Hivi kuna mtu anayeweza kunipa sababu kwa nini EKELEGE hajakamatwa mpaka leo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna mtu anayeweza kunipa sababu kwa nini EKELEGE hajakamatwa mpaka leo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chilisosi, May 7, 2012.

 1. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu wana jamaii,
  Naomba mnisaidie hili jambo linalonitatiza kwa muda mrefu lakini nakosa jibu.
  Hivi kwa nini huyu Ekelege hafanywi lolote mpaka hadi waziri anafukuzwa kazi lakini mie nasikia tu Ekelege yuko ofisini anaendelea kukusanya hela za vyeti vya ukaguzi wa magari ambapo vijana wake WTM UTILITY ya London ndio wawakilishi wake huku na wanakusanya hela bila hata aibu mchana kweupee vyeti unapewa baa tu. Tunajua kuwa huyu mwenye WTM ni mtoto wa aliyekuwa mkurugenzi hapo TBS kabla ya Ekelege na pia ndie anayelipa ada ya shule ya mtoto wa ekelege huku ulaya. Lakini kinachoniumiza kichwa ni kwa nini hawafanywi kitu hawa wezi? Licha ya kuwa hii tenda waliitoa kiholela lakini pia muda wake walioipatia wa miaka mitano tayari umekwisha lakini jamaa bado tu wanauza vyeti. hapa inakuwaje hapa mbona watanzania tunafanywa wajinga hivi mpaka lini?
  .
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukweli kitendo cha Bwana Ekelege kuendelea na kazi mpaka sasa ni aibu na fedheha kwa serikali. Na sasa naanza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu hukume aliyopata Waziri Chami. Inawezekana kabisa Chami hakuwa na ubavu kwa huyu bwana na ametolewa kafara!. Pamoja na makelele yote bungeni na hata kwenye CC bado huyu bwana yuko ofisini, kwa vipi?

  Tuhuma zimetolewa, ushahidi umewakilishwa bungeni, mwanasheria mkuu ameandika lakini Ekelege bado yuko kazini! Mbona Blandina Nyoni alisimamishwa mara moja? Ekelege ana nini? Hata kama watamsimamisha kesho lakini kwa muda ambao amekaa ni dhahiri hakuna waziri yoyote ambaye angeweza kupambana naye.
   
 3. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Ukiona ivyo ujue maovu aliyofanya kuna mikono ya wakubwa la sivyo angeshachukuliwa hatua muda mrefu sana.
   
 4. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nchi hii mambo kama haya yanafanyika kwa network kubwa, ukiona hivyo ujue hayuko peke yake, na sasa analindwa!
   
Loading...