Hivi kuna mahusiano gani ya majani Kifa Uongo na mwili wa binadamu

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
18,679
2,000
Kuna mmea fulani hivi (nimeusahau jina)unaotaka karibu na nje kama ua fulani.
Huu mmea ukiugusa kwa mkono eti unasinyaa hapo hapo kama unakauka fulani lakini baada ya mda unarudi tena ile hali yake ya kawaida (ki nyumbani tunauitaga kifabuongo.

Yaani zamani tulipenda sana kuuchezea.

Je, huwa kuna sayansi gani kati binadamu ya kuugusa ndio unazimia.
 
Jackson94

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
366
500
Kuna mmea fulani hivi (nimeusahau jina)unaotaka karibu na nje kama ua fulani, huu mmea ukiugusa kwa mkono eti unasinyaa hapo hapo kama unakauka fulani lakini baada ya mda unarudi tena ile hali yake ya kawaida (ki nyumbani tunauitaga kifabuongo.

Yaani zamani tulipenda sana kuuchezea. Je! huwa kuna sayansi gani kati binadamu ya kuugusa ndio unazimia.
Huwa haukauki bana sema unasinyaa tu.
 
Kamongo

JF-Expert Member
Mar 20, 2009
980
1,000
... uzushi Mkuu! Sio binadamu tu; ukiguswa na chochote hata kuku unasinyaa. In short hakuna mahusiano yoyote kati yake na binadamu tuache stori za kusadikika.
Sishangai watz mkiendelea kuwa masikini mna Imani za ajabu sana
 
Carleen

JF-Expert Member
Nov 6, 2018
4,612
2,000
Basii kawaelewa ni kuwa unasinyaa, haya mpeni majibu siyo mna kazi ya kumponda tu hata kumuelewesha hamumueleweshi..!

Mtoa mada, kama sijakosea hiyo huwa ni defense mechanism ya huo mmea ukihisi hatari, ni kama vile mdudu akuume ama ajifiche akihisi unamgusa..!!

Kwa undani zaidi watakuelezea wataalamu namie niko hapa nasubiri..!!
 
Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,069
2,000
Acha Uongo. Haukauki. Au unadhani watu hatuufahamu? Kwa nini Watanzania hamuwezi ongea kitu mpaka muweke na Uongo?
Unaelewa maana ya neno KAMA au unamshambulia tu mwenzako?... muwe mnaelewa lugha mtu anayotumia siyo kukurupuka kama mataahira halafu majibu yenyewe hamtoi

Tukirudi kwenye mada...
Ni kwamba mmea ule ambao unajulikana kwa jina la 'mimosa pudica' au na majina mengi mengineyo kama wanavyotaja watu, unafanya vile kujihami.

Kama ukisoma vitabu vya Sayansi utakuta sifa saba za viumbe hai (japo sifa kuu ni nne); mojawapo ya sifa saba ni kuhisi na wanatolea sana mfano mmea huo

Kuhusu kuguswa na kitu kingine (tofauti na wanyama) na kisisinyae sijafanya uchunguzi maana kimmea chenyewe nilikiona enzi hizo kwenye kujifunza somo hilo nikiwa darasa la sita na sikuwa na uwezo wa kujaribu kuchunguza sana hayo

Lakini kuna vitu vingine ambavyo sense yake inafanya kazi pale tu kikiguswa na kitu chenye uhai. Kwa mfano baadhi ya simu za tachi ukigusa kwa mkono uliovaa glovu nguo au kitu chochote kikavu kama mti uliokauka basi haifanyi kazi lakini ukitumia kitu chochote chenye ubichi au chenye majimaji basi inafunction kama kawaida. Hapa sasa huwa inashangaza pia kwani hata vile vikavu ukiviweka umajimaji basi vinafunction kama kawaida

Sasa kwa jinsi mtoa mada alivyouliza ni kama vile amefanya utafiti akagundua huo mmea ukiguswa na binadamu tu ndo unasinyaa na akigusa kwa vitu vingine hausinyai (sina hakika) kwahiyo sijajua kama huo mmea nao una act kama maelezo ya hapo juu au laa lakini hoja inabaki palepale jibu ni kwamba uhusiano uliopo hapo ni kwamba mmea huo unafanya hivyo baada ya kuhisi umeguswa (unafanya hivyo kujihami)
 
Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
2,481
2,000
1. Wewe ni girlfriend wake
Ama
2. Wewe ni yeye kwa ID nyingine

Si kwa povu hili.

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
2,645
2,000
Basii kawaelewa ni kuwa unasinyaa, haya mpeni majibu siyo mna kazi ya kumponda tu hata kumuelewesha hamumueleweshi..!

Mtoa mada, kama sijakosea hiyo huwa ni defense mechanism ya huo mmea ukihisi hatari, ni kama vile mdudu akuume ama ajifiche akihisi unamgusa..!!

Kwa undani zaidi watakuelezea wataalamu namie niko hapa nasubiri..!!
Hii kitu inaitwa "haptonasty" --- mwitikio na mjongeo wa mmea kufuatia badiliko la haraka la kiwango cha presha ya maji upande wa kati wa majani yake, na ndipo husinyaa na kujifunga, ukionekana kama umekauka. Jina: insectivorous plant mfano mojawapo ni Venus fly-trap. Pamoja na faida ya kujihami pia ni njia ya kujilisha. An insect-eating plant.
 
free lander

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
271
250
Kuna mmea fulani hivi (nimeusahau jina)unaotaka karibu na nje kama ua fulani.
Huu mmea ukiugusa kwa mkono eti unasinyaa hapo hapo kama unakauka fulani lakini baada ya mda unarudi tena ile hali yake ya kawaida (ki nyumbani tunauitaga kifabuongo.

Yaani zamani tulipenda sana kuuchezea.

Je, huwa kuna sayansi gani kati binadamu ya kuugusa ndio unazimia.
Hiyo hali inaitwa "thigmonasty". Kuna mimea inayosinyaa ikiguswa kwa ajili ya kujilinda na mingine kwa ajili ya kukamata mawindo yao (chakula). Kifauongo unasinyaa kwa ajili ya kujilinda.
 
free lander

JF-Expert Member
Nov 7, 2018
271
250
Hii kitu inaitwa "haptonasty" --- mwitikio na mjongeo wa mmea kufuatia badiliko la haraka la kiwango cha presha ya maji upande wa kati wa majani yake, na ndipo husinyaa na kujifunga, ukionekana kama umekauka. Jina: insectivorous plant mfano mojawapo ni Venus fly-trap. Pamoja na faida ya kujihami pia ni njia ya kujilisha. An insect-eating plant.
Hiyo ni thigmonasty "response to touch"
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
12,576
2,000
Basii kawaelewa ni kuwa unasinyaa, haya mpeni majibu siyo mna kazi ya kumponda tu hata kumuelewesha hamumueleweshi..!

Mtoa mada, kama sijakosea hiyo huwa ni defense mechanism ya huo mmea ukihisi hatari, ni kama vile mdudu akuume ama ajifiche akihisi unamgusa..!!

Kwa undani zaidi watakuelezea wataalamu namie niko hapa nasubiri..!!
Nakumbuka kusoma soma la Biology. Ni zamani sana ila mmea unaitwa Mimosa plant kama nakumbuka vizuri. Unasinyaa kwa sababu unaposhikwa cell za pale uliposhika zinasukuma maji yake kwenye cell zilizo karibu na zile za karibu nazo zinasukuma maji kwa zinazofuatia... kwa hiyo unakuwa ni mlolongo wa maji kuhama kwenye majani na kuhamia kwenye stem, hivyo majani yanasinyaa. Kwa nini yahame? Wanasema ni namna ya kujinga ili mmea usiliwe na wanyama kwani majani yakiwa yamesinyaa yakuwa hayatamanishi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom