Hivi kuna mikakati ya kuunemesha ulimwengu au kuuangamiza. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna mikakati ya kuunemesha ulimwengu au kuuangamiza.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Oct 2, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimechoka mwenzenu tena nasema nimechoka .Nimechoka kusikia kila aina ya misaada na mikakati ya kuunemesha ulimwengu na Tanzania,lakini kila kukicha mjomba wangu,shangazi yangu binamu yangu nk.anazidi kuwa maskini.Kinachoendelea hasa ni nini?Sasa Tanganyika sijui kuna MKURABITA,sijui MKUKUTA lakini najua mambo ni yale yale,kuzidi kwa umaskini.Tulidhani matatizo haya yako Africa,Asia na Marekani ya Kusini tu,kumbe sio.Wamarekani ya Kaskazini na Ulaya nao karibuni watakuwa kama sisi.Mabenki yamekula hela na kufirisika,sasa wanachukua za Benki kuu ya Marekani na Uingereza,wakizimaliza sijui itakuwaje.Watu wanaachishwa kazi kwa maelfu,lakini kinachoendelea hasa ni nini jamani?Je tuliingizwa mkenge katika udanganyifu wa mifumo ambayo haiko 'sustainable?' Na mbona mambo haya yanaonekana kama yamepangwa? Mm,shida tupu.
   
Loading...