Hivi kuna kipengele chochote cha Katiba au Sheria kinatoa tafsiri ya neno 'Dini' na 'Ibada'?

Abuu hanifa

JF-Expert Member
Aug 17, 2021
256
274
Kwa utafiti niliofanya kuhusu Taifa kutokuwa na Dini au Taifa kutofata dini yeyote, maneno haya yanapatikana katika katiba iliopo ile ya kiswahili pekee.

Bali sijaona maneno hayo ktk katiba ya kiingereza. Nilitatajia nikute katiba ya kiingereza ikitamka maneno haya;
  • Our state has no official religion
  • Our state is irreligion, au
  • Our state is neutral toward religion.

Bali kauli ya kuwa Taifa letu halina dini, nasikia zaidi kutoka kwa wanasiasa.

Sijui kama yupo mwanabodi anaefahamu kifungu gani cha katiba ya kiingereza inayotamka kuwa taifa letu hakuna dini au Halifungamani na dini yeyote.

Au kuna anaejua kifungu chochote cha sheria chenye kufasiri maana ya neno "Dini" na neno "Ibada"?!?!.
 
Tuoneshe wewe kifungu cha katiba iwe kwa kiswahili au kingereza kinachosema Tanzania ina dini.
Soma vizuri maelezo yangu halafu ndoo uulize swali lako vzr. Lkn kwa kukusaidia tu tafiti kutoka taasisi zinaheshimika kimataifa mfano PEWFORUMS zinaeleza kuwa nchi zinazojipambanua hazina dini hupendelea au kuipa kipaumbele moja ya dini.


Lkn muhimu zaidi kwanza kuelewa maana ya neno "dini" na "ibada" ndio tutajua iwapo Tanzania ina dini au haina
 
Back
Top Bottom