Hivi kuna kiongozi hapa Tz anaweza kukemea mlegezo?

we acha tu hizo siku si zilitabiliwa bado mengine zaidi ya hayo yanakuja.
 
suala hili sio la viongozi ni la jamii nzima, lakini hata kama lingekuwa nilao lazima uangalie viongozi wenyewe wanaongogwa na mfumo gani mpaka wakafikia hatua ya kukataza mfumo flani.
viongozi wa dunia hii karibia wote wanaongozwa na mfumo wa kumpoteza mwanadamu na kumtoa katika maadili na kutokumtambua MWENYEZI MUNGU, hivyo haitakuwa rahisi kiongozi kupinga mambo ya wakubwa wake, ndoo maana utasikia leo ushoga, kesho wanawake wawe na haki sawa na wanaume lakni pia jana walipanda na propaganda ya kutete haki za watoto, lakin hawakomei hapo watakuja na uongo wa kupiga vita ukimwi lakn mfumo unaotumika utashangaa, sasa jiulize inamaana haya yote hawa viongozi hawayaoni haya?
viongozi wetu hawashughuliki na mambo ya siyo ma maslahi na wao, wako busy kujilimikizia mali na kufanya wengine masikini, cha msingi sisi kama jamii inayoathirika tuchukue htua
 
Dawa sio viongozi bali ni sisi wenyewe huku mitaani tunapoishi ndio tuna dawa yao.Nakumbuka kuna siku moja asubuhi pale Ubungo Stand kuu ya Mabasi ya Mikoani kuna mdada mmoja alichofanyiwa na makonda na wapiga debe nadhani hatakaa arudie tena kuvaa ule utumbo wake aliouvaa,maana bila ya Polisi kuingilia kati na kumtoreshea kituoni kwao yule Mdada angekufa kwa mikono kuingizwa sehemu zake za siri bila kuchagua ni mbele au nyuma.
 
Ndugu yangu, mlegezo haukuanza leo, haya ni marudio, ngoja nikurudisheni nyuma wana JF wenzangu. Miaka ya sitini huko, nikiwa na umri wa miaka kama tisa hivi, nilikuta mtindo wa "Mchinjo" au "Dinglish" (wazee wenzangu watanisahihisha kama nimekosea matamshi)kwa akina kaka na Tight kwa akina dada, mitindo hiyo pamoja na kukemewa ikafuatiwa na mlegezo ambapo bado suruali ilikuwa ya kubana na kwa juu lilivaliwa shati kuuubwa likiitwa puto, akina dada wakaendelea na tight. Serikali ilipiga sana kelele hadi kufikia hatua ya kutumia chupa ya bia kuipitisha mapajani hadi miguuni, na isipopita basi suruali yako inapasuliwa hadharani. Hiyo ikaonekana kama dawa kidogo, ikafuatiwa na mtindo wa "Bell Bottom" au "pekoz" ambapo sasa suruali ilibana sana kuanzia kiunoni hadi magotini halafu inatawanyika chini kama kengere, upo hapo?

Mtindo huu pia ukapigwa vita, ndipo ikaja bugaloo mbayo ilivaliwa na jinsia zote na hiyo ni miaka ya sabini. Hayo yote yalipita sio kwa kelele za viongozi. Kwa kuwa nchi yetu haina vazi la taifa nadhani tuyaache ipo siku yatajifuta au kufutwa na mitindo mipya.
 
Back
Top Bottom