minda
JF-Expert Member
- Oct 2, 2009
- 1,068
- 67
hivi karibuni nilitembelea wilaya ya mpwapwa na katika kijiji kimoja mwanafunzi mmoja wa kike aliyemaliza kidato cha 4 mwaka jana katika shule ya kata ya kata hiyo mpya iliyoanzishwa hivi karibuni alishiriki kwenye kinyang'anyiro cha udiwani viti maalumu kupitia chadema na almanusrat aukwae udiwani. hata hivyo iligundulika kwamba huyo 'denti mstaafu' hakuwa na kitambulisho cha mpiga kura na hakushiriki kwenye zoezi hilo.
hivyo nikaamua kumuuliza ni kwa nini licha ya kushiriki kama mgombea kupitia chadema lakini hakushiriki zoezi muhimu la uchaguzi?
akaishia kuniambia,"nilikuwa nambwelambwela tu"
hivi wakuu, nini maana ya neno hilo kwa kiswahili fasaha? ashakhum si matusi mtaniwia radhi kama neno lenyewe ni tusi kwani lengo langu hasa ni kujifunza.