Hivi kitu gani kinamfanya mwanamke kumnyanyasa mwanaume kimwili, kifikra na kisaikolojia?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Nilikuwa nasoma jarida moja mitandaoni imeonekana miaka ya hivi karibuni wanawake wengi wamekuwa wakiwanyanyasa wanaume kimwili, kifikra na kisaikolojia.

Kwa wale wasiofahamu, ukisikia mwanaume ananyanyaswa na mwanamke wake kimwili, kifikra na kisaikolojia ujue hapo tunazungumzia mwanaume kunyimwa tendo la ndoa, mwanaume kusimangwa na mwanamke wake, mwanaume kila saa kutukanwa, mwanaume kufanyiwa vitibwi vya kila aina na mengineyo

Je, ni kwanini wanawake wanawafanyia hivi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ww unayenyanyaswa ungetoa ushahidi kabisa, au unaogopa mkeo asijeona mwandiko wako ngumi zikaendelea ?
 
Uongo mtupu. Wanaume wengi huwa wanapenda kwa macho tuu na wanawake wanapenda toka moyoni.

Ndio maana ukimtenda mwanamke anaumia zaidi ya mwanaume kutendwa.

Sasa from there you can tell nani atateseka kisaikolojia zaidi.

Hiyo research yako haina ukweli hata chembe.
 
Uongo mtupu. Wanaume wengi huwa wanapenda kwa macho tuu na wanawake wanapenda toka moyoni.

Ndio maana ukimtenda mwanamke anaumia zaidi ya mwanaume kutendwa.

Sasa from there you can tell nani atateseka kisaikolojia zaidi.

Hiyo research yako haina ukweli hata chembe.
Haha mwanaume akitendwa haumii? Nani kasema
 
Aaaaa subutu..... Mwanamke aninyanyase Dah labda wanaume wezangu ndo wanafanyiwa hivyo.... Khaaaa.!!!!! Yani huo ni upumbavu kabisaaaaaaaaa..... Mm ndo huwa nawatesa tu......
 
kwa wale wasiofahamu ukisikia mwanaume ananyanyaswa na mwanamke wake kimwili,kifikra na kisaikolojia ujue hapo tunazungumzia mwanaume kunyimwa tendo la ndoa, mwanaume kusimangwa na mwanamke wake, mwanaume kila saa kutukanwa, mwanaume kufanyiwa vitibwi vya kila aina
na mengineyo
Wacha niwe "The Devil's advocate"
Wanawake tukipenda, tunapenda haswaaa; Kushoto - Kulia, Kaskazini - Mashariki. Na tutavumilia na kuheshimu waume zetu sana, sana, sana!
Tatizo linakuja pale uvimilivu unapofika mwisho --->Penzi nalo litapungua. Na table ziki turn tu i.e. mwanaume akashikwa pabaya, either alifanya kosa au kipato kimeshuka; hapo ndio mwanaume ataimba na kucheza wimbo wa Taifa.
Ila tukipenda, Walahi tunapenda!!
# When A Woman Loves- R.Kelly 😉
 
Sio wanawake wote,ila wengi wapo hivyo,na kinachowaharibu ni marafiki,unakuta mwanamke yuko kwenye ndoa lakini kijiwe chake kikubwa ni Salon,ikukmbukwe kuwa wanawake wanapokutana kule Salon wanapeana ushauri mbovu sana,kila mmoja anajaribu kuonyesha alivyo mbabe kwa mwanaume na jinsi gani anavyoweza kumuendesha mwanaume,sasa asie na akili anabeba na kuyapeleka nyumbani kwake,ikumbukwe kama umeolewa ni bora zaidi kuwa na marafiki wanandoa,lakini unakuta mwanandoa na marafiki zake ni wanawake walioachika kwenye ndoa,waliozalishwa na kuachwa,waliotendwa na wanaume kwa visa mbalimbali,sasa hapa usitegemee atapata kitu cha maana zaidi ya kubeba ule uovu na hasira walizo nazo hao watendwa na kuzipeleka nyumbani,ambapo mwisho wa siku ni masimango kwa mwanaume,hayo yapo ila wanaume wengi hawayasemi kwa kuona aibu...
 
Mwanamke aninyanyase? Hawa viumbe sijawahi kuwaza kuwekeza moyo wangu hata kwa 10%, nimetengeneza gap kubwa mno la furaha inayotokana na mwanamke.
 
When a woman fedup by R Kelly
Wacha niwe "The Devil's advocate"
Wanawake tukipenda, tunapenda haswaaa; Kushoto - Kulia, Kaskazini - Mashariki. Na tutavumilia na kuheshimu waume zetu sana, sana, sana!
Tatizo linakuja pale uvimilivu unapofika mwisho --->Penzi nalo litapungua. Na table ziki turn tu i.e. mwanaume akashikwa pabaya, either alifanya kosa au kipato kimeshuka; hapo ndio mwanaume ataimba na kucheza wimbo wa Taifa.
Ila tukipenda, Walahi tunapenda!!
# When A Woman Loves- R.Kelly 😉
 
kimtazamo naona kama wanaume wengi wamesahau majukumu yao muhimu yakuhudumia familia kiasi ambacho wanawake wanafanya hayo majukumu ndo mana wanatokwa na imani na kuanza kunyanyasa wanaume

Na hili Mungu aliliona mapema ndo mana hakutaka kugawa madaraka kwa mwanamke kwani alijua kama ni kiumbe ambacho hakina subra pindi anapokuwa aidha na m ali, fedha. cheo na viyu kama hivyo

Wahenga walisema filisika ujue tabia ya mkeo na unadhihirishwa na huu uzi
 
Hayo ndo maisha halisi ya wanaume ndani ya jamii pana sio hawa waliojificha kwenye keyboards wakijitapa na kuonyesha umwamba
 
Mkuu kumbe ulishamaliza kazi??
Na huu ndio ukweli ukiukataa tegemea maumivu na magonjwa ya moyo.
 
Back
Top Bottom