Hivi Kumpinga Kikwete ni Ufisadi? Simwelewi Mh.Kimaro au anasababu zaidi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Kumpinga Kikwete ni Ufisadi? Simwelewi Mh.Kimaro au anasababu zaidi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shadow, Apr 14, 2009.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Demokrasia imeweka wazi kwamba mtu anahaki ya kugombea au kuchaguliwa. Kugombea ndani ya CCM ni haki ya kila mwanachama kwa hiyo na katiba yao imeweka bayana. Let them leave democracy to take its root. Kwa nini waogope kama mgombea wao yupo makini? Pili, kama wanahuakika kwamba kuna rushwa etc kwa nini wasihusishe TAKUKURU? Mh. Kimaro et al please do not muzzle democracy for the sake of personality. Otherwise, badilini katiba iseme m/kiti hapingwi ieleweke.

  Take Note: watu wasije tumia kiini cha 'ufisadi' kuzuia watu makini kuchukua fomu kwa kuwahusisha na ufisadi. Naona wanaelekea kufanikiwa katika hili!( Iam in support of the democracy and rule of law and not ufisadi offcourse!!)

  Date: 4/13/2009
  Mbunge awashambulia mafisadi wa CCM wanaojiandaa kwa urais
  Ally Sonda, Moshi

  MBUNGE wa Jimbo la Vunjo(CCM) Aloyce Kimaro,amewataka mafisadi wanaojiandaa kumng'oa madarakani Rais Jakaya Kikwete na kundi la wabunge waliojitoa kafara kupinga ufisadi kuvunja mtandao wao mara moja kwa kuwa hautafanikiwa.

  Akizungumza kwa kujiamini na huku akishangiliwa na umati wa watu,Kimaro alisema mwaka ujao wa uchaguzi, Rais Kikwete atashinda kwa kura nyingi sanjari na wabunge mahiri wanaomsaidia kupambana na ufisadi wakiwa ndani na nje ya Bunge.

  Kimaro ambaye alikuwa akiwahutubi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kata ya Kahe Mashariki,alisema mafisadi wote wasiotaka Kikwete aendelee kuiongoza nchi kutokana na chuki za kuumbuliwa wataaibika zaidi mwaka ujao.

  "Hivi sasa tunajua kuwa wapo mafisadi wanajipanga kuhakikisha kuwa Rais na wabunge waliojitoa mhanga kufa kwa kupinga ufisadi nikiwemo mimi tunang'oka mwaka 2010. Nasema hivi, hang'oki mtu hapa,Kikwete ni Rais hadi 2015 na sisi wabunge tutashinda vilevile, Mungu yupo mbele yetu,"alisema Kimaro.

  Alisema bomu alilolilipua bungeni kuhusu uuzwaji wa nyumba za serikali ambalo limeanza kuleta mafanikio baada ya nyumba hizo kuanza kurejeshwa ni sehemu ndogo sana ya mikakati yake ya kupambana na mafisadi 'wanaoitafuna' nchi bila kunawa.

  Kimaro alisema ufisadi ndani ya Tanzania ni mkubwa na ndiyo sababu nchi inaendelea kuwa maskini na hivyo kujiendesha kwa kuombaomba misaada kutokana na watu wachache kuiba raslimali za taifa na kuzitorosha nje ya nchi.

  Akizungumzia watu wanaolimezea mate jimbo lake na hivyo kujipanga kuwania ubunge mwakani, Kimaro alisema hana tatizo na vyama vya upinzani ambavyo vimeanza kutangaza kusimamisha wagombea, bali ugomvi wake ni kwa wanaCCM walioanza kujitangazia ubunge wa jimbo hilo hivi sasa.

  Aliiomba CCM wilaya ya Moshi Vijijini, kuwaonya wanachama hao kwa madai kuwa wanaleta mgawanyiko ndani ya CCM, kitendo ambacho kinaweza kutumika vibaya na kambi ya upinzani kuwasambaratisha wanaCCM.

  "Mheshimiwa Mwenyekiti wa CCM, nakiomba Chama kiwaonye wanaCCM hawa wanaojitangazia ubunge wa Vunjo wakati wanajua kuwa mimi ndiye Mbunge halali wa Vunjo,nakuomba sana waonye la sivyo wataona cha mtema kuni,"alisema Kimaro bila kufafanua.

  Katika mkutano huo, uliohudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi,ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ya wilaya hiyo,Alhaji Musa Samizi,Mwenyekiti wa CCM,Gabriel Masenga aliwataka wanaCCM wote wanaotaka ubunge wa Moshi Vijijini na Vunjo wasubiri muda muafaka ufike.

  "Napenda kuwaomba wanaCCM wote wanaotaka Ubunge kwenye majimbo yetu mawili(Moshi Vijijini na Vunjo) wawe watulivu muda muafaka ufike,tutawapa fomu,tutawachuja kwa kura kama anafaa,kujipitishapitisha hivi sasa ni kuleta vurugu ndani ya Chama na Jumuiya zake"alisema Masenga.

  Masenga alitumia mkutano huo kuwataka baadhi ya wanachama wanaokikashifu Chama na viongozi wake baada ya kuadhibiwa kwa mujibu wa Katiba na hivyo kutishia kukihama CCM , waondoke mara moja na kujiunga upinzani kwa madai kuwa kuendelea kwao kuwa CCM ni sawa na kukumbatia Bomu.

  "Wapo baadhi ya wanaCCM wameadhibiwa kwa kukiuka katiba ya Chama,sasa wana hasira wamekuwa wakikashifu Chama na baadhi ya viongozi,sasa kwa niaba ya Chama nawaomba waondoke CCM,huenda wakijiunga na vyama vya upinzani watafanya kazi yao vizuri ya kupambana na CCM,"alisema Masenga kwa kujiamini.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 14, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Anatafuta kula, unajua ukishakuwa mtumwa wa tumbo, unaweza fanya lolote lile, leo JK akimwambia nipe mtoto wako bure anatoa, achilia mbali mke! mwanaume na akili zako huwezi ukasimama n kuongea utumbo kama huo, lakini ukishakuwa mtumwa wa tumbo, lolote laweza kutokea ..... hapa kasema je huoni kuwa katika matendo yake yuko radhi kuua mtu!
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  jamaa kapoteza sana mwelekeooo...wana vunjo poleni kwa kuwa na mwakilishi wa aina hiyooo.

  hivi kuna anayeweza kuthibitisha kuwa JK na mafisadi hawana ugomvi wowote ni suala la muda tuuu wanangojea term ijayo watese upya na kuonyesha kuwa mtandao umefikia lengo la kuongoza kwa vipindi viwili kwa mikakati ileeeeeeeeeeeeeeeeeeee....
   
 4. T

  Tujisenti JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Labda haelewe maana ya "ufisadi"
   
 5. k

  kela72 Senior Member

  #5
  Apr 14, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee anadalili nyingi za "kuchanganyikiwa", unajua anajikomba kwa JK kwasababu anajua alimuumbua Mkapa bungeni, mtu ambae alikuwa mwenyekiti wake alipokuwa anatafuta ubunge, sasa anajua bado Ben ananguvu kwenye siasa za CCM..... na anahofu watu wake (Ben) watammwaga mwaka 2010. Sasa kimbilio lake pekee ni kujigonga kwa JK kwani anahisi JK anafurahia sana Ben kushambuliwa....
  Lakini huyu ni mnafiki tu, hivi kweli unaweza kuupiga vita ufisadi wa akina Rosatam huku ukmtaka JK aendelee kukaa madarakani!? Angalia jinsi JK anvyosaidia/kaa kimya jinsi mafisadi wanavyo washughulikia watu wanaowapinga....! Hivi kweli kwa mfano rais awe Magufuli kweli Rostam na mafisadi wengine wataweza kutukana watu wanaowapinga kwa kutumia vyombo vyao vya habari? kweli Rais makini atakaa kimya tu?
  Ni kweli anatafuta kuchumia tumbo tu, hana lolote! hakuna ufisadi utaopigwa vita ya kweli ndani ya "oungo-zii" wa mkulu huyu kwani nae ni zao la mafisadi.
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Ndiyo matatizo ya kubwabwaja maana mara nyingi unayoyabwabwaja hayaingii akilini hata kidogo.
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hawa wabunge wa CCM wanaojidai wanapinga ufisadi, hoja iliyoibuliuwa na wapinzani; ni watu hatari sana katika vita ya kuikomboa nchi yetu kwani hawajui marafiki wa mafisadi na nani maadui wa kweli wa mafisadi!! Ni jambo la kushangaza hawa jamaa kumuweka Jakaya katika kundi la wachukia mafisadi huku wakijua wazi kuwa mtu anaewalinda KAGODA, MEREMETA,DEEP GREEN etc ,is none other than JAKAYA MRISHO KIKWETE; halafu leo nyie wenyewe mnadhani muungwana yuko upande wenu nadhani kwa hakika Kimaro wa Vunjo na wenzake hawamuelewi muungwana; huyu bwana is closer to Lowassa na Rostam than you can care to believe!! Nyie ngojeni tu kama hamuamini kuwa hayuko nanyi mpaka hapo atakapowaliza ndio mtamjua kuwa muungwana ni mkwere wa Msoga na Subash Patel ni kaka yake!!
   
 8. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  MKU BUBU, hiyo ndiyo CCM uliyokuwa na matumainio nayo na ile ile tulokuwa tukikueleza kuwa kumpata mpiganaji wa kweli humo ni sawa na hakuna kabisa.
  Vita vyao ni wale wanaokanyagana basi lakini kichama soji ni hilo hilo. Na Tumsubiri shujaa Mwakyembe ifike zamu yake kula kiapo cha utii kwa JK.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Apr 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,886
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Chama chenye wanachama millioni 4 kamwe hakiwezi kukosa mtendaji mzuri zaidi ya Kikwete na ambaye hajatiwa mifukoni na mafisadi.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,622
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio kumpata bora zaidi ya Kikwete from within, bali huyo safi atayeweza kuhimili mikiki kuchupa toka chini mpaka juu bila ya kupanda ngazi inayomilikiwa na wenye nazo.

  Sio issue ya wanaCCM milioni nne, ni chama chenyewe ndio kimejiweka rehani kwa wenye nazo. Ile 2000, JK was not the best option lakini kilichofanyika kinajulikana, nani alikemea zaidi ya kumwaga pongezi?.

  CCM ina bado ina watu safi na wenye uwezo kuliko JK lakini wataanzia wapi kujikwamua toka kwenye lindi la uchafu, si nao watachafuka tuu au watachafuliwa?.

  Pamoja na udhaifu wote wa serikali ya JK, 2010 bado ni yeye tuu kwa sababu mpaka sasa hakuna dalili ya mbadala yoyote sio ndani wala nje. CCM chafu, upinzani hamna kitu, bora kuendelea na zimwi likujualo..
   
 11. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2009
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  JK alitakiwa kuacha kazi tangu EPA ilipogundululika sababu kisheria Jakaya ni illegitimate president sababu ameingia pale with fraud money. End of the story, hakuna sijui anapinga ufisadi, sijui anafanya nini. The guy is criminal and fraud, so why bother to argue that he need to run for 2010?

  Jakaya and his buddies need to stand before judge and explain about the EPA money. I think all this noise kuhusu Jakaya anapinga ufisadi is total nonsense, how can you fight against Ufisadi wakati you took a position due to UFisadi. So, does it make sense? Jakaya need to be on top of the list, end of the story.
   
Loading...