Hivi kuna uhusiano gani kati ya maji ya Kilimajaro na Serikali?

Habari za mihangaiko wakuu?

Nimekua nikifuatilia mara kwa mara warsha, sherehe au hata semina zinazousu serikali. Kila inapotokea kuna shughuli yoyote ya kiserikali basi utakuta pale meza kuu maji yiliyowekwa ni Kilimanjaro pure drinking water.

Sijawhi kuona shughuli yoyote ya kiserikali wameweka maji ya uhai, safina, masafi etc.
Hivi kutakua na uhusiano gani kati ya serikali na hayo maji ya kilimanjaro?
Hata mimi nimekuwa nikijiuliza swali hilo kila ninapofika kwenye mikutano kwa maji ni Kilimanjaro tu?
 
Mi nadhani ni brand na pia yeye ndio alikuwa wa kwanza kushika soko.
Kuna uwezekano tender za mwanzo kabisa alizikamata yeye. Kwahyo mazoea yanaendelea.
Halafu tusisau kuwa maji ya Kilimanjaro ni maji yaliyoanza kutengenezwa zamani sana... kabla kila mjasiriamali hajaja na brand yake! Kipindi yanatoka ilikuwa ni watu wenye fedha ndefu tu ndio utawaona wanayanywa. Hivyo umaarufu wake umeanzia mbali. Ofcourse na watengenezaji wake wamejitahidi kuyafanya yaaminike!
 
Mkuu ukiwa na maisha magumu utamlaumu mtu? Mbona unafatilia ishu ambazo sio za msingi? Muda wa kufatilia hayo maji si ungekaa na familia yako
Kwa nini wewe huu muda wa kuchangia hii thread, usikae na familia yako? ........... Hata hivyo JF kuna nyuzi na majukwaa kibao kama hupendezwi ma kimoja wapo piga chini........ Kwani lazima usome au uchangie kila nyuzi............hivi ingekua nyuzi haina mashiko si moderator wangeifuta tayari? .......... Huu utaratibu wa kupangiana cha kupost munaotoa wapi?
 
Kwa wale waliosoma Marjeting walitakiwa walielewe hili kirahisi, inaitwa "Brand loyalty".
Mfano mwingine ni chewing gum(big G), soda(coke) etc.
Lakini pia ni status iliyojijengea, ni Heineken fulani hivi katika aina za maji
 
Bro; maji ya Kilimanjaro processing yake inafanyika at source; Shirimatunda at the foot of the mountain baada ya barafu safi kuyeyuka na kushuka toka kileleni maelfu ya mita kupitia mabonde yasiyojua uchafuzi wa mazingira ni nini. Huwezi kufananisha na vinyesi vinavyochimbwa hapo Vingunguti au Kijiwe Samli pale Jet maeneo yalitojaa kemikali hatari. The reason is obvious.
 
Kuna maji yanatengenezwa iringa yako poa sana
Hayo maji ya Iringa mkuu kuna jamaa yangu alikuwa anayauza jumla ni mazuri sana, kama miaka 3 yalimtoa na hiyo biashara kaachana nayo, yalikuwa yanafungwa kwenye box sijui kama hadi sasa hivi ndiyo pakage yake...


Maji ya Kilimanjaro yana promote Mlima Kilimanjaro, ndiyo maana huwa yanatumika sana kwenye dhifa mbali mbali za kiserikali au binafsi...

1.jpg
 
Kwa nini wewe huu muda wa kuchangia hii thread, usikae na familia yako? ........... Hata hivyo JF kuna nyuzi na majukwaa kibao kama hupendezwi ma kimoja wapo piga chini........ Kwani lazima usome au uchangie kila nyuzi............hivi ingekua nyuzi haina mashiko si moderator wangeifuta tayari? .......... Huu utaratibu wa kupangiana cha kupost munaotoa wapi?
Wakati ujao ukinijibu kitu jitahidi uandike kiswahili lugha zenu za nachingwea sizitaki
 
Nikinunua maji tofauti na Kilimanjaro nayamaliza hapo aunt natupa chupa likiwa name maji niliyobakiza.

Ila Kilimanjaro naweza hata kuzunguka na maji muda mrefu.
 
Kwa upande wa quality huwezi fananisha Kilimanjaro na brand yeyote ile kwa hapa bongo coz nilijaribu kutumia aina kadhaa za water brand kama rungwe, uhai, dasani na Kilimanjaro aisee Kilimanjaro inawaacha mbali sana hao wenye brand zingine
 
Back
Top Bottom