Hivi Kaunda suti ndio vazi rasmi la walinzi wa viongozi?

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,320
Kaunda suti ni vazi naona linavaliwa sana na viongozi wetu hapa Tanzania kuliko nchi yoyote Africa kama sio Duniani.

Lakini kaunda haivaliwi na viongozi tu, kaunda inapendelewa hata na taasisi za ulinzi na usalama wa nchi yetu.

Walinzi wa rais na viongozi wakuu kaunda suti ni kama vazi lao rasmi, usipowakuta kwenye suti za kawaida hizi ambazo pia wanavaa mara chache sana utawakuta tu kwenye kaunda suti.

Naomba kuuliza, je kaunda ndio wazi rasmi la walinzi wa viongozi wetu?
 
Zipo nyingi.Kuna kombati (vitenge) za JWTZ,Nguo zisizo fanana/sare,kanzu,suti za kimagharibi,nguo za kawaida zinazovaliwa na makoti marefu ya mvua na hizo Kaunda suti.
 
Ni vazi lililo frexible ana uwezo wa kuhifadhi silaha yake na bado akaonekana nadhifu bila kubanwa na ndio maana vazi kma la suti wanavaa mara moja moja hasa kwenye special occasion(mtazamo huru)
 
Unajua ukiuliza kitu jitahidi uulize kile ambacho leo na kesho kitakusaidia sasa unataka kujua sawa je ukaambiwa ndio.
Siku ukakutana na mtu kajivalia tuu kama ulivyoaminishwa tayari unahisi au unaingiwa na hofu kuwa huyu ni mfu fulani kumbe ni laa hivyo haitakusaidia chochote mkubwa hata ukijua
Unaonekana weye si mwenzetu.Kwani haupendi stories za kumezea kahawa?
 
Unajua ukiuliza kitu jitahidi uulize kile ambacho leo na kesho kitakusaidia sasa unataka kujua sawa je ukaambiwa ndio.
Siku ukakutana na mtu kajivalia tuu kama ulivyoaminishwa tayari unahisi au unaingiwa na hofu kuwa huyu ni mfu fulani kumbe ni laa hivyo haitakusaidia chochote mkubwa hata ukijua
jamaa mkali
 
Wanasema ..."kuuliza si ujinga"...!Inaonekana ukiwa stendi huwa hufuatilii misemo na nahau za kiswahili.
 
Flexibility ndo sababu nahisi! Na zile kaunda zao zina mipasuo sana kuwapa urahisi wa kunyumbulisha mwili nafikiri...inapolazimika kufanya hvo
 
Mimi naona wangekuwa wanavaa misuli na vizibao ndiyo wangekuwa flexible zaidi.Maana hata kukimbia au kuruka mitaro wangekuwa hawana wasiwasi wa kuchana nguo au zikawabana.
 
Mkuu inabidi uwe flexible and still look smart...
 
Back
Top Bottom