Hivi kuna siri/mahusiano gani kati ya pilau au sherehe /sikukuu fulani

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Yaani ningependa kujua hivi kwa nini katika sikukuu au sherehe fulani au shughuli yeyote ile iwe ya furaha au majonzi/huzuni kwa nini pilau lazma ipikwe na sio chakula kingine kile kisichiendana na mchele.
 
itakuwa ule wali mchafu kama sikosei mleta mada naona umelimiss pilau changanya ukiwa hauna hela kila kitu nikutamani tu hata chumvi
 
labda huko kwenu mjini..ila huku kwetu Serengeti huwa ni ugali wa mtama na nyama nyumbu
 
Yaani ningependa kujua hivi kwa nini katika sikukuu au sherehe fulani au shughuli yeyote ile iwe ya furaha au majonzi/huzuni kwa nini pilau lazma ipikwe na sio chakula kingine kile kisichiendana na mchele.

Ni ujinga wa watanzania wanafikiri kula pilau ni dili wakati ni kitu cha kawaida sana.
 
Sisi sherehe yoyote bila ebitoke, nyama na maharagwe haijanoga. Uweke na nyanya chungu yaani nsanyuse hapo sasa.
 
Yaani ningependa kujua hivi kwa nini katika sikukuu au sherehe fulani au shughuli yeyote ile iwe ya furaha au majonzi/huzuni kwa nini pilau lazma ipikwe na sio chakula kingine kile kisichiendana na mchele.
Ni msosi special unaohitaji maandalizi nengi ambao hauwezi kupikwa kila siku.. Ni sawa tu na kwenye mahusiano kuna siku maalum za 'kutunukiwa'
 
Yaani ningependa kujua hivi kwa nini katika sikukuu au sherehe fulani au shughuli yeyote ile iwe ya furaha au majonzi/huzuni kwa nini pilau lazma ipikwe na sio chakula kingine kile kisichiendana na mchele.
Pilao/wali nazi ni kitu kingine dingiiii!
 
Ni ujinga wa watanzania wanafikiri kula pilau ni dili wakati ni kitu cha kawaida sana.
Si ujinga mkuu hii kitu inaendana na uhalisia. Zamani ugali ulichukua nafasi kubwa sana kiasi kwamba ukipikwa wali nyumba fulani watoto wa majirani hawabanduki maeneo hayo na ilizoeleka huwa unapikwa siku maalamu. Sasa kwa kitu pilau lenyewe ilizoeleka katika matukio maalum haswa kipindi cha sherehe. Sasa pilau sio kipindi hicho tena, limezoeleka kiasi kwamba hata wewe unasema ni kitu cha kawaida lakini imezoeleka ni chakula chenye mvuto kwa masherehe hata mikusanyiko..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom