Hivi kipindi cha mada moto nacho kimepigwa BAN kama gazeti la Mawio?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Televisheni ya channel 10 miezi ya karibuni ilianzisha kipindi ilichokuwa ikikiita mada moto ambacho kilikuwa kikirushwa hewani LIVE kila siku za Jamatatu, Jumatano na Ijumaa kuanzia saa 4 usiku.

Kipindi hicho ambacho Mwendeshaji wake alikuwa Albert Kilala, alikuwa akichagua mada moto inayojadiliwa sana ndani ya jamii na kumuita mshiriki ambaye anaona anaweza akaiongelea na kuifafanua vyema mada hiyo kwa jamii ya watanzania.

Katika kipindi kifupi tokea kipindi hicho kianzishwe, tayari kilshajizolea umaarufu mkubwa, ambapo watu wengi wengi walikuwa hawabanduki kwenye luninga zao katika muda huo husika ili kukiangalia.

Mwendeshaji wa kipindi hicho alikuwa pia akitoa fursa kwa watazamaji kuuliza maswali mbalimbali kwa yule mgeni anayealikwa kwenye kipindi hicho.

Mimi mwenyewe nilikuwa mshabiki mkubwa mno wa kipindi hicho, na nilikuwa si-tune TV station nyingine yeyote unapofika muda wa kurushwa hewani kipindi hicho.

Hata hivyo mara ya mwisho kabisa wa kituo hicho kurusha kipindi hicho ilikuwa tarehe 8/01/2016 ambapo ilimualika Mwanasheria nguli wa chama cha Chadema, Tundu Lissu.

Sasa kwa kuwa katika kurushwa kwa kipindi hicho na kituo hicho, kuonekana kukosoa 'madudu' mbalimbali yanayofanywa na watawala, inaonekana kipindi hicho kilikuwa hakiwapendezeshi sana watawala.

Miongoni mwa mada moto kabisa zilizokuwa zikijadiliwa mara kwa mara na kipindi hicho kwenye kituo hicho cha luninga ilikuwa ni kuhusu mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar, kutokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliofanyika tarehe 25/10/2015 kulikofanywa na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha.

Sasa kwa kuwa kipindi hicho tayari kilishajizolea mashabiki wengi sana, kitendo cha kukisitisisha kipindi bila kutajwa sababu zake, kimewasikisha sana wapenzi wa kipindi hicho.

Ndiyo maana zinaanza kuibuka hisia miongoni mwetu kuwa, kutokana na kusikia kuwa sababu zilizopelekea kupigwa LIFE BAN gazeti la Mawio, ni kutokana na kukomalia kwake kuandika makala nyingi zinazohusu mkwamo wa kisiasa huko Zanzibar, isije basi ikawa kituo cha channel 10 nacho kikawa kilipigwa 'mkwara' mzito na watawala wa kusitisha mara moja matangazo ya kipindi hicho.

Kama hisia zetu hizo mashabiki wa kipindi cha mada moto zitakuwa siyo sahihi, basi tunamwomba mwendeshaji wa kipindi hicho Albert Kilala ajitokeze hadharani na atueleze sababu zilizofanya atunyime 'uhondo' mashabiki wake, kwa kusitisha ghafla kipindi hicho tulichokuwa tunakipenda sana tena saaaaaaana..............................
 
Hakuna uhuru wa habari kama unakosoa serikali tawala, naomba uelewe hivyo.
 
Back
Top Bottom