Hivi kazi ya bunge ni kuisafisha Serikali na sio kuisimamia? Naona bunge limejipanga kuisafisha Serikali dhidi ya ripoti ya CAG

masara

JF-Expert Member
Jul 20, 2016
1,738
2,279
Za muda huu wadau,

Kama wengi tunaofatilia mtifuano kati ya Speaker na CAG ambapo wengi wa wachambuzi wanashidwa kutoa taswira ya moja kwa moja kama Spika anatumika na upande wa kulia au ni msimamo wake tu.

Nimesikiliza kwa makini na kutafakari Speaker Ndugai alivyo-ongea na waandishi wa habari baada ya kutoka ziara za ulaya.

Pale anaposema, hizi taarifa za CAG sio za kuamini moja kwa moja na kuanza kuzitangaza udhaifu wake maana kwa taraibu ni kwamba zinatakiwa zipelekwe PAC na LAAC na wao ndio wawahoji wanaotuhumiwa ndio kamati hizi zitoe hitimisho.

Swali langu ni kwamba, anaposema tusiziamini hadi wawahoji na anaposema ataweka utaratibu wa wenyeviti wa kamati wawe wanatoa taarifa ya kila riport na ufafanuzi wa kina tofauti na wa mwaka jana.

Mawazo yake ni sawa lakini,ukiangalia kwa upande wa pili ni kama anajipanga kuishafisha Serikali dhidi ya taarifa ya matumizi mabaya ya fedha maana katika maelezo yake alielezea,watuhumiwa wataaitwa na kuonyesha vielelezo vya matumizi. Lakini hakuelezea kama atawabana waeleze kwa nini taarifa ya C.A.G. imeonesha uchafu huo.

Kwa maelezo hayo ni wazi kabisa bunge letu kwa kipindi hiki limejipanga kuisafisha Serikali kwa namna yoyote ile dhidi ya ripoti ya CAG na ili CAG aonekane hakutoa taarifa sahihi.

Tujikumbushe (kama sikosei) mwaka jana kuna ile riport ya tilion 1.5, kutojulikana.

Baada ya wananchi na wabunge wa upinzani na wananchi.kupiga kelele. Taarifa ya kamati ya bunge ilikuja na taarifa ya kuisafisha na kuelezea pesa ilikoenda.

Lakini kilichonishangaza wabunge wa CCM walianza vijembe kwa wapinzani juu ya madai yao.

Sasa unajiuliza hivi wabubge wetu wanasimamia serikali au ni kinyume chake

Wa sangara
 
Ndio udhaifu wenyewe huo mkuu, na sasa udhaifu unaingia wa kiwango cha juu kuwahi kutokea kwenye historia ya ulimwengu, bungu la TZ limeondoa hadhi ya neno bunge duniani.
 
Nilimshangaa Spika eti kusema anawaamini hao PAC sijui na hao wengine eti kuwaamini kuliko mtoa ripoti nikajua ana tatizo sio bure yaani hao wana kamati wataweza kujua tatizo wamshinde mhasibu mbobezi kuna tatizo kwa baadhi ya vichwa vya watu kabisaa...huko kwenye kamati zenu mmechaguana tuu bila kuzingatia taaluma zenu ndio maana muda wote mnaogopa kuisimamia Serikali...
 
Hilo sio bunge tena bali ni genge washangiliaji wakimshangilia mtukufu ..nakusema anastahili kupewa sifa za Kila aina
 
Ndugai kamfunika Waziri Mkuu kwa kutetea Serikali dhidi ya Hoja za Spika

Huenda Ndugai anatamani cheo cha Majaliwa

Yale yale ya Lowassa na Samuel Sitta
 
Back
Top Bottom