hivi kila mfanyabiashara/mjarimali lazima aende kwa mtaalamu/mganga wa ndumba?

x - mas

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
800
500
Amani iwe nanyi wapendwa,kume kuwa na kasumba ya wafanyabiashara wengi kuhusisha biashara zao na imani za kichawi ikiaminika watapata wateja wengi au kuzuia biashara zao zisipigwe ndumba.Binafsi naona watu hao ni wajinga yaani hawana maarifa sahihi ya biashara,nashindwa kuamini mtu ambaye na muamini mwenye busara zake tunamtegea kwa mawazo mazuri amenishauri ni waone mawichdokta ili niweze kufanikiwa,inakuaje watu wanaihusudu sana hii kitu?kazi kwelikweli...
 

Kubota

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
532
1,000
Hii dunia ni very complicated linapokuja suala la Imani! Kwa wanaoamini kuwa pesa huja au hongezeka kwa ngekewa, au bahati, au kuwa na nyota nzuri au wale wanaodhani wateja huvutwa na majini ni lazima watatafuta wataalamu wa ndumba! Hapo tena ukute na huyo mjasilia mali au mfanyabiashara maisha yake yameinamia kwenye kuamini kuwa hao wataalamu wa ndumba ndiyo wanamajibu ya maswali yote ya hapa duniani!

Amini amini nakuambia biashara inafanywa popote duniani na lugha iko moja tu! Siri kubwa ya kufanikiwa inatoka kichwani kwa mhusika! Kufanikiwa kwenye biashara kunahitaji akili ichangamke na wala si kweli kwamba kila mtu anaweza kufanikiwa kwenye biashara hasa zenye ushindani! Mtu anawezamaliza waganga wote kama hajui kwamba biashara ni sayansi na maarifa ya kisayansi ambayo unaweza kujifunza toka kwa waliofanikiwa! Hata uchanjwe chale hadi makalioni iwapo hujui kwamba mteja ni mfalme, hujui siri ya kumshawishi huyu mfalme aje kuchukua mzigo kwako, kwa wakati na kwa ubora anaotaka wewe utaishia kuwaneemesha tu hao waganga! Kuna mambo mengi sana ya kujifunza ili kufanikiwa kwenye biashara lakini watu wanafikiri watazipata mbinu hizo kwenye hayo matunguli na kufukua gagulo makaburini! Watu wasome vitabu, waombe ushauri kwa waliofanikiwa, wahudhurie mafunzo na semina zinazohusu ujasilia mali hata kama ni kwa kulipia. Bahati mbaya sana wale wanaoamini uganguzi pekee watabaki kusingizia watu wengine kuwa ndiyo wamesababisha wasifanikiwe!

Watu hawajui mahesabu ya kujua faida na hasara, hawatunzi vizuri kumbukumbu za mauzo, hawana mbinu za kupanua mitaji yao! Mtu anasema kunawanunuzi eti akinunua kwako akakulipa hiyo pesa yako yote inaenda kwake! Ni kama vile kwenye kilimo watu wengi sana wanaamini kuwa kuna watu wanaiba kichawi, eti shamba limestawi vizuri mtu wakati wa kuvuna anaishia magunia kidogo tofauti na matarajio! Ukishaelimika na kutembea sana unabaini kuwa haya mambo ni mauza uza tumepandikiziana vichwani ili tuyaamini.

Watu wanatengeneza pesa sana kwa sababu ya ujinga wetu na hasa ujinga na uvivu wa kutofanya utafiti! Utafiti ndiyo ulifanya wataalamu wakagundua uongo kuwa dunia ni kama mfano wa meza kumbe dunia ni duara! Kwenda kwa waganga ni uthibitisho wa mtu asiyejiamini na hajui anachotafuta na mtu asiye elimika! Hata ukiona wasomi wakienda kwa waganga kumbuka kuwa kwenda shule ni tofauti na kuelimika. Kadri watu wanavyoelimika zaidi imani hizi hupungua sana. Maeneo ya dunia hii yaliyoshikiria sana imani hizi ni maeneo yenye umasikini sana na ujinga. Hata ngazi ya kitaifa mikoa yenye imani zilizojichimbia sana kuhusu uganguzi kuna umasikini na ujinga zaidi. Kadri elimu inavyoingia kwenye jamii taratibu Imani hizo hupungua na kufanya watu wajibidiishe zaidi kufikiri kuliko kutegemea miujiza.

Niwie radhi sana kwa maelezo marefu mimi sinaga dogo mweeee!!
 

x - mas

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
800
500
Hii dunia ni very
complicated linapokuja suala la Imani! Kwa wanaoamini kuwa pesa huja au
hongezeka kwa ngekewa, au bahati, au kuwa na nyota nzuri au wale
wanaodhani wateja huvutwa na majini ni lazima watatafuta wataalamu wa
ndumba! Hapo tena ukute na huyo mjasilia mali au mfanyabiashara maisha
yake yameinamia kwenye kuamini kuwa hao wataalamu wa ndumba ndiyo
wanamajibu ya maswali yote ya hapa duniani!

Amini amini nakuambia biashara inafanywa popote duniani na lugha iko
moja tu! Siri kubwa ya kufanikiwa inatoka kichwani kwa mhusika!
Kufanikiwa kwenye biashara kunahitaji akili ichangamke na wala si kweli
kwamba kila mtu anaweza kufanikiwa kwenye biashara hasa zenye ushindani!
Mtu anawezamaliza waganga wote kama hajui kwamba biashara ni sayansi na
maarifa ya kisayansi ambayo unaweza kujifunza toka kwa waliofanikiwa!
Hata uchanjwe chale hadi makalioni iwapo hujui kwamba mteja ni mfalme,
hujui siri ya kumshawishi huyu mfalme aje kuchukua mzigo kwako, kwa
wakati na kwa ubora anaotaka wewe utaishia kuwaneemesha tu hao waganga!
Kuna mambo mengi sana ya kujifunza ili kufanikiwa kwenye biashara lakini
watu wanafikiri watazipata mbinu hizo kwenye hayo matunguli na kufukua
gagulo makaburini! Watu wasome vitabu, waombe ushauri kwa waliofanikiwa,
wahudhurie mafunzo na semina zinazohusu ujasilia mali hata kama ni kwa
kulipia. Bahati mbaya sana wale wanaoamini uganguzi pekee watabaki
kusingizia watu wengine kuwa ndiyo wamesababisha wasifanikiwe!

Watu hawajui mahesabu ya kujua faida na hasara, hawatunzi vizuri
kumbukumbu za mauzo, hawana mbinu za kupanua mitaji yao! Mtu anasema
kunawanunuzi eti akinunua kwako akakulipa hiyo pesa yako yote inaenda
kwake! Ni kama vile kwenye kilimo watu wengi sana wanaamini kuwa kuna
watu wanaiba kichawi, eti shamba limestawi vizuri mtu wakati wa kuvuna
anaishia magunia kidogo tofauti na matarajio! Ukishaelimika na kutembea
sana unabaini kuwa haya mambo ni mauza uza tumepandikiziana vichwani ili
tuyaamini.

Watu wanatengeneza pesa sana kwa sababu ya ujinga wetu na hasa ujinga na
uvivu wa kutofanya utafiti! Utafiti ndiyo ulifanya wataalamu wakagundua
uongo kuwa dunia ni kama mfano wa meza kumbe dunia ni duara! Kwenda kwa
waganga ni uthibitisho wa mtu asiyejiamini na hajui anachotafuta na mtu
asiye elimika! Hata ukiona wasomi wakienda kwa waganga kumbuka kuwa
kwenda shule ni tofauti na kuelimika. Kadri watu wanavyoelimika zaidi
imani hizi hupungua sana. Maeneo ya dunia hii yaliyoshikiria sana imani
hizi ni maeneo yenye umasikini sana na ujinga. Hata ngazi ya kitaifa
mikoa yenye imani zilizojichimbia sana kuhusu uganguzi kuna umasikini na
ujinga zaidi. Kadri elimu inavyoingia kwenye jamii taratibu Imani hizo
hupungua na kufanya watu wajibidiishe zaidi kufikiri kuliko kutegemea
miujiza.

Niwie radhi sana kwa maelezo marefu mimi sinaga dogo
mweeee!!


maelezo ni mengi lakini yana uzito na manufaa wakati nikiyasoma sikutaka nifikie kikomo kutokana na utamu wake 'big up'Naunga mkono hoja zako upo sahihi. Naweza nikasema 'SIRI YA MAFANIKIO NI JUHUDI NA MAARIFA'hayo mambo ya ndumba ni upotofu wa kimawazo na mitazamo,asante.
 

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,777
2,000
Hawajiamini tu. Wafanyabiashara wasiojiamini ndio hukimbilia huko.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom