Terminator
Member
- May 27, 2009
- 32
- 10
nimekuwa nashangazwa sana na akili za watu kutokana na matendo ambayo binadamu hufanya, maana katika maisha kuna binadamu wameamua kuishi katika aina fulani ya maisha, mfano mwizi au jambazi, ushoga, mlevi wa kupindukia,na mambo mengine mabaya kama hayo ambayo watu hao ndio identity yao katika jamii.watu wa aina hii sio wa rahisi kuwashangaa kwa sababu ni tabia zao ambazo zinatambulika katika jamii.
ila hili la mtu ambaye usiye mtegemea kuvaa ukichaa na kufanya mambo ambayo yanaishangaza jamii, nasema hivyo kutokana na wimbi lilivyo sasa kwa mtu yeyote anaemiliki gari,kwa sasa ikitokea umepata ajali aidha uwe umesababisha au umesababishiwa na unakuwa katika wakati mgumu kutokana na watu wa maeneo utakapopata ajali kukosa utu, huwezi pata msaada wa watu kukuokoa ,kinachofanyika ni wizi kwanza mengine baadae kwa wale wenye utu ila asilimia kubwa ya watu hukimbilia mali na hata kama una vitu kama dhahabu unaweza katwa sikio au mkono ilimradi mhusika apate mali,
tabia hii kwa kweli inakera sana, maana hujui nini kitakutokea wakati wowote uwapo safarini. mfano kuna jamaa yangu wa karibu alibanwa na lori njiani ikabidi atanue kuepusha ajali akaenda kumgonga mwendesha pikipiki, kwa bahati mwendesha pikipiki alipata michubuko ila sasa,mwenye gari aliyegonga alitaka asimame ili kutoa msaada na pia kusubiri askari wapime,ila kilichotokea ni raia walianza kurusha mawe kwenye gari jamaa aliamua kuondosha gari yake kunusuru maisha yake.kwahiyo kilichoendelea ule msaada wa kumpeleka hospitali hakuwepo tena,pia gari husika halikupatikana tena.
pia hili lililotokea karibuni kwa marehemu sharo milionea, yaani limenikera sana watu badala ya kumsaidia waliamua kumvua nguo maana anaona kama kumpiga sachi anachelewa bora aondoke na nguo aende kuzikagua mbele ya safari. kitendo hicho ni cha kidhalilishaji, aidha namshukuru mkuu wa wilaya ya muheza kwa maamuzi aliyochukua ya kuwatafuta wote waliohusika katika kitendo hicho, na ninaamini watapatikana maana wote ni wakazi wa eneo hilo.
kwa hiyo hali hii ndio maana nashindwa kujua ni umaskini wetu umeondoa utu wetu badala ya kusaidia majeruhi au marehemu, mtu anakimbilia mali. hata utambuzi wa mhusika unakuwa mgumu kutokana na document muhimu za mhusika kuwa zimeibwa.
watu hawa ni ndugu zetu na wanahudhuria misikitini na makanisani,ila matendo haya kweli ni kinyume na maandiko tunayosoma.