Hivi kuna nyimbo za injili za kuchezeka na kuhamusha ari ya kumsifu Mungu kama za AIC?

Online Pastor

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,949
2,000
Miye ni muumini mkubwa wa nyimbo bora za injili,na hata maktaba yangu ya nyimbo imejaa nyimbo toka madhehebu karibu yote.

Nina old and new school songs za RC,KKKT,SDA,AICT na nyinginezo.

Binafsi,miye nimezaliwa katika u-KKKT na japo nilishaachana na udhehebu,ila navutiwa zaidi na nyimbo za AICT!

Kuna jinsi wanavyopiga yale ya magita yao mpaka roho inauwiwa kububujika.Kuna kwaito inapigwa mule mpaka moyo na roho vinafurahia

Hivi niko peke yangu ninayeyaona haya?

Wewe unapendelea nyimbo zipi za injili?
 
wilcoxon

JF-Expert Member
Jun 25, 2017
974
1,000
Siyo pekee yako mkuu katika upande wa kwaya A.I.C.T wapo vizuri, ngoja nikupe list yangu
1.CHANG'OMBE VIJANA CHOIR (CVC) hii kwaya kwa upande wangu hawajawahi kutoa kitu kibaya always album zao huwa ni hatari now days nyimbo zao zinatumika mpaka D. R. C Congo.

2.Neema Gospel Choir (A. I. C. T CHANG'OMBE) hawa watu na wenyewe ni balaa gita huwa zinapigwa ni hatari wana watu wanasauti kweli mfano Mage And Samweli Limbu hafu hawa jamaa kwa uimbaji wa live wapo vizuri sana.

3.A. I. C. T Shinyanga sasa hawa na wenyewe ni balaa hawajawahi kukosea. Huwa nawapenda kweli.

4.A.I.C.T makongoro hawa na wenyewe wapo vizuri kuna siku mkuu wa kaya alienda mwanza na wenyewe walikaribishwa kuimba kilichotokea mkuu wa kaya alishindwa kujizuia ilibidi anyanyuke aende akaimbe.

Aisee kwa kifupi wapo vizuri.
 
jiwe la maji

JF-Expert Member
May 17, 2014
1,064
2,000
Binasfi nakubari uwimbaji wa kwaya wenye lafudhi za kisukuma unaotumia magita zaidi ya kinanda.

Kuna kwaya zimesha kengeuka ule uwimbaji wao wa asiri nami nimesha puuza kazi zao zote mpya. AIC Kambarage, Makongoro, Sauti ya Jangwani, Nkinga Christian choir, na Barabara ya 13 Ulyankuru.

Sijawahi kuzikubali kwaya za mbali na huku isipokuwa KKKT Mabibo albam ya Sauti ikatoka na kwaya za RC za zamani.
 
Kaizer

JF-Expert Member
Sep 16, 2008
25,281

Mkuu nimekusoma with interest. Mwaya za RC za sasa zina utofauti gani na za zamani?
 
elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,071
2,000
Miye ni muumini mkubwa wa nyimbo bora za injili,na hata maktaba yangu ya nyimbo imejaa nyimbo toka madhehebu karibu yote.

Nina old and new school songs za RC,KKKT,SDA,AICT na nyinginezo.

Binafsi,miye nimezaliwa katika u-KKKT na japo nilishaachana na udhehebu,ila navutiwa zaidi na nyimbo za AICT!

Kuna jinsi wanavyopiga yale ya magita yao mpaka roho inauwiwa kububujika.Kuna kwaito inapigwa mule mpaka moyo na roho vinafurahia

Hivi niko peke yangu ninayeyaona haya?

Wewe unapendelea nyimbo zipi za injili?
Mimi gospel za kuchezeka kwangu no nadhani gospel zinaguza na kukufanya utafakari ni zile za kusikiliza mfano nyimbo za kuabudu.
Nyimbo za Ambone Mwasongwe kama nguvu ya msamaha, kuaminiwa na Mungu, karibu yesu, ambha yawe na sayuni za Mzee wa Upako, ebeneza - Paul nani sijui yule mkenya, baba yetu - Jackson Benty
Nyimbo za kuchezeka personally naona zinazingua ndiyo maana sijawahi kumwelewa rose mhando labda kwa wimbo mmoja ule wa uko kama raggae unaitwa nitashukuru.
 
Al-Watan

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
11,920
2,000
AIC walipiga mpaka reggae. "Stir It Up" ya Bob Marley, wakaimba "Tembea Naye" wakimaanisha tembea na Yesu.

Kwaya si lazima iwe depressing.
 
Online Pastor

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,949
2,000
elmagnifico

Ambwene,nimetokea kumkubali hasa katika albamu yake hii ya sasa.
Nazikubali nyimbo za kadhaa kama:Upendo,Misuli ya Imani.

Rose Muhando alifanya vizuri kwenye ile Albamu yake ya kwanza ya Mteule Uwe Macho.
Miye binafsi hii Albamu pekee ya Rose ninayoikubali,kwani aliimba kwa moyo,na ndiyo albamu pekee ya Injili ambayo nimekariri mashairi ya nyimbo zote mwanzo mwisho.
Hii albamu ilitikisa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom