Hivi kina dada mnapofiwa na wakwe zenu huwa mnahuzunika kweli?

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Dec 27, 2019
2,919
15,604
Wadau ni wazi kuwa katika maisha yetu ya kisasa, kina dada wengi huwa wanawachukia wakwe zao wa kike na wifi zao, hasa pale Mama wa Mume anapoona kachoka na hivyo angehitaji kuishi kwa mwanawe wa kiume ili kupata matunzo na uangalizi wa karibu lakini pia kufurahia matunda ya jasho lake katika kumlea mtoto wake wa kiume.

Itokeapo hilo, basi migogoro, mikwaruzano na bifu babu kubwa hutokea kati ya Mke na Mama mkwe. Kwa bifu zile zilivyo, hivi inapotokea wifi au Mama mkwe kufariki nyie kina dada huwa kweli mnahuzunika kwa misiba hiyo, au huwa mnaigiza tu kuhuzunika wakati moyoni moyoni mwasema bora hivyo?
 
Haya Mambo bhana huwezi kuyatolea jibu la moja kwa moja, moyo wa mtu ni kichaka,

Wiki 2 zilizopita ulitokea msiba wa Bibi mmoja huko kijijini, enzi za uhai wake alikuwa nae mke mwenzie hawakuwa na maelewano hata kidogo, lakini ajabu mke mwenzie alilia na kuhuzunika mpaka kupandisha presha, kila mtu alikuwa akimshangaa huyo bimdogo
 
Mkwe wako ni sawa na mzazi wako, machungu ya kufiwa hayatofautiani

Kuna wanawake wana uadui na wakwe zao lakini jamani not at that level ya kufurahia msiba wa mzazi wa mumeo

Ila pia wadada na sisi ni wakwe wa baadae, tunavyowatreat wakwe zetu we will get the same treatment from our daughters in law, tuwe wema tunapoingia kwenye familia za watu
 
Ule ni unafiq tu, Ukishawajua wala hayo mambo hayakusumbui kwa sababu yapo kila siku, Unashangaa mtu hata hajawai kukaa na mwendazake hata kwa siku chache tu hawana ile bond ya familia lakini mtu akitwaliwa unaona watu baki wanalia huku akilia kwa kujibaraguza, Lakini ukweli ambao watu hawaukubali ni kwamba ule ni unafiq tupu, Watu waliofiwa kweli hawana muda wa kuelezea jinsi ambavyo wameumizwa na mpendwa wao.
 
Haya Mambo bhana huwezi kuyatolea jibu la moja kwa moja, moyo wa mtu ni kichaka,

Wiki 2 zilizopita ulitokea msiba wa Bibi mmoja huko kijijini, enzi za uhai wake alikuwa nae mke mwenzie hawakuwa na maelewano hata kidogo, lakini ajabu mke mwenzie alilia na kuhuzunika mpaka kupandisha presha, kila mtu alikuwa akimshangaa huyo bimdogo
Analia atakosa wa kutokuelewana nae.

Maisha yalivyo Kila mtu Ana umuhimu wake na huwezi kuuona umuhimu wa mtu Hadi aondoke kwenye maisha yako
 
Kwakweli inategemea
Nisiwe mnafki
Mma mkwe wengine adi wanaroga wake za watoto wao
Akifa hulii wala nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom