Hivi kuna ubaya gani tukifanya siasa za kuvumiliana pasi na kuumizana?

Suzy Elias

JF-Expert Member
Nov 9, 2021
1,067
6,193
Kwanini CCM hutumia gharama za aina yeyote ili tu kubakia madarakani kipi wanahofia endapo watapatikana wengine kuongoza nchini?

Yanini tunakubali kujiandalia kisasi cha haja kwa mambo ambayo yanaepukika jsmani?

Kwani leo akitawala CCM na kesho NCCR keshokutwa Chadema kuna ubaya gani?

Hivi leo Mbowe awe Rais wa Nchi kisasi kwa Samia kinaepukikwa vipi?!

Hivi leo Chadema wawe watawala katika Nchi hii wana CCM hiyo amani mtaitoa wapi?!

Ukweli ni kwamba CCM na Viongozi wake popote walipo kwa haya manyanyaso kwa wafanya siasa wenzenu ni hatari kwa ndoto na maisha yenu ya baadae.

Kwa ninachokiona sasa NI RAHISI KWA MAGUFULI KUSAMEHEWA NA CHADEMA NA SI SAMIA.

Muda utaongea.
 
Hii nchi inawenyewe na wenyewe ni CCM,wengine msubiri mgawo ,kama tutaona ipo haja ya kuwagaia ubunge nafasi mbili tatu,kama tutaona tuwaingize kwenye serikali yaani kila kitu, sisi ndio tunaoamua.

Na kama mkisusa basi tunawachukua kutoka hukohuko kwenu na kuwaingiza kwa nguvu kwenye vyombo husika kama kule bungeni,hakuna wa kutuzuia.

Wapinzani hisabuni miaka tuu,ila serikali mtaisikia ikitajwa na kuandikwa lakini haitotokana na wapinzani. Na hamna vya kujipanga wala kujipangua ,tumeona mmekuja na Ukawa sijui ukuta sasa ugaidi ,chezea dola.

Tunawaweka jela aafu tunawaachia,yaani CCM inawachezea masharubu wapinzani.
 
CCM ni kundi la mafisadi lililokamata bunge, mahakama, polisi, na serikali yenyewe, ni wachafu kwa matendo yao waliyowafanyia watanzania ndio maana wana hofu itakuwaje siku wakiondoka madarakani.

Unapoona wamejitungia sheria za kinga jiulize wanaogopa nini kama wao ni wasafi? hiki ndicho kithibitisho namba moja kinachowafanya waogope kuitoa hii nchi kwa wapinzani.

Lakini sababu ya pili ni umimi, wamevimbiwa na madaraka, wameigeuza nchi yetu ya kifalme; baada ya wazazi wao kushiba sasa ni zamu ya watoto wao, ndio maana leo unaona majina ya watoto wengi ambao wazazi wao walishakuwa viongozi awamu zilizopita nao wameanza kuonjeshwa mema ya nchi.

Kadiri muda unavyozidi kwenda, ndivyo ambavyo wanazidi kujichimbia mizizi, sitoshangaa wakati ukifika Mungu akitujalia uhai, na hao watoto wao watarithisha madaraka ya nchi yetu kwa wajukuu wao, huku wengine tukiendelea kuitwa wapiga kura ambao hata hizo kura zetu haziheshimiwi.

Untill the day we wake up, tutaendelea kuchezewa huku tukiishia kuandika tu mitandaoni wakati wao wakiendelea kuitafuna nchi yetu na matunda yake, sisi kazi yetu ni kuendelea kumwagilia miti ya hiyo matunda.

Bado tuko utumwani nawaambia, hatuna uhuru wowote, na yeyote anayefurahia hali tuliyonayo hivi sasa ni either mjinga asiejielewa, au nae ni sehemu ya wanyonyaji wa nchi hii, sorry nimemwaga povu la kutosha coz this is the only forum I possess.
 
Kwanini CCM hutumia gharama za aina yeyote ili tu kubakia madarakani kipi wanahofia endapo watapatikana wengine kuongoza nchini?

Yanini tunakubali kujiandalia kisasi cha haja kwa mambo ambayo yanaepukika jsmani?

Kwani leo akitawala CCM na kesho NCCR keshokutwa Chadema kuna ubaya gani?

Hivi leo Mbowe awe Rais wa Nchi kisasi kwa Samia kinaepukikwa vipi?!

Hivi leo Chadema wawe watawala katika Nchi hii wana CCM hiyo amani mtaitoa wapi?!

Ukweli ni kwamba CCM na Viongozi wake popote walipo kwa haya manyanyaso kwa wafanya siasa wenzenu ni hatari kwa ndoto na maisha yenu ya baadae.

Kwa ninachokiona sasa NI RAHISI KWA MAGUFULI KUSAMEHEWA NA CHADEMA NA SI SAMIA.

Muda utaongea.
In short, sisiemu hawako tayari kuachia madaraka kwa njia ya kura kwa namna yoyote ile. Katika maneno na matendo yao hilo wamelidhihirisha wao wenyewe. Ukifuatilia matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020, hilo utaliona waziwazi.
 
Kwanini CCM hutumia gharama za aina yeyote ili tu kubakia madarakani kipi wanahofia endapo watapatikana wengine kuongoza nchini?

Yanini tunakubali kujiandalia kisasi cha haja kwa mambo ambayo yanaepukika jsmani?

Kwani leo akitawala CCM na kesho NCCR keshokutwa Chadema kuna ubaya gani?

Hivi leo Mbowe awe Rais wa Nchi kisasi kwa Samia kinaepukikwa vipi?!

Hivi leo Chadema wawe watawala katika Nchi hii wana CCM hiyo amani mtaitoa wapi?!

Ukweli ni kwamba CCM na Viongozi wake popote walipo kwa haya manyanyaso kwa wafanya siasa wenzenu ni hatari kwa ndoto na maisha yenu ya baadae.

Kwa ninachokiona sasa NI RAHISI KWA MAGUFULI KUSAMEHEWA NA CHADEMA NA SI SAMIA.

Muda utaongea.
Magufuli ameshapatwa na yake bado Samia.
 
Back
Top Bottom