Hivi kumbe mapenzi ndo yanauma hivi!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
17,664
2,000
Wiki iliyoisha tu kuna msela wangu kaachwa akawa analalamika mpak kulia! Kiberenge wa watu ndo kwanza sielewi nikawa namcheka naona huyu nae anajitafutia visa tu!

Yalayalayala!! Kumbe jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza na hata yule muhenga aliesema "usiombe yakakukuta" yaonyesha yalimkuta makubwa!.. wiki hii ikawa yangu kiberenge wa watu sina hata raha huku sio kutoswa ni kuteseka sasa! Nimeamka asubuhi hata sijakaa sawa nikaona sms yake ati "SIKUTAKI TENA!" nikajua mbwembwe zake tu kumpigia si akapokea jamaa linaniambia "Mkuu mpaka umeseviwa BATA bado unatafuta nini kwa huyu mwanamke!!" Simu ikakatwa hapohapo nikapatwa na kiu mixer mkojo kwa wakati mmoja!.

Baadae kupiga tena akapokea Sasa kitesa roho wangu! Nikaanza mlaumu na kulalamika jibu nililojibiwa ni "Bwana ee tafuta wa kumpa hayo mapenzi yako ya kibatabata!" Simu ikakatwa kupiga tena nakuta nishachezeshwa buloku pande zote.. haikutosha nikaamua nimfate ana kwa ana si nikakutananae aniambie hata sababu ya kuniacha,nilichoambulia nilichekwa halafu akaondoka ila kwa mbali nikasikia neno kama akisema "nimekuacha na uwabata wako" anyway sikusikia vizuri ila nikaona isiwe tabu nami nivunge nisimtafute!

Sasa tabu ipo hapo kwenye kuvunga! Jamani mapenzi yanauma nyie yani maumivu nayoyasikia sijui hata yanatokea wapi ila nachosikia yani mgongo unakuwa wamotooooo halafu Kama unafinywafinywa! Kichwa kimeshaparanganyika hapa nimejikuta nalia huku nimesimama lakini machozi yanaelekea masikioni!!

Mapenzi si kitu cha mchezo jamani😪

1625741268485.png
 

Amazing H

Member
Jun 22, 2021
50
150
USHAURI

1. Chukua siku tatu bila kumtext wala kumfatilia au kumtafta mahara popote

2. Kama huna mtu yeyote wa kuwasiliana nae, weka simu mbali usijishughulishe na lolote kwenye simu hata games usicheze, hii itakusaidi kukwepa kumtumia text

3. Pendeza, acha kuvaa yale mavazi uliokuwa ukivaa pindi uko nae, jibadilishe kabisa,jipende aswa kama unauwezo wa kununua viwalo nunua, tupia upendeze

4. Badili muonekano wa chumba na achia kutembelea sehem mlizozoe kukutana

5. Sali sana, Mungu anakupenda muombe atakupa mpenzi mwingine

6. Amini kila kinachotokea kina 7bu zake asa kukukuza/kukufunza, yanakutokea sababu hayajawai kukutokea na mshukuru Mungu kwamba yametokea, je, vp angekuficha?!

7. Kubali ukweli hata kama ni utani/uwongo

8. Fikiria ni mwanamke wa aina gani ungependa awe mke wako asa kitabia

9. Spend time na washikaji na panga mipango yako kila hasubui na mambo yote yatimize kwa namna ulivo yapanga

10. Epuka kuwaza visasi, vitakupa majuto na kukuongezea majonzi kuliko uliyo nayo sasa hivi

11. Anza kuishi mwenyewe, acha kufikiria kumpata mwingine

12. Kama unamachungu na utokwa machozi , nenda sehemu ambayo unatakiwa uwe pekee yako nakushauri anza kumfikiria na lia kabisa lia ata ukimaliza masaa matatu unamwaga machozi, acha machozi yatiririke itakusaidia kupunguza machungu na usione haja tena ya kumlilia

13. Amini KARMA ipo itamlipa naye ipo siku itamtokea cha msingi ongeza juhudi na bidii katika shughuli zako, waza mapene waza vitu vikubwa, nyumba, magari nk kwa ujumla waza ndoto zako

MUACHE AENDE ZAKE!!

Huo ndio ushauri wangu utaniletea mrejesho
Keep to be UWABATA chama la wana hiyooooo!!
maxresdefault(1).jpg
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
17,664
2,000
USHAURI

1. Chukua siku tatu bila kumtext wala kumfatilia au kumtafta mahara popote

2. Kama huna mtu yeyote wa kuwasiliana nae, weka simu mbali usijishughulishe na lolote kwenye simu hata games usicheze, hii itakusaidi kukwepa kumtumia text

3. Pendeza, acha kuvaa yale mavazi uliokuwa ukivaa pindi uko nae, jibadilishe kabisa,jipende aswa kama unauwezo wa kununua viwalo nunua, tupia
Nitapita kweli! Ngoja nicheki..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom