Hivi kuna kiongozi hapa Tz anaweza kukemea mlegezo?

funza

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
7,459
3,136
Huu uvaaji wa vijana wavulana kwa wasichana siku hizi umekuwa wa kusikitisha sana Viongozi wapo busy na mambo Yao huku jamii maadili yanazidi kubomoka uvaaji mlegezo sasa ni rasmi Pia vinguo vya kubana kwa akina mama navyo vinaelekea kubaya zaidi na Hakuna kiongozi atakayethubutu kulikemea hili janga linalovuruga maadili kwenye jamii
 
Siku ikitokea kiongozi akasimama hadharani na kukemea uvaaji Mlegezo hapa Tanzania Nina uhakika yatakuwa ni maajabu ya karne
 
Hili halihitaji viongozi kukemea...ni jukumu langu,na wewe kuhakikisha tunazua kama sio kufuta kabisa mmomonyoko wa maadili...kuna namna nyingi sana tunaweza kupambana na hili...mfano kupiga bhan uvaaje usiozingatia maadili kwenye public places! Kwenye dala dala n.k
 
Wenyewe wanavaa milegezo huoni wanavohangaika kupandisha suruwali wakiwa majukwaani
 
Kwani mlegezo ni dhambi?? Wakikua wataacha mi mwenyewe huo mlegezo ndo ulikuwa ugomvi wangu na walimu shuleni na mama nyumbani. lakini mwisho nimeacha mwenyewe tu..Ujana maji ya moto huwa unapoa
 
Z
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom