Hivi kazi ya mawaziri ni kuinadi CCM?

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,047
6,508
Hivi karibuni baada ya kumalizika mkutano mkuu wa CCM Kanali (mstaafu) Kinana amekuwa akizunguka huku na kule akiambatana na mawaziri kufanya siasa yenye nia ya kuijenga CCM.
Binafsi sina tatizo na Waziri kama yuko likizo akatumia muda wake wa mapumziko kutumikia chama. Ninashawishika ni kinyume cha taratibu za kazi kutumia rasilimali za umma kama magari, posho za safari kutoka serikalini kwa lengo la kutumikia chama.
Nadhani ni vema kazi ya kujenga chama wakaachiwa waajiriwa wa chama watennde kazi hizo.

Nidhamu na kuheshimu kazi na uweledi ni muhimu sana kwa sasa katika jamii yetu sisi Watanzania.
Hizo kazi za wizarani nani atafanya kama kila waziri akiwa barabarani kujenga chama?
Napendekeza CCM iweke mfumo wa kuigwa na vyama vingine. Hivi mfanyakazi wa umma wa kada ya chini akiacha kazi zake na akitumia gari ya ofisi na rasilimali zingine kufanya kazi za NGO binafsi kwa mfano, na jambo hilo likafanyika bila makubaliano rasmi na bosi wake ataangaliwa tu aendelee au atawajibishwa?Jibu liko wazi atawajibishwa.
Ifikie mahali mawaziri wawajibike kwa umma kwa kuwa wanalipwa kwa kodi zetu na hawalipwi na CCM

Rai yangu ni kuwataka mawaziri na watumishi wengine wa umma tuwatumikie Watanzania kwa nidhamu na unyenyekevu kwa kuwa si wote wanafurahishwa na porojo za majukwaani. watu wanataka kuona kazi zinafanyika zinazoleta tija katika jamii.

Wanapokuwa katika ziara hizo ni kazi ngapi ambazo zinalala Wizarani? mafail na mambo mengi yanakuwa yanasubiri baraka za Waziri, hivyo wanachelewesha mambo kwa kiasi kikubwa. Hili ni tatizo la mifumo yetu, sheria zetu na taratibu zetu. Tumeshindwa kabisa kuwa na mfumo ambao unatenganisha shughuli za chama kilichopo madarakani na shughuli za Serikali. Nionavyo mimi, Waziri, Rais, waziri mkuu etc wanatakiwa kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi zao za vyama. Sasa wanapopanda katika majukwaa na kufanya kazi ya chama, je wananchi ambao ni wanachama wa vyama vingine wanakuwa na nafasi gani? Je hawabaguliwi hapa? na jee gharama zao zinalipiwa na nani? Na CCM? magari yao? na madereva ni wa CCM? Nadhani zinalipiwa na walipa kodi wote ambao wana itikadi tofauti, iweje sasa yeye atumie kodi zetu kukijenga chama cha mapinduzi? ambacho wengine hakubaliani na sera zao za chukua chako mapema na tumeona kimeshindwa kazi? kikae pembeni?

Hapa lipo tatizo. Tumeshindwa kuwa na mpaka ulio wazi kati ya shughuli za chama na serikali. Na hili ni hata kwa watumishi wa umma. Tumeshindwa kuwa na watumishi wa umma ambao hawafungamani na chama tawala. Mtumishi wa Umma yupo pale kuwatumikia wananchi, wanatakiwa kubaki kuwa hivyo hata chama gani kikija kutawala wao wanabaki vilevile. Na hata taasisi zetu nyingi sio huru. Tatizo hili ni vizuri tukajaribu kuli-address katika zoezi linaloendelea hivi sasa la mabadiliko ya katiba.

Moja ya ndoto yangu kubwa katika zoezi hili ni kuweza kutupatia taasisi huru, watumishi wa serikali huru, kutenganisha shughuli za chama na serikali, tuweze kuwa na mgawanyo wa madaraka mazuri kati ya yale mafiga matatu; Bunge, Mahakama na Dola. Pia tuweze kuongeza utamaduni wa vyombo hivi kuchungana na kudhibitiana, yaani checks and balances. Unaweza kufakinisha mambo haya iwapo tu tutapunguza madaraka makubwa ya Rais na kuangalia muundo wa taasisi na vyombo vyetu kadhaa kama vile Bunge. Sijasikia mjadala katika zoezi la marekebisho ya katiba kuhusu Bunge letu. Ninaamini katika taasisi ambayo ina muundo mbaya, muundo wa kiimla na kidikteta ni Bunge letu. Kwani nionavyo mimi, Spika ana madaraka makubwa ndani ya Bunge. Yeye ni Alfa na Omega. Inabidi tubadilishe muundo huu. Na jee Spika na Naibu Spika wanapokuwa wametoka katika chama cha siasa, tena ni wajumbe wa NEC na kamati kuu, je wanaweza kuendesha shughuli za Bunge bila upendeleo? Je Spika ambaye pia ni mjumbe wa NEC na kamati kuu ni wakati gani anakuwa Spika na ni wakati gani anaacha kuwa mjumbe wa NEC na Kamati kuu? Anawezaje kuvaa kofia hizi mbili bila kuathiri demokrasia na haki ndani ya Bunge?? Haya ni mambo ya kuyajadili kipindi hiki.

Vyombo vingine ni kama vileTAKUKURU, TBC1, Magazetui ya Serikali, Jeshi la Polisi, Mahakama na hasa uteusi wa majaji. Katika hili la uteuzi wa majaji, ningependa kuuliza swali moja: Katika siku za hivi karibuni, utasikia mara nyingi sana, Serikali kupitia Mawaziri ikisema kuwa kama mnaona mmeonewa, nendeni mahakamani, ni wepesi sana kuwaambia watu waende mahakamani. Swali langu ni je, kwa nini wakimbilia kuwaambia watu kwenda mahakamani? Je wana uhakika wa kushinda kesi siku zote? iwapo unatambua kuwa Mahkamani kuna kushinda na kushindwa, kwa nini ukimbilie kumwambia mtu kwenda mahakamani?!! kwa nini usishauri njia za mashauriano? Lingine la kuangalia, kwa nini mambo mengi yanapelekwa mahakamani halafu serikali inasema haliwezie kujadiliwa kwa sababu lipo mahakamani? kwa nini zinafunguliwa kesi haraka haraka katika matukioa ambayo yana utata ili kuzuia mijadala? Kwa nini mamlaka zinazohusika zinakubali kufungua haraka haraka ambazo hazina kichwa wala miguu? yule kichaa aliyetangazwa na Kova na aliyekamatwa eti kuhusika na kumtesa Ulimboka ameishia wapi?? 2015 ukisikia Kova anawania Ubunge kupitia chama cha CCM jimbo la Kinondoni, utashangaa?? Je mambo haya yananahitaji akili sana kujua kuwa hatuna taasisi huru?? Ukisema kuwa taasisi zote zinatumikia chama tawala umekosea???

Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na hasa uteuzi wake, nadhani huyu ni vyema akathibitishwa na Bunge, na jee kuna haja ya yeye kuwa Mbunge?

Je kuna mantiki gani, kwa mfano, Rais kuteua watendaji wakuu wa mifuko ya jamii?? kama vile NSSF n.k.??!! Kwa nini nafasi hii isiwe ya ushindani wa wazi?? Kwa Rais kumteua Mtendaji mkuu wa NSSF naona ni sawa kabisa na Rais kwa mfano, kumteua Mtendaji Mkuu wa NMB au NBC! Rais ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Tawala anapomteua Mtendaji mkuu wa NSSF, halafu NSSF wakitumia pesa za michango yetu kuikopesha serikali iliyopo madarakani ili ijenge machinga complex na chuo kiuu cha Dodoma, halafu CCM ijitape kuwa imefanya makubwa kwa kujenga chuo kikubwa, je huoni kuwa hapa kuna mfumo mchafu ambao umehalalishwa, umesafishwa na unatumika kuwahadaa wananchi na kuhakikisha kuwa chama kilichopo madarakani kinapata upendeleo wa kuendelea kukaa madarakani. Na hii sio haki kwa vyama vingine na kwa Watanzania wote hasa wale wanaochangia mifuko hiyo. Kwani hawawezi kukopa hata shilingi elfu kumi kutoka katika michango yao!!!!

Je kuna mantiki gani kwa Rais kuteua Wenyekiviti wa bodi mbalimbali?? kama vile TANAPA, Korosho Pamba? Kahawa n.k??!! Kwa nini asichaguliwe na wadau wenyewe miongoni mwao?

Je ni kwa kiasi gani Jeshi la polisi ni neutral? tumewahi kushuhudia Makamanda waandamizi baada ya kustaafu wanagombea nafasi za kisiasa kupitia chama tawala!! Je ni lini walichukua kadi za chama tawala? au walikuwa wakifanya kazi za polisi huku wakiwa ni wananchama wa chama tawala? na hivi ni kinyume na sheria!! Tumewahi kuona msajili wa vyama vya siasa baada ya kustaafu akigombea nafasi ya kisiasa kupitia chama tawala!! si hao tu pia wapo Makatibu wakuu, mabalozi, watendaji wakuu wa taasisi mbalimbali na mashirika ya umma!! Lakini hatujawahi kuona watu wa aina hii wakigombea kupitia chama chochote cha upinzani!!! je ni kwa nini???

Njia pekee ya kuleta uwajibikaji ni kupuguza madaraka ya Rais na hasa huu utitiri wa uteuzi ambao hauna kikomo na wala hauwezi kuchungwa wala kudhibitiwa. Matokeo ya uteuzi huu wa utitiri unaleta hulka na tabia mbaya sana ya kila mtu kujipendekeza, kufanya unafiki na fitna kwa minajili ya kusubiri uteuzi. Matokeo yake ni kulindana na kukosekana kwa uwajibikaji.
 

Kimagege

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
283
88
hii nchi wanaichuma a kama shamab la bibi.kimsingi hiyo sio kazi yao ila inawabidi wafanye kwani ccm wakiondoka madarakani ulaji nao utaondoka.its more important ccm kubaki ikulu even if that will mean wanachi kula nyasi.
 

Chipolopolo

JF-Expert Member
Feb 14, 2012
1,425
724
Una hoja ya nguvu mkuu na si hoja ya nguvu.Binafsi nimeyakubali mawazo yako.Kwa mtindo huu wa mawaziri kuzunguka na makada wa CCM ni kama wanataka kuturudisha enzi za chama kilipokuwa kimeshika hatamu.
 

Kitanga

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
366
227
Kazi ya Mawaziri si kuwa makada wa chama cha siasa. Wao wana majukumu ya kuhakikisha sera za nchi zinatekelezwa kutokana na bajeti husika na kushauri Rais juu ya utekelezaji wa mambo ya kisera. Waziri wa Elimu anatakiwa kuhakikisha wizara yake inatekeleza Sera ya Elimu ya 1995 kwa ufanisi mkubwa yakiwamo masuala ya utoaji wa elimu bora, kuwaendeleza walimu, ujenzi wa Maktaba na Maabara, ujenzi wa nyumba za ualimu, upatikanaji wa madawati na mengineyo. Ndo maana baadhi ya Mawaziri hawajafika huko maana wataeleza nini kuhusu mfano, wanafunzi kumaliza darasa la saba bila kujua kuandika na kusoma? Au kwa nini walimu waendelee kukopwa hata haki zao za msingi kama vile hela za likizo na promosheni?

Katiba mpya itasaidia kubadili utumiaji mbaya wa fedha za umma kw njia hii. Lazima mawaziri, Wakuu wa Mikoa/ Wilaya waiwe makada wa vyama. Inawezekana. Tutoe maoni yetu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom