Hivi kuna ulazima wa kuoa/kuolewa??

HAZOLE

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
1,551
708
jamani hebu tulitazame hili kwa kina maana binadamu tumetofautiana kwa mambo mengi.
 
Inategemea na mtu, familia! kabila, dini, mahali anapoishi, mila, desturi, mtazamo na uzoefu binafsi wa mtu.
 
Siyo lazima kama mtu anaweza kushinda vishawishi na kuepuka zinaa kwa mujibu wa Biblia. Mtume Paulo alisema ni vizuri kama watu wangeishi kama yeye maana alikuwa hajaoa lakini ili kuepuka zinaa ni heri kila mtu awe na mke wake mwenyewe.
 
Ni uamuzi wa mtu mwenyewe! Lakini tamaduni nyingi hasa za Afrika hazilipokei suala la kutooa au kutoolewa!
 
Ni kweli hakuna ulazima lakini kisayansi, binadamu tuna mambo mawili mkuu ambayo kwa hayo tukaletwa duniani:

1. Tulizaliwa ili tuishi duniani, pili
2. Kuzaa

Iwapo moja kati ya hayo halitimii, basi ukamilifu wa binadamu haupo
 
Hata hivyo ili kuzaa sio lazima uoe au kuolewa. Ni woga wa binadamu dhidi ya maneno ya wanajmii ndio unaopelekea watu kulazmisha kuoa au kuolewa. Nawafagilia sana wadada wanaoendesha maisha yao bila kuwa na mtindio wa kutaka kuolewa
 
Kama huko single afu unatembelea MMU sishangai unajiuliza kama ni lazima kuoa/kuolewa. Nadhani ma thread yanawatisha vijana. I thank God sikuwahi tembelea MMU kabla sijaolewa maana labda na mimi ningekuwa kati ya wale wanaoogopa ndoa.
 
sio lazima,hata yesu alikufa bila kuwa na mke wala mtoto,ni maamuzi yako tu
 
Inawezekana haujui lengo la kuoa au kuolewa!
anajua sana ila haya mambo wanayotufanyia kina dada na kwa kina dada kwa wale wanaumme wasio waaminifu kwa kweli inauma sana,ndyo maana kasema hivyo
 
Sio lazima, laki kunawakati kuna umuhimu, unakuwa na kampan ya kushare vitu mbalimbali ktk maisha, haswaa pale mkeo au mumeo anapokuwa ni best friend.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom