MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Wakuu binafsi siungi mkono ukwepaji wa kodi unaofanywa na baadhi ya watanzania wasiokua waadilifu mahali popote nchini lakini kwa hili acha tu nami niseme neno kidogo.
Binafsi Mimi sio mtaalamu sana wa mambo haya lakini kwa uzoefu wangu wa kazi hiyo mwaka moja niliowahi kukaa pale chini ya mwalimu wangu bwana Chilagi ambaye meneja wa Sumatra nyanda za juu kusini kwa sasa sitaki kuamini kwamba eti tunaambiwa Makampuni zaidi ya 200 yanafungiwa kujishughulisha na kazi hizo kisa tu ni ukwepaji kodi! Hapana,huu ni kama uonevu mkubwa uliofanywa naamini na baadhi ya watu ambao walimpa Rais details zisizozokua sahihi.
Sina interest yoyote kwenye kampuni yoyote ya uwakala Bandarini lakini mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Ni ngumu sana kwa utaratibu wote ninaoufahamu wa clearing mtu kupitisha mzigo bila kulipia, kwa milolongo yote mpaka mzigo unatoka si rahisi mziogo ukatoka bila kulipiwa tusidanganyane hapa! Inawezekana pia yapo Makampuni yalikua yanakwepa kodi lakini hayawezi kua yote 200.
Serikali ikubali isikubali kwa sasa itakosa mapato kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu kwa sasa kuna Makampuni mengi sana ya nje yameshakosa imani na Makampuni ya ndani hali inayowapelekea Makampuni hayo kufikiria kutumia mawakala wa Makampuni ya nchi zingine kusafirishia mizigo ya wateja wao. Hili serikali yetu isipoliangalia kwa umakini wake madhara yanaweza kua makubwa sana tena sana.
Tusimung'unye maneno hapa tatizo lilikua TPA na TRA bado uchunguzi haujafanyika wa kutosha na inawezekana kamchezo hako bado kapo sasa! Mizigo yote inalipiwa ila malipo yake huishia kwenye mikono ya watumishi waliokua waaminifu wa TPA na TRA na hapa kuna taarifa pia baadhi ya maafisa wa benki hasa CRDB pia wanahusika na ujanja huo.
Sitaki kwenda mbali sana zaidi ya kuiomba serikali ipime kwa umakini uamuzi wa kuyafungia Makampuni yote zaidi ya 200 Bandarini.