Hivi kuna nini STAR TV mbona hiki kipindi kimetoweka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna nini STAR TV mbona hiki kipindi kimetoweka?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Sep 30, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280


  Asubuhi ya saa 12.30, STAR TV, kila siku walikuwa wanarusha hewani kipindi cha “someni magazeti” lakini katika kipindi hiki cha uchaguzi wameingia mitini na sasa hivi ni vigumu kukukubali hoja za “sababu zisizoweza kuzuilika” ili tuafiki hili pazia nene la vichwa vya habari vya magazeti.

  Ninahisi kuna mkono wa CCM baada ya kuona mambo ya ushindi wa asilimia themanini wa mwaka 2005 sasa yameyeyuka…….Na Ikulu iko mashakani………………

  Kama kuna mwanajamvi mwenye taarifa zaidi anijulishe ili nami nielimike vinginevyo basi nitabaki na hisia zangu ambazo yawezekana kabisa siyo sahihi
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Huwa naskiza wakisoma magazeti asubuhi kupitia RFA, lakini sina hakika kama na kwetu kijijini wanasikia au wanapigiwa miziki ya Viky Kamata?
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hahaha hahaha
  kila mwana atarejea nyumbani this time.
  kipindi kigumu sana kwao hiki.
  tatizo tuna vyombo huru vya habari vya kuhesabika nchini. vyote vilivyosalia ni mamluki na wapanda mbegu mbaya dhidi ya jamii.
  Ndo maana kila kukicha unasikia fulania ameacha utangazaji kajitosa siasa
   
Loading...