Hivi kuna tofauti gani kati ya wafanyakazi wa trl na tazara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna tofauti gani kati ya wafanyakazi wa trl na tazara?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Oct 2, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni muda mrefu sasa masikio yetu yamesikia matatizo ya wafanyakazi wa TAZARA.Hata hivyo sioni kama yupo mtu anayesikia kilio chao.Kama kawaida yake serikali ime endelea kunyamaza kimya kana kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya serikali na TAZARA,na kwamba haihusiki kabisa na matatizo ya wafanyakazi hawa.Tumesikia kwamba wafanyakazi wa TAZARA hawajalipwa mishahara yao kwa miezi mitatu sasa.Kwanza niwape pongezi wafanyakazi hawa kwa uvumilivu wao mkubwa.Sijui hata wanaishije.Halafu katika hali isiyo ya kawaida kabisa wanaendelea kufanya kazi,tena ngumu za kufunga mafurushi na kuyapeleka kwenye vyumba vya kuyahifadhia tayari kupakiwa kwenye mabehewa.Swali ninalo jiuliza mimi ni kwamba,hivi kuna tofauti gani kubwa hasa kati ya wafanyakazi wa TRL na TAZARA? Kwa mtazamo wangu mimi hakuna tofauti yeyote,kwa vile wote wako kwenye mashirika yanayomilikiwa na serikali ingawa TRL kwa kiasi kidogo na wote wanatoa huduma kwa wananchi.Kwa mtazamo mwingine ningesema serikali ingepashwa kuwahudumia zaidi wafanyakazi wa TAZARA kwa vile wao hawana muwekezaji.Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa, serikali imewasaidia wawekezaji uchwara wa TRL kulipa mishahara ya wafanyakazi wao, huku ikiwaacha wafanyakazi wa TAZARA wakihangaika.Mantiki hasa ya kitendo hiki binafsi siioni.Hizi ni 'double standards' ambazo zinaendelea kuleta hisia za rushwa katika mkataba mzima wa TRL.Ninaiomba serikali ichukue hatua za haraka za kuwasaidia wafanyakazi hawa wa TRL kwa vile hili ni jukumu lao la msingi.
   
Loading...