hivi kauli hii ina ukweli wowote naomba maoni yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

hivi kauli hii ina ukweli wowote naomba maoni yako

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Aug 14, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  professor mmoja tz amesema ni aibu kwa nchi kama Tanzania, kukumbatia Kiingereza, kitendo alichosema ni sawa na kuwatengeneza wasomi wenye uwezo wa kukariri badala ya kuelewa wanachokisoma...hivi kuna ukweli wowote`??maana nchi nyingi za ulaya zinatumia lugha zao kwa kufundishia mashuleni mpaka vyuo vikuu english kwao imekua kama lugha ya biashara tu kuwaunganisha kimataifa ila kwa mujibu wa mtaalamu huyu wa lugha anasema kua hili suala la lugha ya Kiswahili kuwa ya kufundishia, limezua mjadala kwa muda mrefu, lakini mpaka sasa hatuna kinachoeleweka…kwa nini isitumike kuwa lugha rasmi ya kufundishia katika shule na vyuo vyetu?

  “Kwa kukumbatia Kiingereza sijui tunalenga kuwapa maarifa vijana wetu!

  Tunafundishanaje kwa lugha za kukopa? Nashauri kwa kuanzia, somo la Uraia lifundishwe kwa Kiswahili kwa sababu linagusa Watanzania moja kwa moja,” alisema.

  Aliongeza: “Wengine wanahofia tukiruhusu Kiswahili basi Kiingereza kitashuka au kupotea,
  jamani Kiingereza si Biblia au Korani.

  Mbona China wanatumia zaidi Kichina lakini wanajua Kiingereza? Lakini sisi tunang’ang’ania
  kuungaunga sentensi katika Kiingereza, sababu ni kwamba, tunalazimisha.”

  Alishauri, kwamba kama zilivyo nchi nyingine duniani zinazoenzi lugha zao za asili, huanzisha vituo maalumu vya lugha za kigeni, hivyo kuwafanya raia wao kuwa na uwezo wa kujua lugha zaidi ya moja bila kupoteza lugha zao za asili.

  Alitolea mfano wa Iceland, kwamba ingawa ni nchi ndogo ya kisiwani, ikiwa na raia
  wasiozidi 350,000, lakini imeweza kulinda lugha yake kwa kuifanya ya kufundishia hadi chuo kikuu.

  “Sasa kama hawa wenzetu wachache wanafahamu umuhimu wa lugha yao, kwa nini si sisi?

  Utashangaa hata miswada bungeni inaandikwa kwa Kiingereza, wakati hata baadhi yetu hatuijui kabisa lugha hiyo.

  “Mahakamani nako kumbukumbu kuanzia mahakama za wilaya zinaandikwa kwa Kiingereza!

  Tunamwandikia nani? Nashauri tuwe na uzalendo wa kweli na tukifanye Kiswahili kuwa ni lugha ya kufundishia nchini.”
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ipeleke JUKWAA LA LUGHA
   
 3. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  umesahau kuwa Tanzania ukijua kuongea kiinglishi ndo umesoma hata kama ulifeli kwa darasa!!!
   
 4. V

  Vonix JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Watz hawaaminiki,anasema hivi anafanya vile uchwala tu hajui anachosema,mchunguze utakuta watoto wake wako nje kama si kenya au uganda.wachaga na wahaya hawezi akawaambia upuuzi kama huo,vijana wetu wamechanganywa sana na mitaala ya elimu ya nchi hii. nini maana ya kumfundisha mwanafunzi kiswahili masomo yote primary na kiingereza kama somo moja,halafu akifika form one masomo yote kiingeza,kiswahili kama somo moja.unategemea huyu mwanafunzi atafaulu form four subutu???? atafaulu kwa kukariri tu.na madhara atakayo pata mwanafunzi huyo ni huko elimu ya juu. Katika hili hakuna anaelizungumzia watu wanaona mfumo huu uko sawa sawa wanakaa kimya.
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  PROF yuko sawa.tudumishe lugha yetu.
   
 6. o

  ommie Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Prof yuko sawa ila ye amesoma na lugha gani?
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa jamani kama sheria za nchi tu zimeandikwa kwa kiingereza (so i heard) inakuaje mnang‘ang‘ana kudumisha lugha msiyoitilia maanani?!Na watu wasipojua kiingereza nani atawatafsiria sheria zao na mikataba inayoletwa kila siku?!Wageni?!
   
 8. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Duniani hakuna nchi yoyote iliopiga hatua ya maendeleo kwa kutumia lugha ya kigeni!
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  uko sahihi kabisa ndio maana tunashindwa kuendelea mpaka leo hii kwasababu tunatia saini mikataba tusiyoielewa na yanapotokea matatizo ya kisheria tunashindwa kutetea
   
 10. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Fuatilia kwa makini umombo wa spika mh, Anna Makinda.
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Bahati mbaya saaana nimesahau source yah ii infor nilipoisoma for ni kitambo saana. Kuna research ilifanywa ya kutumika kwa Kiingereza Vs Kiswahili katika kufundisha masoma darasani… huo utafiti ulilenga kwa wanafuzi wa Secondary schools.. Inasemekana kua walichukuliwa wanafuzi 10 bora kwa kufaulu darasani NA wakachukua wanafunzi ambao ni kumi wa mwisho katika kufaulu darasa hilo hilo… Hao wanafunzi walipo fundishwa somo la science kwa kiingereza… wale kumi bora walifaulu vizuri kama kawaida yao – na wale kumi wa mwisho walifeli kama kawaida yao….

  Hilo somo liliandaliwa kwa Kiswahili na wakafundishwa upya… na vile vile kupewa tena mtihani kama awali – wale kumi bora walifaulu vizuri kama kawaida yao alafu wale kumi wa mwisho walifeli kama kawaida yao pia… Huu utafiti uliandikwa kwa kirefu… na ulinivutia saana.

  Nafikiri wazo la kupromote Kiswahili ni wazo zuri lakini sio kwa kigezo tu cha kusema wanafunzi ndo wataelewa saana….
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mpaka hapo tunaweza kufikia muafaka i kwamba kiingereza ni muhimu kwetu kuliko hata kiswahili.Kwasababu mambo mengi ya muhimu yapo katika lugha ya kiingereza..Kama tunataka KWELI kukidumisha kiswahili tuanze kukipa umuhimu kwenye kila nyanja...sio tunaimba kiswahili lugha yetu wakati mambo muhimu na ya maana yanawakilishwa kwa lugha ya kigeni.
   
 13. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  AshaDii, nimeipenda sana hii
   
 14. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #14
  Aug 14, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Niliipenda pia... hapa niko accessing my brain... nataka niiwakilishe hapa
  najua wengi wata pata one or two things ambazo ni constructive...
   
 15. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  kama aina athari zoznte zile iachwe hapa
   
 16. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  kwa nini uanzie katikati....anza mwanzo.......Vasco......
   
 17. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  BAKITA haina ofisi inayoendana na hadhi na majukumu yake. Tuanze na hilo. Aibu aibu aibu aibu aibu aibu aibu gani iliyoje hii...!! Loh.
   
 18. M

  Mr.creative JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kwa sasa hatuwezi kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia kwani lengo letu kwa sasa nikuwa na soko la ajira kimataifa
   
 19. bht

  bht JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  kiswahili chenyewe (fasaha) kinatupa tabu....
  vitabu na nyenzo za kufundishia (material) vimeandikwa kizungu
  Haya sasa hicho kiswahili sijui tuanzie wapi (wengi watasema tutafsiri nyenzo)
  Wakati mwingine tunapenda sana kuhamisha lawama, yaani lugha ndo inaonekana kukwamisha maendeleo ya elimu nchi hii....

  BTW Asha Dii asante kwa hiyo taarifa (which I concur with)
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Aug 15, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli Waingereza wana kila sababu ya kujiona wao wako juu! Kudadadadeki!

  Na hapo kwenye sheria za nchi mimi ndiyo ninachoka kabisa. Sheria zipo kwa ajili ya wananchi wote na kwa manufaa yetu sote. Wananchi tulio wengi hatukijui vizuri Kiingereza. Sasa kwa nini hayo masheria yanaandikwa kwa Kiingereza? Yanaandikwa kwa lugha hiyo kwa manufaa ya nani? Ukisikia ujinga, upumbavu, na nusu ujuha ndiyo huo sasa.

  Haingii akilini kabisa kuandika hayo masheria kwa lugha ya kigeni wakati tuna lugha yetu nzuri tu. Hivi ni nchi gani ya Kiafrika ambayo inaandika sheria zake kwa kutumia lugha yao? Ukiondoa labda kule Afrika ya Kaskazini huku kwingine kote kusini mwa jangwa la Sahara nadhani wote tunatumia mojawapo ya hizo lugha za wakoloni wa kizungu. Kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo.

  Na kama hatuwezi hata kuandika sheria zetu wenyewe kwa kutumia lugha yetu wenyewe kuna jingine ambalo tutaliweza kweli? Sidhani hata kidogo.

  Sijui lini Waingereza wataanza kuandika sheria zao kwa kutumia lugha ya Kiafrika! Na kwa kuendelea kushobokea Kiingereza daima milele sisi tutaonekana duni mbele yao. Na hatushobokei lugha tu bali hata mifumo ya kiutawala tunashobokea.
   
Loading...