Hivi kuna kiongozi wa serikali ana ubavu wa kushusha bei za vitu? Naona kama tunadanganywa

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,494
2,040
Ingawa mimi sio mchumi wa namna yoyote, lakini kutokana na uzoefu wa utafutaji wa hapa na pale naelewa kwamba ili bei ya vitu ipande ni pale kunapokuwa na uhitaji mkubwa wa vitu kiwango kinachozidi uzalishaji.

Kwa mantiki hiyo hiyo ili vitu vishuke bei ni lazima uzalishe sana kuliko uhitaji uliopo. Lakini kama huwezi kuzalisha mwenyewe basi utalazimika kuagiza toka nje au uruhusu watu waagize toka nje.

Kujaribu kuwachimba mkwara wafanya biashara ni kujidanganya tu. Naamini kila mfanya biashara angetamani auze kwa bei mdogo kuliko wenzie ili amalize haraka mzigo wake, lakini hakuna mtu anaweza kufanya hivyo endapo bei haimlipi.

Hebu Wanasiasa waache usanii.
 
Tatizo hili jambo watu wameligeuza kuwa la kisiasa wakati ni la kitaalam zaidi.
 
v4N.jpg
 
Hakuna mwafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake viongozi wa afrika ni janga
 
Sio wote mkuu,lizards wengine wamejaribu mno kuyafanya hayo,maendeleo kwa raia na utawala bora,Mauritius,ushelisheli,Botswana,na sasa Ghana na Senegal!yes Africa we can na hii generations ya walalamishi wa social media watakapokuwa wameondoka ,next generation hasa vijana they will take Africa forward.
Hakuna mwafrika anaeweza mletea maendeleo mwafrika mwenzake viongozi wa afrika ni janga
 
Wafanyabiashara walibinywa pumbu sana awamu pendwa, sasa acheni wafidie kidogo.
 
Sio wote mkuu,lizards wengine wamejaribu mno kuyafanya hayo,maendeleo kwa raia na utawala bora,Mauritius,ushelisheli,Botswana,na sasa Ghana na Senegal!yes Africa we can na hii generations ya walalamishi wa social media watakapokuwa wameondoka ,next generation hasa vijana they will take Africa forward.
Ongezeko la maghorofa mijini sio maendeleo
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom