Hivi kazi ya wabunge wa CCM ni kumsifia Rais na Serikali na sio kukosoa na kuhoji?

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,738
2,279
Za mda huu wadau,

Nimekuwa nikijiuliza sana kuhusu wajibu wa wabunge wetu wa CCM, Pale wanapoamua kuwa upande wa Serikali asilimia mia moja hali wao ni fimbo ya Serikali.

Unakuta mbunge anasifia serikali kuliko hata anavyomsifia mwezi wake au mtoto wake anapofanya vizuri.

Ikumbukwe Tanzania tuna mihimili mitatu kwa lugha nyingine hii mihimili sio rafiki maana kila mhimili ni sawa na kazi yake ni kumuangalia mwenzake. Kwa manufaa ya wananchi.Maana bila hivyo inchi itakuwa mali ya watu wachache.

Sasa mhimili ambao unatakiwa kumuangalia na kumchunga rais wenyewe ndio unageuka kuwa unapogeza na kuomba uongezewe muda .

Yaani hadi mtu unayesikiliza hoja unabaki unasema,hivi huyu anayeogea haya anajielewa kweli au anamapungufu ya akili.

Mtu anasimama anajenga hoja ya kusema tuiongezee serikali mda na ikibidi usiwepo uchaguzi.

Yaani ameshidwa kuwaza nje ya boks kuwa,endapo kama watajenga bunge imara na katiba imara,hata Rais akiogoza miaka miwili lazima matokeo yataonekana.

Hivi hawajui kuwa wao kama bunge likisimama vizuri wanaweza kujipatia sifa kuliko Serikali maana wao ndio.Wanaoidhinisha matumizi ya serikali na pia wanaisimamia.

Lakini matokeo yake inaonekana serikali ndio inalisimamia bunge na kulipangia nini cha kufanya.

Namshukuru Rais Magufuli kwa kuwaonesha kuwa wanaokosea sana kusema aongeze muda lakini bado wanakomaa tu bila aibu.

Natamani bunge liweke mfumo wa kuiweka Serikali kiti moto ili kuleta maendeleo ya kweli na ya muda mrefu..


Wa sangara
 
Unayosema yote hayawezekani sababu ya rushwa hakuna anayeingia mjengoni kialali na sasa imezuka tabia ya kutangazwa mshindi wakati ameshindwa unadhani hapo mbunge atakuwa na ubavu wa kuibana serikali.
 
Wote si wasafi hao, na Bwana mkubwa anajua hivyo, kwa kuficha uchafu huo inabidi wakubali kila kitu maana jamaa ndo yupo kwenye power.
Kinachobaki ni kusifia tu, bora liende ila meza inachafuka na tumbo linazidi kutanuka. Ndo Tz ya wazalendo hiyo.
 
Kisu cha kukata wabunge jimboni kwa sasa kipo kwa Mr. Chairman. Unadhani hapo nini kitaendelea.

Acha walinde ugali mzee. Kuna mmoja yeye alijisemea kabisa toka amalize chuo hajawai fanya kazi popote zaidi ya bungeni unadhani akitoka hapo ataenda wapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo ni katiba yetu ambayo inalazimisha mbunge lazima atokane na chama cha siasa,mwenyekit wa ccm ndo Rais hapo mbunge hana uwezo wa kupingana na mwenyekiti wake kwani ana uwezo wa kumnyanganya kadi na hapo sifa ya ubunge anakosa, so katiba ndo tatizo kubwa labd kungekuw n wagombea binafsi like Uganda Bobi wine ingesaidia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
lazima katika hotuba yao waseme mtumushi ******** alieletwa na mungu pia uongezee tumuombee lasivyo utatenguliwa
 
Nusu ya wabunge wa ccm wako isivyo halali bungeni na nguvu ya serikali ndio imewaingiza humo. Katika mazingira hayo lazima wasifie serekali tu.
 
Habarini wandugu, napenda kuuliza kwa mwenye kujua hivi wabunge wetu wamepatwa na nini hwatuwakilishi tena sisi hawapeleki tuliyowatuma, hawatusemei. Karibu wote wakipewa nafasi ni kusifia raisi, serikali inaonekana hawaajui hali za wananchi wao. Wamekata/ Hawana mawasiliano na wananchi wanaowawakilisha. Nina wasiwasi uchaguzi wa mwaka huu yanaweza tokea yasiyotegemewa. Ok nimekumbuka kuna nafasi za uteuzi kwa watakaopigwa chini kwenye uchaguzi pengine ndio kinachowatoa ufahamu
 
Huo ndio uwakilishi wenyewe.. hata Magu (MSc) anawakilishwa kwa sifa, nderemo na mapambio. Hujui uchaguzi umekaribia?
 
Habarini wandugu, napenda kuuliza kwa mwenye kujua hivi wabunge wetu wamepatwa na nini hwatuwakilishi tena sisi hawapeleki tuliyowatuma, hawatusemei. Karibu wote wakipewa nafasi ni kusifia raisi, serikali inaonekana hawaajui hali za wananchi wao. Wamekata/ Hawana mawasiliano na wananchi wanaowawakilisha. Nina wasiwasi uchaguzi wa mwaka huu yanaweza tokea yasiyotegemewa. Ok nimekumbuka kuna nafasi za uteuzi kwa watakaopigwa chini kwenye uchaguzi pengine ndio kinachowatoa ufahamu
Wewe mwanamke ni mjinga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mwak 2020! Ni mwaka mwingine tena wanasiasa watapigania matumbo yao na ya familia zao ifikapo Oktoba. Hivyo unyenyekevu dhidi ya serikali na vyama vyao, haukwepeki.
 
Back
Top Bottom