Hivi kiingereza ni ishara ya maendeleo au ulimbikeni?

Ringtone

JF-Expert Member
Nov 21, 2013
489
145
Niko ktk folen ya hapa lugalo hospital.nesi anaita jina mkaka hivi anasimama kwa mikogo huku akitembea kama pepe kale vile,ingawa mwili hana kivile!who's calling me?anauliza swali kwa wagonjwa wenzie!naam kamuona nesi kila nesi akiuliza swali yeye anajibu kizungu.basi watu wanamtolea macho naye madoido ndo yanaongezeka.
mara ikaita simu si akaanza kuongea kiswahili akichanganya na kibukoba.sasa kizungu ni ishara kwamba umeendelea?
 
kwikwikwiwiwiw alikuwa baba koku, basi wala usiumiza kichwa atakuwa alikuwa akidumisha mila
 
Ndiyo, Kiingereza ni ishara ya maendeleo, ustaarabu, usomi, hadhi, na mengineyo mengi yaliyo mazuri.

Na ndo maana hata sheria zetu zinaandikwa kwa Kiingereza na hata lugha itumiwayo mahakama za juu ni hiyo.

Kwani ulikuwa hujui?
 
kina koku wanamatatizo sana kwao huko ndo ukijua kiingereza ndo unamaendelao... ila kiingereza huna pesa ni makelele tu akina issue mjini
 
Ndiyo, Kiingereza ni ishara ya maendeleo, ustaarabu, usomi, hadhi, na mengineyo mengi yaliyo mazuri.

Na ndo maana hata sheria zetu zinaandikwa kwa Kiingereza na hata lugha itumiwayo mahakama za juu ni hiyo.

Kwani ulikuwa hujui?

hahaha, apo msee umechemka! kujifunza kiingereza ni sawa na kujifunza lugha yoyote ile duniani!
 
Mimi sijaona kosa lake. Kuna mambo mbali mbali yanaweza kuwa yamechangia.
Inawezekana kakaa nje ya nchi ambapo alikuwa anaongea Kiingereza hivyo kufanya ulimi wake kuwa mwepesi kwenye Kiingereza kuliko kiswahili.
Pia inawezakana kasoma katika shule ambayo wanazuia kuongea kiswahili au kihaya bali kingereza tu na hivyo kufanya azoee hiyo lugha.
Kuhusu maringo hiyo ni huruka ya mtu.
Ila baba Kiingereza bora ukipende tu katika ulimwengu huu wa dotcom. Bila hiyo lugha hata Mchina hamuelewani.
 
Niko ktk folen ya hapa lugalo hospital.nesi anaita jina mkaka hivi anasimama kwa mikogo huku akitembea kama pepe kale vile,ingawa mwili hana kivile!who's calling me?anauliza swali kwa wagonjwa wenzie!naam kamuona nesi kila nesi akiuliza swali yeye anajibu kizungu.basi watu wanamtolea macho naye madoido ndo yanaongezeka.
mara ikaita simu si akaanza kuongea kiswahili akichanganya na kibukoba.sasa kizungu ni ishara kwamba umeendelea?

ndyo tatizo la mtumwa hapendi kuwa huru hata akiwa huru atatamani kurudi utumwani .tumeshindwa kabisa kujivunia lugha yetu.
 
Hiyo uwa inatokea nishamuongelesha kimombo muuza duka nikaona amenitolea mimacho nikashtuka kumbe niko Tz.

Uwa inatokea wengine ni bahati mbaya tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom