Hivi Kinana na Polepole ninyi ni wafiwa au Waombolezaji?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,338
4,672
Msiniulize maswali tena.Na wala msinione ni mchokonozi au najikuna au kimbelembele.Tuko msibani.Msiba mzito wa Kitaifa.Ndugu yetu tuliyekuwa tunamtumainia sana "Makainikia" tuliyekuwa hatujui yuko wapi muda mrefu sana kwa takribani miaka 30 hatimaye tumetangaziwa na "Mzee wetu wa Kaya" kuwa kumbe "alinyomgwa".Na kisha wauaji hao wakampasua na kumuwekea tumboni mawe ya thamani na kumpeleka ughaibuni kusikojulikana bado.Mzee amesema kilichopelekea kujulisha wachunguzi wa alikokuwa ndugu yetu ni "mkono wake" mmoja kuonekana ukielea maeneo ya Feri "bandarini".

Ni msiba mzito sana! Inatia simanzi na inauma sana.Baba yetu wa familia (Mzee Magufuli) "Amelia" sana Jana wakati akitutangazia familia juu ya msiba huu mzito tena wa kitesaji na wa kinyama.

Kila mwanafamilia analia kivyake.Mzee Mapesa Amelia kivyake.Mzee Butiki yeye amelia "Kimwitongo". Nami wa Kaskazini kule Kilalacha,Mrema nalia kivyangu.Nalia kwa kwikwi kubwa na nimechanganya na Kikerewe.Nalia hadi "lisinjagongwe" limenikaba.

Kwa hiyo msiniulize kwa nini nawauliza: hivi ninyi wenzetu wanafamilia ni wafiwa au mumegeuka kuwa waombolezaji? Hivi ninyi ni kampuni ya mazishi tu mnasubiria mupewe taratibu za wapi matanga ya Huyo ndugu yetu "Makanikia" yatafanyika?

Kinana na Polepole hatujawaelewa kabisa! "Baba" wa familia kasema baadhi ya watu walioshirikiana na wale "wauaji" wa ndugu yetu makanikia ni rafiki zenu sana.Na sio siri tena kila mwanafamilia anajua hao jamaa akina Team Chenge huwa munakaa nao kwenye "biashara zenu" za kichama.Tunafahamu kuwa wewe Kaka Kinana na Polepole ni viongozi wa juu wa hao jamaa katika Klabu yenu iitwayo CCM.

Hivi mbona hatuoni mkimwaga hata chozi na wala hamjatoa kauli yoyote ile mintarafu uanachama wao katika Klabu yenu "pendwa" CCM utakuwaje?

Kwa nini mumekaa kama mumepigwa ganzi hivi na kama miguu,mikono,Mdomo,masikio,pua,ulimi,macho na Ubongo vyote vimepooza?

Nawauliza.Hii ndiyo staili yenu ya kumlilia ndugu yetu "Makanikia"? Sasa tuhitimishe kwamba ninyi mko upande wa waombolezaji au wafiwa? Hivi haiwezekani mukakutanika kwa ghafla na kuazimia "ku-paralyze" uanachama wa hao wanachama wenzenu wakati wanafamilia tunasubiria kazi ya kuwapekua imalizike?
 
Picha zao hizi hapa.

.
6bc361c4b87c1acad6ac56eb773b1d03.jpg


9af4993ba62fe1d197a6536ded056fc3.jpg
 
Back
Top Bottom