Elimu haina uhusiano na utajiri, the summit of education is wisdom, sasa wisdom na kujilimbikizia Mali wapi na wapi , always huwa nina tafsiri kujilimbikizia Mali (utajiri) ni ukilaza , ndio maana watu wenye wisdom kama vile mwalimu Nyerere hawakuwa matajiri.
hapana
maprofessa ma madakta wa vyuo vikuu wote tz hawana hela kama kina chenge, lowassa, kikwete, mramba, yona, rostam, mkapa, mengi, manji, mgonja, rutabanzibwa nk.
Matajiri wakubwa duniani kama bill gates na larry wa facebook wali drop out of college.
Tajiri mkubwa kuliko wote tz mzee bakhresa hana elimu.
Hivyo jibu ni hapana.
Ungeuliza kama kuna uwiano kati ya kusoma sana na kuishi maisha mazuri statistically jibu lingekuwa ndio.
PhD, Professor, Masters etc si kipimo cha kusoma sana. It's a system and there are ways to work it.
Nilishangaa mtoto mmoja - very smart - anasoma Ph.D ya sayansi ya ubongo at a prestigious college in the field, alipewa kazi ya kuandika habari za chumi za emerging markets na the so called BRICs, na jinsi public policy inavyoweza kunyanyua maisha ya watu masikini. Akawa hana pa kuanzia. Akasema anayemjua ni Muhammad Yunus tu wa Bangladesh ambaye hatafit kwa sababu hakutumia public policy kama elected official. Nikamwambia nenda kasome kazi za Fernando Henrique Cardosso. This was a no brainer, Cardosso being an academic turned president of one of the BRICS, he was bound to have tons of materials fit for this, off the top of my head I gave that name.
Muda si mrefu akanishukuru sana kwa sababu alipata materials kibao, na hata hakumjua president Cardosso. Na sio yeye tu, darasa lake zima la Ph.D walikuwa hawajawahi kumsikia, wanamuuliza "wewe umemsikia wapi huyu?" mtu kawa rais wa Brazil kwa miaka 8, 1995-2003.
Na nikiangalia kweli, wanasoma sana, lakini kila wanavyozidi kusoma ndo wanavyozidi ku specialize kwenye vitu vidogo kiasi kwamba hawana muda na vingine. Enzi za Renaissance men wanaojua mengi zinapita.
Sasa ukiangalia Ph.Ds kama watu wasio na muda wa kuwajua watu kama kina Cardosso unaweza kusema dhana nzima ya kupima usomi kwa Ph.D ni potofu. Unaweza kupima u specialist kwa Ph.D, lakini u specialist na usomi si kitu kimoja.
kwa post ya ndugu kiranga-ambayo nakubaliana nayo- wanaume wasiogope kuoa wasichana wenye PhD. Ni kwaWa
Inategemea Chuo kikuu umesomea digrii, maters na Phd za nini??!!!
Mf. Education (ualimu) ni kifo cha mende, hata ukiwa profesa
Uganga wa kutibu ( kazi kulilia mishahara na rushwa)
Haaaaaaaaaaa
Lakini kwa watu wa biashara, lazima utakuwa tajiri tu!! Bilivu mi, ukiwa na Bcom, then MBA.... Hapo ni ****-make bingo tu, njia nyeupeeeeee
Nimekujibu!!!
Sijajua kama unazungumzia utajiri,uhalisia au jinsi ilivyo.
Kwanza kuwa na PhD au masters sio kusoma sana ni kipimo cha elimu ya mtu
Kuhusu uhalisia ni kuwa hakuna mahusiano ya kusoma na kipato kwa kuwa labda niseme ni mazoea tu yametufikisha mahali tunadhani kusoma na kipato vina mahusiano.
Kama unazungumzia utajiri,ni kuwa kuwa na PhD sio kuwa tajiri.Shuleni na vyuoni hatufundishwi kutafuta au kuwa tajiri.Wapo watu hawajaenda hata shule ya msingi lakini wana kipato kikubwa.
Jinsi ilivyo ni kuwa wale "walio soma sana" hulipwa fedha nyingi lakini hii haina maana kuwa ukisoma kwa kiwango fulani ndo utakuwa na kipato kikubwa au utajiri.
Juzi wametangazwa list ya matajiri 40 africa wakiongozwa na Aliko Dangote, wote 40 hakuna hata mmoja mwenye masters..
Na bongo napo tukatajiwa list ya matajiri wa 5 wakiongozwa na bakhresa na katika wote watano mwenye masters ni mzee mengi tu wengine wote hakuna kitu lakini ndo wana pesa mbaya..
Kwa wanaotafuta utajiri mkubwa hawawezi kusoma sana as shule inachukua mda mwingi na wao hawana huo muda idle wa kusoma as mda mwingi wanatumia kusaka pesa na utajiri