Hivi kukitokea utata wa jambo, wananchi tunatakiwa kuwahoji Rais na Mawaziri au Wabunge?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,544
2,000
Ni utaratibu uliozoeleka kwa jambo lolote likitokea wananchi kuomba ufafanuzi kwa mawaziri, au wakimlilia Rais. Lakini kwa utaratibu wa siasa za uwakilishi si ilitakiwa tuwapigie kelele wabunge na mkubwa wao Spika.

Mfano bei ya mafuta ya kula ikipanda, Tozo ikiongezeka, mkataba wa gesi usioeleweka, majibu ya mambo hayo si tunapaswa kuwapigia kelele wabunge na spika watupe majibu badala ya kumtupia lawama mtu kama Mwigulu nk?

Pengine tukiwapigia kelele watakuwa macho kutuwakilisha matakwa yetu serikalini. Tukiupigia kelele uongozi si wao watabweteka na kushindwa kufanya kazi yao wakijua hayawahusu?

Eti limekaaje hili?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom