Hivi Kazi Ya Wabunge Si Kuchochea Uwekezaji Mfano Shinyanga, Ruvuma, Singida, Lindi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Kazi Ya Wabunge Si Kuchochea Uwekezaji Mfano Shinyanga, Ruvuma, Singida, Lindi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by August, Nov 24, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Ili kueteleza Maendeleo ya Nchi yetu na Kupunguza tatizo la Watu kukimbilia Arusha, Dsm, na Mwanza Ni lazima Serikali ikawa na Mipango endelevu ya ku-balance Shughuli za Kilimo na Uendelevu wa Shughuli Nyingine za Kibiashara Kama Viwanda Ambayo Itakuwa Pia ni Kichocheo cha Kuendeleza Miundo Mbinu Mingine Kama Barabara, Umeme, Nyumba Bora na Elimu. Ni meliona tatizo Hili Hususana Katika Mikoa ya Shinyanga, Singida, Tabora, Lindi, na Ruvuma, mfano
  Singida, wana Potential Kubwa saana ya Kimaendeleo Lakini Kikwazo Cha Barabara na Umeme Unakwanza Juhudi za Kuibadili Singida, Au ndio Tuna Subiri Jumuiya ya Afrika Mashariki Ichoche hayo Maendeleo? na Hata Mkoa Wa Ruvuma Hali Ni Hiyo Hiyo Mpaka Mbinga. Pale Singida kuna Alizeti, Kuna Pamba , Vitungu , Kuku wa Kienyeji, Mbuzi nk

  JK afungua Kiwanda Cha Nguo USA River Arusha
  Wawekezaji nchini wametakiwa kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi, nguo na kushona mavazi kwani kwa kufanya hivyo si tu wataongeza ajira na mapato ya nchi, bali pia watawahakikishia wakulima wa zao la pamba masoko ya uhakika na bei nzuri ya zao hilo.

  Rai hiyo ilitolewa juzi na Rais Jakaya Kikwete wakati akizungumza na wananchi pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha Jambo Spinning Mill kilichopo Usa River mkoani Arusha mara baada ya kufungua kiwanda hicho.

  Rais Kikwete alisema kinachotakiwa hivi sasa ni kuongeza uzalishaji wa zao la pamba kwani kwa wastani, wakulima nchini wanazalisha kilo 200, 250 hadi kilo 300 wakati wakulima wa nchi za nje wanazalisha kilo 800 mpaka zaidi ya kilo 1,000 kwa hekta.

  “Sisi tunao uwezo wa kuzalisha pamba kwa wingi zaidi ya tunayoizalisha hivi sasa mara mbili hadi tatu kama tutaamua kwani bado hatujaanza kazi ya kuzalisha pamba hadi ikafika mahali tukajidai na hii ni moja ya shabaha kubwa ya serikali katika mkakati wa kusukuma kilimo kwa kasi kubwa zaidi ujulikanao kama Kilimo Kwanza,” alisema Rais Kikwete. Rais Kikwete alisema serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi na wawekezaji nchini hivyo basi ina jukumu la kuweka mazingira mazuri ili wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza.

  “Hivi sasa serikali inaondoa vikwazo vya kuzuia uwekezaji hapa nchini inachofanya ni kuharakisha utoaji wa leseni, kuondoa urasimu katika masuala ya ulipaji wa kodi, kuwezesha viongozi na watendaji wa serikali kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati mwafaka na kuwezesha shughuli za uwekezaji kufanyika katika uwazi na kumalizika katika kituo kimoja,” alisema.

  Aidha, Rais Kikwete pia aliwataka wamiliki wa kiwanda hicho kujitahidi kuangalia maslahi ya wafanyakazi wao kwani kama watawaenzi na wao watafanya kazi kwa bidii na uaminifu, jambo litakalowezesha kiwanda kudumu na kutoa huduma inayotakiwa kwa wananchi.

  Akisoma taarifa ya kiwanda hicho, Mkurugenzi Mtendaji wake, Salum Hamis Salum alisema nyuzi zinazotengenezwa katika kiwanda hicho, zinatokana na pamba ya nchini inayochambuliwa na kiwanda tanzu na hicho cha Jambo Ginnery kilichopo mkoani Shinyanga. Salum alisema matarajio ya kiwanda hicho ni kufikia uwezo wa kufuma nguo za kisasa, kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi huku wakiwa na lengo la kuingia katika soko la AGOA.

  "Changamoto zinazotukabili ni kuyumba kwa uchumi wa dunia ambako kwa kiasi kikubwa kumeathiri sana soko la nyuzi na gharama kubwa za uendeshaji wa kiwanda ikiwa ni pamoja na kupanda kwa gharama za umeme,” alisema Salum. Mwaka 2004, Watanzania wanaomiliki kiwanda hicho walianza uwekezaji wa zaidi ya dola za Marekani milioni 50 katika ujenzi. Matarajio yao ni kukipanua zaidi kwa kuongeza uwekezaji hadi kufikia dola za Marekani milioni 200. Kwa sasa kina wafanyakazi 220 na matarajio ni kuwa na wafanyakazi 1,000
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Tatizo la nchii hii kila kitu kaskazini, mikoa mingine imesahaulika kabsaa, Ruvuma sasa wamegundua hiyo uranium, Chuma ipo miaka mingi kule liganga na makaa ya mawe lkn zimejaa porojo tupu miaka nenda miaka rudi, Pamba ilipigwa marufuku kulimwa mikoa ya kusini eti sababu ya mdudu mbaya wa pamba anayepatikana msumbiji, Umeme miaka arobaini na zaidi ya Uhuru mikoa ya kusini haijaingizwa kwenye gridi ya taifa, hapo unategemea kutapatikana maendeleo kweli? Wale wamisionary pale Peramiho walikuwa tayari kuleta umeme wa maji kutokana na vyanzo vya mito iliyopo kule lkn serikali na siasa zake ikakataa. Haya leo hii nimesoma humu humu JF Lindi na Mtwara kuna deposit kubwa ya Gold, kama ilivyokuwa miaka ya tisini watu walienda sana Tunduru kwenda kuchimba haya madini lkn serikali haikufanya lolote. Mikoa ya kusini km ilivyo nchi yetu ni tajiri sana wa madini lkn hii serikali bana ipo ipo tu, sijui ni jitihada gani inafanya, wao kila kitu ni ARUSHA, Kilimanjaro na Mwanza. Hebu angalia mbuga kama selou, ni watanzania wangapi wanaifahamu? haitangazwi hata kidogo lkn wanyama wapo tele, lkn kila tukiamka ni serengeti, manyara, Ngorongoro, na siku hizi ukipita pale mikumi ndo utalia ufe mbuga imekuwa jangwa, yaani hakuna mwenye uchungu. Kuna ziwa Nyasa wala halitumiki ipasavyo, Bandari za Lindi na Mtwara nazo, lkn nasikia Mkulu anajenga nyumbani kwake Bagamoyo bandari mpyaa. kila siku huwa najiuliza hawa wabunge wa mikoa ya kusini waliopo bungeni wanafanya nini huko? kusinzia tu akina KOMBA, sijui Jenista Mhagama, yule mtoto wa Kawawa aaagh inachefua kwa kweli.
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Mkuu. kama ulivyo eleza, kule Mbinga wanapakana ni Ziwa Nyasa, lakini kutokana na Miundo mbinu mibovu, watu wanashindwa kuwekeza kwenye mambo kama Beach , na Hotel za Kitali, wakati Ndugu zetu wa Malawi kwao wanatumia hili ziwa ipasavyo, ukienda Mtwara, bandari ndio hivyo imelala kama sio kufa, ambayo ingesaidia kukuza biashara hapo Mtwara na kuongezea na Miundo mbinu ya Barabara kwenda Tunduru, Ruvuma, nk, wao wanapenda Hadithi za MGC ya Bush, ambayo sasa imeingia kigugumizi kutokana na Ufisadi, na licha ya hivyo kwanini mpaka tusubiri hiyo fedha ya Bush? yaani miaka 40 ya Uhuru wetu ni Hadithi tu. Kidogo nawapongeza Halmashauri ya Mbinga kwa Kuwekeza kwenye Umeme wao, ni Mategemeo Yangu Mikoa mingine watajifunza kutoka Mbinga na Sio kusubiri Umeme wa Mafisadi, Maendeleo ya Sehemu kwanza huletwa na Wakazi wa sehemu Husika wakisaidiana na Viongozi wao (Wabunge), wakiisubiri hii serikali ya Kifisadi watakula wa Wali wa Chuya.
  Kuhusu Mbuga kuna Pia ya Katavi, Huko Rukwa labda sasa hivi Pinda atashughulikia kwa ukaribu, lakini juu ya Yote kwa nini tusubiri bahati nasibu wakati vitu vipo chini ya uwezo wetu.
   
Loading...