Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Kila siku mnakandia wabeba box afu mnakuja inbox kuuliza jinsi ya kuja kiwanja 😀

Hao wachache maisha yamewachapa mbona huongelei waliotoboa huko ughaibuni. Kila sehemu wapo wanaofanikiwa na wanaofeli.

Unataka kusema wote waliobaki bongo wametoboa? Mbona kila siku mnalia njaa. Tukidondoka wanyamwezi toka kiwanja ni kupigwa mizinga tu.

Wapo kibao waliotoboa nje sema wewe inaonekana circle yako ni ya waliosanda so unakutana na waliofulia wenzako, wengine tunadondoka bongo kila siku spending like there's no tomorrow na kurudi kiwanja. Tupo in the corporate world now tushapita kubeba box. Tunawekeza pia for our families ikibidi hata kuiba rasilimali maana bongo watu bado wamelala usingizi wa pono wanasubiri serikali iwafanyie kila kitu.

Nimerudi kiwanja last week toka kula vumbi bongo. Kama unataka kuja kiwanja usisite kuuliza 😜
Waelezeee maelezo yanajitosheeza
 
Waseme na wale wanaotoka mikoani kuja Dar,,, huwa wanajikuta kilixhowaleta dar hawakipati na kurudi makwao wanaona aibu,,siku wakirudi wanakuta waliowaacha wana maisha next level zaidi yao!! Hii inawakumba hata watumishi wa umma waliopangwa kazi nje ya mikoa yao mara nyingi hujikuta wana madeni tu huko mijini wanaogopa hata kurudi nyumbani
 
Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
Hakuna usiano wowote kufeli ni kufeli tu hata ungeenda mwezini kama kufeli kupogo tu inategea huko kufeli kwa mtu. Kuna mwengine kufeli ni kuwa idle hahahaha
 
Hao ni wachache vipi walio wengi waliofanikiwa?

Hata hapa nchini kuna watu pia wamekwama na wamechoka ila pia kuna watu pia wamefanikiwa.

Hivyo kuna wanaofanikiwa na kuna wasiofanikiwa katika kila maeneo.
 
Kongole kwa Joannah kuanzisha uzi huu. Ni ukweli usiofichika kwamba baadhi ya diaspora wana hali ngumu huko walipo, na hasa wale ambao wanaishi bila kuwa na documents stahili. Lakini hata wengine ambao ni wanafunzi na wanaruhusiwa kufanya kazi masaa 20 kwa wiki wanaweza kujiwekea savings lakini hawafanyi hivyo. Sana sana wanaishia kununua nguo na sneakers ambazo kwa kweli sio bei ndogo. N sawakirudi bongo na hivyo vinguo vyao na slang yao basi wanaona wame-win only kuja kushangaa waliowaachaa bongo wao wako mbele kimaisha kuliko wao. ila kuna baadhi ya diaspora pia wamefanikiwa sana na wanasaidia sana familia zao bongo, na wao pia wame-invest vizuri kwa ajili wakirudi waweze kujikimu na kuishi maisha mazuri. Badala ya baadhi yetu humu kumshutumu Joannah, tutumie hoja hii hasa kwa wale ambao wako ughaibuni kuona hii kama "Wake Up Call" kwamba tusijisahau sana kwa kuwa kuna siku tutarudi kwetu bongo, na hivyo ni muhimu kujipanga!!!. Au sivyo ndiyo yale ya kurudi nyumbani na begi la nguo, hereni na macheni feki huku mwili una matatoo kibao na huna hata hela zaidi ya dola 2000 mfukoni. Unakuja kutamba na Kingereza ambacho bado ni kibovu anyways, na kujiona uko vizuri, kumbe unachekwa mtaani.

Kama wewe uko nje, kumbuka siku moja utarudi home, hivyo jipange. Hujachelewa. Hata kama umri umeenda, piga miaka yako kama 3 hivi kazi bila kuchoka au kufanya anasa ambazo hazina maana huko. Ukijitahidi, si haba hata ukirudi na dola 150,000 itasaidia kupata kibanda chako cha retirement na chenji kuanzisha mradi wa kukuweza kujikimu bila kuwa omba omba. Itazuia aibu ya kurudi na begi tu na pea tatu za viatu ambaa hata hizo viatu havina mwenzake.
Umenena Vyema Sana mkuu....nimependa hapo kwenye"Wake Up Call"nadhani watakuelewa
 
Wachangiaji wwengi hawana experience wala exposure/kusafiri wala kuishi nje /hukobulaya na marekani...

So wanaongea stori za kusadikika ,za kuambiwa na zakuongeza chumvi..

Ni wachache tu humu wenye kuujuwa ukweli!

Wabongo wengi wana tabia ya kufurahia kufeli kwa mtu, yani ukifeli kwao ni sherehe... wanapata faraja kuona mambo ni magumu kwa wote na sio wao tu, hawafurahisi na habari njema za mtu.

Unafki ndio balaa , pamoja na ule ujinga wa masikini jeuri- kujifanya huna shida na kitu fulani wakati " kimoyo moyo" unakaitamani ile mbaya
Hao mdio aina ya wabongo walio wengi ..

Wengi wanaponda sana idea za kusafiri na kuishi nje , lakini wanapopata taarifa za watu walio nje kufanikiwa huwa wanapata wivu na kujenga chuki sana !

Asilimia kubwa ya wanaoenda nje kwa njia halaili na kwania ya kujikwamua kimaisha hufanikiwa tena kwa asilimia kubwa kabisa ...
Kwa maana huwezi kulinganisha maisha ya bongo na U.S au canada ... na ukiona mtu anakwambia "komaa tu hapa hapa fursa zipo nyingi ujue ana akili mgando na hana exposure "

Na kama siku ikatokea akapata chance ya kusafiri, basi atafunguwa akali yake na kujuwa kumbe kuna maisha nje ya mipaka ya tz .!
I second you
 
Hiki ndicho Wabongo wasichoelewa. Na hawataelewa hadi siku watakapotoka Tanzania. Na kwa sababu hawatotoka, watakufa tu bila kuelewa. Watu wana hela kwenye nchi zilizoendelea lakini wanapanga mwanzo hadi mwisho.Cash ni muhimu sana ktk nchi zilizoendelea kuliko assets.
Ulaya watu hawajengi nyumba wewe. Kwako kujenga nyumba ndiyo kipimo cha maendeleo.
 
77 Reactions
Reply
Back
Top Bottom