Hivi kuna ukweli kwamba wanawake walioajiriwa hujitongozesha kwa mabosi?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kuna dhana kwamba wanawake walioajiriwa wanakabiliwa na mazingira ambayo yanawalazimisha kuingia kwenye vitendo vya kutoka nje ya ndoa zao, ukilinganisha na wanawake ambao hawajaajiriwa hususani mama wa nyumbani jambo ambalo katika maisha ya kawaida bila utafiti linaonekana kama vile ni kinyume yaani akina mama walio majumbani ndio ambao hutoka nje zaidi.

Niliwahi kuwahoji wanawake kadhaa jijini Dar, mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Nilifanya mahojiano hayo ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

Lakini bila shaka suala la mapenzi kwa wanawake walioajiriwa lina nguvu na kwa hiyo limekuwa likifanyiwa tafiti katika sehemu mbalimbali duniani. Tofauti na tafiti ambazo zimefanywa hivi karibuni zinaonyesha kwamba mwanamke mmoja kati ya kumi walioajiriwa huwa anaonyesha tabia za kimapenzi au kujitongozesha kwa bosi wake.

Tafiti hizi zinaonyesha kuwa yule mmoja kati ya kumi ambaye hujitongozesha kwa bosi huishia kutembea naye au hata kuolewa naye kama hana mume na pengine kuvunja ndoa yake. Inaelezwa pia kuwa mmoja kati ya wanawake kumi wanaojitongozesha kwa mabosi huwa anapandishwa cheo. Hii ina maana kwamba wanawake wanaopandishwa vyeo kwenye maeneo ya kazi huenda mmoja kati ya kila kumi hupandishwa kwa sababu za kimapenzi hata hivyo siyo lazima iwe hivyo.

Katika mahojiano na jarida moja nchini Marekani mwanamke mmoja kati ya watano alikiri kwamba yuko tayari kujitongozesha kwa bosi ili kujaribu kulinda nafasi yake kazini au kupandishwa cheo. Jarida hilo halikufanya mahojiani ili kujua idadi wanaume wanaotumia nafasi zao kazini kuwadhalilisha wanawake kijinsia.

Wanawake wenye watoto ambao walihojiwa kwenye tafiti hizo walisema kwamba ajira zinawasumbua na wamefikiria kuwa ni ngumu kujigawa kazini na nyumbani kishughuli.

Tafiti hizo hata hivyo hazikulenga katika kuonyesha kwamba wanawake ni dhaifu bali huenda zimelenga katika kuonyesha kwamba idadi ya wanawake wanaojitongozesha kwa mabosi ni ndogo kuliko inavyotazamwa au kuaminika na pia kuonyesha kwamba bado wanawake walioajiriwa wako kwenye nafasi kubwa zaidi kushiriki mapenzi kuliko wale walioko majumbani. Ni juu ya wanawake ambao wanadhani ni halali kuuza thamani zao kwa ajili ya kazi kubadili mwenendo huo..
 
Kama ulivyoanza kusema... ni dhana tu..... mahusiano ya kimapenzi hayajali uko wapi... hayajalishi kama umeajiriwa au uko nyumbani.Hayajali kuwa wewe ni mfanyakazi au wewe ni mkulima uliye kijijini.Ni hulka iliyo ndani ya binadamu.Kama ambavyo kuna mafisadi wenye kuweza kufanya chochote ili wafaidike na nafasi zao, vilevile huwezi kukosa mafisadi wa kike wenye kujua sehemu tete ya kugusa ili wafanikiwe kile wanachotaka.Kwa kifupi, pamoja na kwamba hukuonyesha chanzo cha ulichonukuu wala theme ya utafiti huo uliounukuu..bado inabaki kuwa wapo wanawake walio mahiri 9/10 kama ulivyosema wenye kupata stahili zao iwe ni cheo au marupurupu kwa vile wanastahili kama wengine.

Mbona pia kuna dhana kama hiyo kuhusu wanawake wa majumbani ambao wakiachiwa pesa ya mahitaji huishia kupewa kila kitu bure kuanzia buchani, sokoni hadi kwa fundi cherehani?.....haya ni mambo binafsi ya mtu binafsi na hulka zake za kutaka dezo bila kutoka jasho halali maana hata hicho wanachokifanya ili kufikia malengo siyo kazi ndogo - hutoka jasho pia.
 
hayo ni mawazo tu.
inategemea tabia ya mtu na aina ya bosi uliyenaye.
kuna hata kina mama wa nyumbani wanajitongozesha kwa wauza mboga na wanasaliti nyumba zao.si kweli ni mawazo tu ya baadhi ya watu, kama ilitokea kwa 1 basi na wengine wanajumuishwa.
kwanza ofisi zina wanawake wengi huyo bosi atatembea na wote?
 
si wanawake tu pia kuna wanaume wengine wanatabia ya kujikomba komba kwa mabosi wao! kwa vile wanawake wana vitu vya ziada ndio maana wanatumia hii kama silaha!!
 
Kaka yangu ni tabia na hulka ya mtu ndo anakuwa hivyo huwezi ukamcheat mumeo kwanini ufanye uupuuzi huo na bosi wako kisa kupandishwa cheo au kazi hivyo vyote vina umuhimu gani kuliko kujali utu wako na heshima uliyonayo wewe mwanamke mm ndomana nilisema liwepo juwkwaa la wanawake ili niweze kuwafunda watu humu mjengoni
 
hiyo ni tabia ya mtu mana hata kama ni mfanyabiashara anaweza kujitongozesha kwa wateja wake......ama ni mama mwenye nyumba anaweza kujitongozesha kwa wapangaji......nadhani ni hulka ya mtu.
 
asilimia kubwa ya wanawake wanafanya hivyo maofisini. usije kujilinganisha nao kabisa wewe mwanaume,.......wao wana altenative yao...watakuacha kimaisha fasta hutaamini kumbe wametumia tu kifaa chao.. ukimwi sasa...
 
Kama wanakuja hapa na kujinadi kuwa mwanaume bila kuwa na pato la mil 2 kwa mwezi hawamtaki unadhani hili linashindikana?
'
Bila shaka linawezekana kabisa!
 
asilimia kubwa ya wanawake wanafanya hivyo maofisini. usije kujilinganisha nao kabisa wewe mwanaume,.......wao wana altenative yao...watakuacha kimaisha fasta hutaamini kumbe wametumia tu kifaa chao.. ukimwi sasa...

mwanamke sio mwenzio ndugu anaweza kumiliki mali nyingi tena za samani kwa maramoja ambazo mwanaume angeweza kuzisotea kwa miaka nenda rudi ili avipate.
 
Tena usalita wa wanaume unaumiza mpaka utummbo unaweza kukatika katika huko tumboni khaa
 
Dunia ya sasa imakaa kingono ngono tuu :confused:, wanaume KUSHNEI na wanawake NeiNei
Eti kujitongozesha kwa bosi???? Kisa salary iongezwe hovyooo kabisa!!!!!
 
Back
Top Bottom