatafunika kwanini anafanya hivo akasema analipoza ni la baridi lilikua kwenye friji.....
Kina mama wengine ni kichefuchefu
 
Mhh mm nakumbuka kijijini mzazi km anataka kumpa mtoto labda muhind wa kuchoma anamtafunia anampa coz hata blender hakuma
 
Umaskini na elimu pia vinachangia sio kila mzazi anauwezo wa kununua blender, na hiyo ipo sana vijijini wamama wengi hulazimika kuwatafunia watoto wao kutokana na aina ya Chakula.
Wakat Mwingine akina mama tunapitia mengi nilishaona mama anamnyonya mwanae pua na sehem zingine ili kunusuru maisha ya mtoto baada ya kuzama kwenye dimbwi la maji na kupoteza faham, wengi wetu tulidhan mtoto amefariki lakini baada ya yule mama kunyonya sehem mbalimbali za mtoto baadae mtoto alizinduka mpaka Leo yuko hai.
 
Mhh mm nakumbuka kijijini mzazi km anataka kumpa mtoto labda muhind wa kuchoma anamtafunia anampa coz hata blender hakuma
Kwanini ampe mtoto mahindi ya kuchoma kama hana meno, mara mia na hao wa vijijini hawajui hata madhara ya kumpa mtoto chakula kigumu hivo na madhara ya kumtafunia
Sio hawa kina mama wa mjini wenye degree zao kufanya mambo ya hivo
 
Umaskini na elimu pia vinachangia sio kila mzazi anauwezo wa kununua blender, na hiyo ipo sana vijijini wamama wengi hulazimika kuwatafunia watoto wao kutokana na aina ya Chakula.
Wakat Mwingine akina mama tunapitia mengi nilishaona mama anamnyonya mwanae pua na sehem zingine ili kunusuru maisha ya mtoto baada ya kuzama kwenye dimbwi la maji na kupoteza faham, wengi wetu tulidhan mtoto amefariki lakini baada ya yule mama kunyonya sehem mbalimbali za mtoto baadae mtoto alizinduka mpaka Leo yuko hai.
Blender kwa mjini, vijijini kuna vilee vimti vya kupekechea, pia chakula cha mtoto kukikoroga koroga kinafaa mfano ndizi, viazi mviringo, viazi vitamu hata wali vikipikwa kwa muda vikakorogwa vinafaa kabisa kuliwa na mtoto

Hiyo ya kumnyonya mtoto ni kawaida sio kijijini tu, mtoto mdogo akiwa na mafua unamtoaje? Au akicheua maziwa yakapita puani unafanyaje? Ni kumnyonya tu pua tena unafanya taratibu lol
 
Kuna mama nilikuta anamnywesha sipy soda mtoto wa miezi kama 11 hivi yani nilisisimka vibaya sana. Na mtoto anaonekana kazoea maana aliikata fasta
 
Usije kuta hata wote humu tuliwahi tafuniwa chakula na kulishwa,hayo ni mapenzi ya mama kwa mtoto yaliopitiliza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom