Hivi kitendo cha ndege kutoka mbali kuchukua majeruhi ambao Rais wao hawajui, imekaaje hii?

Nkobe

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
2,204
3,277
Wadau najaribu kufikiria, kitendo cha ndege kutoka huko mbali duniani na kuwachukua majeruhi wa Lucky Vicent ambao Rais wao aliishia kuwaona kwenye TV, kimekaaje? Yaani Rais wao aliishia kutoa pole kwa Twitter, hakuwahi kuwaona lakini Raia wa mbali wamewaona na kuwapa msaada.

Kibaya zaidi wametumia rambiramb kwa tukio la kuaga miili na kuwaacha watoto wamelala Mount Meru ambayo haina vifaa tiba vya kutosha
 
Muwakilishi wa Rais , Makamu wa Rais aliwaona...

Acha kujitoa ufahamu,majanga hayana muwakilishi,anayehudhuria kwenye misiba na matukio yote ya kutisha na kuhudhunisha anakuwa ameenda yeye kama yeye,kusema kuwa amemuwakilisha fulani ni uswahili tu.

Kama vile tumbo lisivyo na muwakilishi,ndivyo mguso na mwitiko wa mtu katika matukio ya kuhudhunisha usivyoweza kuwakilishwa,Ulishawahi kusikia mtu amekula kwa niaba yako kisha wewe ukashiba?Anayelia msibani kilio chake ni kielelezo cha namna alivyoguswa na msiba husika,kamwe huwezi kusema mtu aliyae msibani analia kwa niaba ya mtu mwingine,analia kutokana na "emotional intelligence" yake.

Kukaa kimya ni dalili za kutoguswa na matatizo ya wenzako,kiongozi wetu katika masuala ya kufariji wafiwa "amepungukiwa na utukufu" hawezi kujishusha na kunyenyekea yeye anataka aabudiwe tu,ukimgusa atakuambia ajali iliyochukua Maisha ya hao watoto haikuletwa na serikali yake na wala haipo kwenye ilani ya chama chake!
 
Nimekuelewa kwakweli
 
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
Kila siku tunaambiwa na kunajigamba kwamba China ndio Marafiki zetu lakini tumeona jinsi wamarekani wanavyoguswa na matatizo yetu kama Malaria,Ukimwi, kifua kikuu, umeme wa REA ,Barabara na juzi tumeshuhudia wakitoa ndege Marekani kuja kuwapeleka watoto wetu wanane wakatibiwe Marekani.
Hata hivyo Tanzania ni Taifa la watu wasio na shukrani.
 
Wadau najaribu kufikiria, kitendo cha ndege kutoka huko mbali duniani na kuwachukua majeruhi wa Lucky Vicent ambao Rais wao aliishia kuwaona kwenye TV, kimekaaje? Yaani Rais wao aliishia kutoa pole kwa Twitter, hakuwahi kuwaona lakini Raia wa mbali wamewaona na kuwapa msaada
bado mnatafuta likes kwa msiba? So so sad... subirini utokee mwingine bas pls
 
Kaka ukianza kufikiri juu ya watawala wetu kwa undani unaweza kukana uraia wako
, acha ibaki hivyo hivyo puzia usife mapema mkuu
Wadau najaribu kufikiria, kitendo cha ndege kutoka huko mbali duniani na kuwachukua majeruhi wa Lucky Vicent ambao Rais wao aliishia kuwaona kwenye TV, kimekaaje? Yaani Rais wao aliishia kutoa pole kwa Twitter, hakuwahi kuwaona lakini Raia wa mbali wamewaona na kuwapa msaada
 
Hakuna ndege yeyote inaweza kutua popote Tanzania bila ruhusa ya serikali kwahiyo mkuu anataarifa hizo.
 
Acha kujitoa ufahamu,majanga hayana muwakilishi,anayehudhuria kwenye misiba na matukio yote ya kutisha na kuhudhunisha anakuwa ameenda yeye kama yeye,kusema kuwa amemuwakilisha fulani ni uswahili tu.

Kama vile tumbo lisivyo na muwakilishi,ndivyo mguso na mwitiko wa mtu katika matukio ya kuhudhunisha usivyoweza kuwakilishwa,Ulishawahi kusikia mtu amekula kwa niaba yako kisha wewe ukashiba?Anayelia msibani kilio chake ni kielelezo cha namna alivyoguswa na msiba husika,kamwe huwezi kusema mtu aliyae msibani analia kwa niaba ya mtu mwingine,analia kutokana na "emotional intelligence" yake.

Kukaa kimya ni dalili za kutoguswa na matatizo ya wenzako,kiongozi wetu katika masuala ya kufariji wafiwa "amepungukiwa na utukufu" hawezi kujishusha na kunyenyekea yeye anataka aabudiwe tu,ukimgusa atakuambia ajali iliyochukua Maisha ya hao watoto haikuletwa na serikali yake na wala haipo kwenye ilani ya chama chake!
Mfano wako unaaply kwa mtu binafsi rais ni taasisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom