Hivi kuna tofauti ya Jaza- Ujazwe vs Jaza- Ujaziwe?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,898
43,802
Hivi Tigo wanamaana gani kutumia neno 'Ujazwe' badal ya 'Ujaziwe', haya ni maneno mawili tofauti naamini. Kwakuwa inayo jazwa ni simu na sio wewe, hivyo wanakujazia na sio kukujaza. Tigo mkiendelea na hiyo caller tune yenu nitawajaza.
 
Hili tangazo la JAZA UJAZWE linafaa lifutwe kabisa. BASATA lizuieni kama mnavyozuia nyimbo zisizo na maadili. Sio kama TIGO hawajui kwamba ni lugha chafu. Wanajua kabisa kwamba tangazo sahihi linapasa kuwa JAZA UJAZIWE. TCRA tafadhalini walazimishe wajirekebishe. Wanaposema 'ujazwe...' wana maana gani? Wanawake (ashakum si matusi) ndio wanaojazwa mimba. Sasa TIGO inawajaza nini wanapojaza simu zao muda wa maongezi?
 
Back
Top Bottom