Hivi katika mazingira haya kuna haja gani ya ndoa?

Andie

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
713
1,636
Salaam wakuu,

Kichwa cha habari nimekiweka kuchochea majadiliano ya mazingira ya "usasa". Awali ya yote niweke wazi mimi nimeoa na Mungu mpaji kanibariki mtoto mmoja wa kiume (asante Mungu) japo nina elimu ila misingi ya familia yangu kwa kweli nimezingatia maadili na tamaduni naweza sema nimechagua kubaki "mshamba" katika kipengele cha ndoa na kuupisha "usasa" unaoshabikiwa na vijana wengi wa kileo.

Nitatibua mjadala kwa mtindo wa kuuliza maswali na nianze kwa kuuliza kuna haja gani ya ndoa kama mwanaume kasoma na ana kazi yake na maisha yake na mwanamke amesoma ana kazi yake? Je hawa wote wanatoka asubuhi na kurudi jioni wote wanamfumo sawa wa maisha wanaoana ili iweje? Nini maana ya kuoana? Wote wanafokewa na mabosi zao nani wakumfariji mwenzie arudipo?

Wanazaa watoto ili iweje wakati wanamwachia house girl watoto 98% ya muda wote?

Je huyu mwanamke anaezaa na kumwachia house girl analea yeye yuko ofisini muda wote ni mama kweli kwa mtoto au house girl anaelea kutwa kucha ndo mama?

Sijui ndo kupenda kitonga, wanaume wa kisasa wanataka kua kama wanawake wakitaka kuoa wanauliza "mwanamke anafanya kazi wapi?" Full kupenda kitonga na wavivu tabia za kike huku wanawake wanataka kua kama wanaume aise.

Ok pia sijapinga mwanamke kujishugulisha kama anaweza Kufanya hivyo ni vizuri ila SIO KUAJIRIWA kwa mfno mke wangu anasimamia miradi ya familia nilizofungua, sio mwanamke kaajirisha na likampuni gani huko au serikalini. Mume traffic mke mkufunzi wa chuo hii aise hapana.

Mimi mwanamke wa namna hii hanivutii hata punje kumuoa, labda kumtumia na kuachana nae. Mwanamke hafui hata nguo zake mwenyewe, hapiki, ana hela za kwake ana malengo ya kwake sasa huyu anaolewa ili iweje?
 
Hivi kumbe unaoa ili upate wa kukupikia na kukufulia?
Swali langu yote si yanafanyika au unapenda urudi umkute mkeo na mwiko na huku jasho linamtoka kisa kukusongea ugali? Achana na mfumo dume wewe kuwa wa kisasa.................... hata km siendi kazini huko jikoni siingi ng'ooo na nguo pia sitafua utafuliwa na utapikiwa na utakula
 
Wewe kweli miss madeko!
 
Asie taka golikipa liko wazi ni mario, mvivu mpenda kitongm ukiangalia sifa hzo ni za wanawake huyu sio MWANAUME ndo maana anatafuta mwanaume aolewe nae.
Umejifunga ktk mawazo yako mwenyewe na siyo kosa.
 
Duhh wew kweli madeko
 
Pointi kubwa hapo ni kumwachia House G mtoto muda mwingi.Hili ni bonge ya bomu.Ingawa kuna wazazi wengine ni heri wawe wanasaidiwa malezi na House G maana maadili sufuri.
 
Kila kitu kina faida na hasara. Hasara ni nyingi kwa kuoa goli kipa. Ungepata bahati ya kufa na baada ya miaka 5 ufufuke na ushuhudie familia yako ambayo mke alikuwa goli kipa, mengi ya kwenye Uzi huu usingeandika.
 
Hivi kumbe unaoa ili upate wa kukupikia na kukufulia?
Swali langu yote si yanafanyika au unapenda urudi umkute mkeo na mwiko na huku jasho linamtoka kisa kukusongea ugali? Achana na mfumo dume wewe kuwa wa kisasa.................... hata km siendi kazini huko jikoni siingi ng'ooo na nguo pia sitafua utafuliwa na utapikiwa na utakula
Hayo ni maoni yake na ww ni maoni yako , kila mbuyu na shetani wake ,
Sema badilika kidogo

Acha kudeka
 
Duuu kama mzazi maadili sifuri, house girl ndo anamaadili ?
Mifano ulotoa hapo ni tabia mkeo alizo nazo (hata kama umesema anasimamia miradi yenu)
unakuja hapa kupotosha watu ati kuna haja kuoa? Kuna vitu mke anafanya wewe hufanyi Wewe unazaa?
Hivi mwanamke kuwa na kazi inamaanisha asifanye majukumu yake? Kama mkeo hafanyi pole yako. Wengine wanafanya.

Mke anaefanya kazi lazima chakula cha usiku apike yeye. Lazima awe na tabia ya kuamka sa11 ili aandalie mtoto uji , chai ndo aende kazini.

Lakini pia weekend usafi lazima afanye afue apange nyumba na kupika chakula cha tofauti na siku zote maana ndo anakuwa na muda wa kutosha.
Mtu kama alizoea kufanya kazi za nyumbani kazi ya kuajiriwa haiwezi kuwa kikwazo.

Sema wenye bahati mbaya wanakutana na ma slay queen basi wanahisi wanawake wote wako hivyo.
Dada wa kazi siku zote ni msaidizi. Kama mm ambae sipendi wadada wa kazi sijui itakuwaje nikilazimika kuwa nae? mm sipendagi mtu kunifanyia kazi yeyote na akifanya isiwe na kasoro.
Naamini mpaka mtu akubali kuwa mke wa mtu anajua majukumu yake.
 
Maelezo haya yanafanana sana na elimu yetu ya TZ. Field na darasani ni mbingu na ardhi.

Kama kuna aliyebahatika kuwa na mke wa namna hiyo, hakika hatokufa.
 
Hivi kumbe unaoa ili upate wa kukupikia na kukufulia?
Swali langu yote si yanafanyika au unapenda urudi umkute mkeo na mwiko na huku jasho linamtoka kisa kukusongea ugali? Achana na mfumo dume wewe kuwa wa kisasa.................... hata km siendi kazini huko jikoni siingi ng'ooo na nguo pia sitafua utafuliwa na utapikiwa na utakula

Mfano mzuri wa mwanamke wa Instagram na Facebook ndio huyu...! Type za akina Joyce kiria..! Hawa wanaendana na akina mario tu.
 
Ukiona unapenda wali maharage..haimaanishi watu wote tupende wali maharage...Wengine tunapenda UGALI tembele.
 
Hivi kumbe unaoa ili upate wa kukupikia na kukufulia?
Swali langu yote si yanafanyika au unapenda urudi umkute mkeo na mwiko na huku jasho linamtoka kisa kukusongea ugali? Achana na mfumo dume wewe kuwa wa kisasa.................... hata km siendi kazini huko jikoni siingi ng'ooo na nguo pia sitafua utafuliwa na utapikiwa na utakula
Ntamkula na mpishi kudadeki.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom