Hivi kuna tofauti gani tukiwa na baraza la mawaziri na lisipokuwapo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna tofauti gani tukiwa na baraza la mawaziri na lisipokuwapo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makame, May 4, 2012.

 1. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nauliza hili kwa sababu zifuatazo:-

  1. Baada ya Uchaguzi wa 2010, Mheshimiwa Rais alichukua muda mrefu kabla hajatangaza Baraza la Mawaziri; katika kipindi ambacho tulikuwa hatuna mawaziri, Nchi ilizama? Ilididimia? Iliganda? Mawaziri wanakula tu.

  2. Kwa Mawaziri wanaotuhumiwa, walishawahi kukutana na kamati za bunge husika; wakaambiwa na hawakuchukua hatua kurekebisha dosari husika. Sasa kama Mawaziri wanaelezewa dosari kinaga ubaga, na hawajachukua hatua; kuna haja kweli ya kuwa nao????

  3. Taarifa ya CAG kabla haijawasilishwa Bungeni ina mikondo yake inayopitia; na kama CAG amekuwa akiripoti kila mwaka; na Mawaziri wanayawacha mulemule ndani ya mjengo kama vile CAG alikwenda kuwatumbuiza; Mawaziri hawawajibiki, mpaka kelele zipigwe na wabunge; kweli kuna haja ya kuwa nao?

  Wana JF, hizo ni fikra ; leteni mawazo yenu
   
 2. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  ..nchi bila baraza la mawaziri???katiba inataka liwepo so for the tym being ni lazima liwepo, wakati wa kutoa maoni kwenye tume ya mabadiliko ya katiba katoe hiyo hoja lakini huku ukiwa na mkakati mbadala utaowezesha kazi zilizokuwa zinafanywa na mawaziri zifanywe bila wao kuwepo..sio mbaya uka share nasi hapa unadhani badala ya cabinet pawe na nini???
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tuache kupotosha na kujenga hoja nyepesi baraza la mawaziri ni la muhimu sana.

  Mapungufu ya mawaziri mmoja mmoja hayaondoi umuhimu wa baraza hilo.
   
 4. K

  Kasimpya Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mawaziri ni muhimu kuwepo kwa sababu ya kutekeleza sera za chama kinachotawala. Cha maana ni mawaziri hao kuwa wachapakazi na waaminifu.
   
 5. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  lisipokuwepo wizi utapungua !
   
 6. C

  Cosmas.olomi Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tofauti ipo ila kwa baraza lilopita ni kama 50 kwa 50 ,sababu Kuna bahadhi ya mawaziri kazi zao zinaonekana waziwazi kuwa zina manufaa kwa jamii na kuna mawaziri wako kimaslahi zaidi ambao wasingekuwepo nadhani taifa lingeokoa pesa ambazo zimefisadiwa na hao mawaziri.   
Loading...